Mbinu za kupata mitaji ya biashara

Habari wana jukwaa hili pendwa,
Nimekuja tushare mbinu mbalimbali za kupata mitaji ya kufanyia biashara mbalimbali
Wengi wetu tumekua tukihaha kutafuta mitaji ya kufanyia biashara na ujasiriamali
Wengi wameshindwa kukopa mabenk hususan mikopo midogo kwa sababu ya kukosa vigezo kama dhamana n,k
Suali jee tunawezaje kupata mitaji ya kufanyia biashara mbalimbali?
Karibuni tujadiliane tupate maarifa
BAADA YA KUJADILIANA INAKUWAJE! HALAFU NISIVYOPENDA KUSHAULIWA! KAMA BENKI HAWAKOPESHI NA NIMEWAAMBIA WASIKOPESHE MTAFANYAJE
 
Kama una afya nzuri ya mwili na akili kijana usiye na ajira unaweza kupata mtaji mdogo wa kuanzia, shida kubwa wengi wanafikiria kuanza na mamilioni, mimi nakupa wazo, kama huna ajira utakuwa unaishi kwa kutegemea mtu mwingine, ukiwa na uwezo wa kula na kulala bila kulipa anza kutafta vibarua, tunza pesa usitumie hadi ufikie malengo, tazamia miradi midogo inayofanywa maeneo yako, iga kama hunauwezo wa kubuni, utapata faida na faida hy itakupeleka kwenye lengo!nguvu zako ni mtaji na aibu yako ndiyo kikwazo kikubwa! Jishushe ipo siku utapanda
 
Back
Top Bottom