Mbinu za Kulinda Faragha Yako Mtandaoni

Mbinu za Kulinda Faragha Yako Mtandaoni

Ntwa A. Katule

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
239
Reaction score
230
Siku zinavyozidi kwenda suala la faragha (privacy) mtandaoni limeanza kupotea na watumiaji wengi wa mtandao hawafahamu kwamba faragha zao wanapotumia mtandao zipo hatarini kuingiliwa. Naweza nikazitaja moja ya faragha chache ambazo huwa tunakuwa hatarini ila hatufahamu.

Watu huwa wanajua kutumia nywila (password) pekee kutawafanya wawe salama mtandaoni. Nywila haizuii mtu kuingilia faragha yako ya kujua kama ni mitandao (website) gani unapenda kutembelea na huwa unapenda kuangalia nini kwenye hii mitandao. Kitu kingine ni kwamba, tunapokuwa tunaperuzi mtandao inabidi tuwe na anuani (IP Address) inayotufanya tuweze kuwasiliana na vyombo vingine vya kieletroniki. Sababu ya kuongezeka kwa vyombo vya kielektroniki iliamuliwa kwamba vifaa vikiwa ndani vitumie anuani ya binafsi (private IP address). Na vikitoka nje uya mfumo wa yule anayekupatia huduma basi vitumie anuani ya umma (public IP address) kujitambulisha sababu anuani ya binafsi haitambuliki.

Ili uweze kuelewa huu muktadha wa anuani ya umma na binafsi, tuangalie mfano unaofanana na huu upande wa barua zinazotumwa kwa posta. Tufanye wewe ni mfanyakazi wa NSSF tawi fulani na unayo ofisi pale NSSF, ambayo ipo chumba namba 102, kwa mfano. Barua zako zinapotumwa huko zinapotoka, hazitumwi kwa anuani ya chumba namba 102, bali zitatumwa kwa anuani ya NSSF. Zikifika zitapokelewa na watu wa Masijala ambao watakuletea kwenye ofisi namba 102. Kwa hapa anuani ya NSSF ni ya umma, na anuani ya ofisi namba 102 ni ya binafsi kwa maana inatumika na kueleweka ndani ya NSSF. Na pengine NSSF wanakuwa na anuani moja ya umma. Na hivyo ndivyo mifumo ya kielectroniki nayo hufanya kazi.

Unapotumia mtandao uwe wa shirika au uwe ni wa kupitia kampuni za mawasiliano, wao watakupatia anuani ya binafsi lakini wakati mawasiliano yako yanaenda nje yatatafsiriwa kwamba yametoka kwenye anuani ya umma (public IP address), na wataokujibu watatumia anuani hiyo hiyo ya umma kukujibu. Lakini mawasiliano yako yakifika kwa anayekupatia huduma mfano Vodacom, wao wanajua wewe mwenye kujibiwa unatumia anuani gani ya binafsi ukiwa ndani. Hiki kitu kwa lugha ya kitaalamu wanaita Network Address Translation.

Sasa tuje kuangalia ni jinsi gani faragha yako inaweza kuingiliwa na tutamalizia kwa kutaja mbinu moja au mbili katika nyingi ambazo unazoweza kutumia katika kulinda unachofanya kisihusishwe na anuani yako ya faragha au ya umma. Hapo juu nimedokeza kwamba , anayekupa huduma ana uwezo wa kujua wewe unatumia anuani gani kwa ndani na kitu gani huwa unafanya kwenye mtandao. Mfano ukiingia Jamii forums, wao wana uwezo wa kuona anuani gani ya umma unatumia. Na watajua hiyo anuani ni ya kampuni gani. Kama wanataka kufuatilia zaidi wanaweza wakaenda kwa mtoa huduma wako na kumbu kumbu ya vitu ulivyovifanya wakapatiwa utambulisho (identity) wako halisi, sababu wanaokupa huduma wanaufahamu. Sijui kisheria limekaaje kama linawezekana au haliwezekani lakini mimi lengo langu ni kukuonyesha jinsi linavyowezekana kitaalamu. Utekelezaji wa sheria unategemeana na matakwa ya wawili wanaojadiliana katika upatikanaji wa utambulisho wako.

Mapendekezo yangu rahisi ya jinsi ya kujilinda ni kutumia vitu vinajulikana kitaalamu kama VPN, Proxy na vinginevyo. Pia zipo web browser ambazo zinakuwezesha wewe kutembelea mitandao na kulinda faragha ya utambulisho wako. Mfano ni browser inaitwa TOR.

Kwa leo ningependa kuishia hapa na ningependa kukaribisha maoni, maswali n.k.

Mr ICT Guru
www.facebook.com/mrictguru/
Instagram: mrictguru
 
Kuna software huwa naitumia kwenye pc huwa inabadili mpaka location, lakini kwenye simu nimefuatilia nyingi hazibadili location, je kunayo app inayoweza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tor wana browser ya Android inaitwa Orbot inayofanya uwe anonymous wakati wa kusurf. Labda ungeijaribu hiyo. Kwa PC Tor could be the best. Ndo software inayotumiwa hadi na watu wanatembelea deep web ili kuondoa alama za wanamopita wakati wa kusurf
 
Mkuu hiyo mbona mie nmeweka inansumbua sanaa dizain kama ni domain au?
 
Mapendekezo yangu rahisi ya jinsi ya kujilinda ni kutumia vitu vinajulikana kitaalamu kama VPN, Proxy na vinginevyo. Pia zipo web browser ambazo zinakuwezesha wewe kutembelea mitandao na kulinda faragha ya utambulisho wako. Mfano ni browser inaitwa TOR.

Kwa utaratibu huo huo hata hizi unazotaja hazina tofauti na ulichosema. Sijajua vizuri kwenye issue ya dark web. Lakini hata huko, nafikiri anatekupatia access ya dark web, basi ndiye atakayejua unachofanya.

Na zaidi ya ulichokiongea, mpaka karibu gadgets zote za kidigitali zina unique numbers ambazo zinajitambulisha kwenye mitandao. Mfano, wasipokufahamu kwa njia ulioelezea, wataangalia kifaa hicho alinunua nani na wapi na anaishi wapi, ila kwa Bongo yaweza kuwa ngumu kidogo.
 
Nadhani tunaongea vitu viwili tofauti. Nazungumzia your web activity using a browser. Not device identities or any other apps. Using TOR software your service provider hawezi jua unapenda kutembelea site gani. Admin wa Jamii forums hawezi jua una surf mtandao unatokea kwenye network gani na mengi neyo mengi. Ukiwa unatembelea deep web hakuna atayeweza jua your location, your public IP address na kadhalika.
 
Subscribed. Nitajaribu hiyo Tor nione.
 
Siku zinavyozidi kwenda suala la faragha (privacy) mtandaoni limeanza kupotea na watumiaji wengi wa mtandao hawafahamu kwamba faragha zao wanapotumia mtandao zipo hatarini kuingiliwa. Naweza nikazitaja moja ya faragha chache ambazo huwa tunakuwa hatarini ila hatufahamu.

Watu huwa wanajua kutumia nywila (password) pekee kutawafanya wawe salama mtandaoni. Nywila haizuii mtu kuingilia faragha yako ya kujua kama ni mitandao (website) gani unapenda kutembelea na huwa unapenda kuangalia nini kwenye hii mitandao. Kitu kingine ni kwamba, tunapokuwa tunaperuzi mtandao inabidi tuwe na anuani (IP Address) inayotufanya tuweze kuwasiliana na vyombo vingine vya kieletroniki. Sababu ya kuongezeka kwa vyombo vya kielektroniki iliamuliwa kwamba vifaa vikiwa ndani vitumie anuani ya binafsi (private IP address). Na vikitoka nje uya mfumo wa yule anayekupatia huduma basi vitumie anuani ya umma (public IP address) kujitambulisha sababu anuani ya binafsi haitambuliki.

Ili uweze kuelewa huu muktadha wa anuani ya umma na binafsi, tuangalie mfano unaofanana na huu upande wa barua zinazotumwa kwa posta. Tufanye wewe ni mfanyakazi wa NSSF tawi fulani na unayo ofisi pale NSSF, ambayo ipo chumba namba 102, kwa mfano. Barua zako zinapotumwa huko zinapotoka, hazitumwi kwa anuani ya chumba namba 102, bali zitatumwa kwa anuani ya NSSF. Zikifika zitapokelewa na watu wa Masijala ambao watakuletea kwenye ofisi namba 102. Kwa hapa anuani ya NSSF ni ya umma, na anuani ya ofisi namba 102 ni ya binafsi kwa maana inatumika na kueleweka ndani ya NSSF. Na pengine NSSF wanakuwa na anuani moja ya umma. Na hivyo ndivyo mifumo ya kielectroniki nayo hufanya kazi.

Unapotumia mtandao uwe wa shirika au uwe ni wa kupitia kampuni za mawasiliano, wao watakupatia anuani ya binafsi lakini wakati mawasiliano yako yanaenda nje yatatafsiriwa kwamba yametoka kwenye anuani ya umma (public IP address), na wataokujibu watatumia anuani hiyo hiyo ya umma kukujibu. Lakini mawasiliano yako yakifika kwa anayekupatia huduma mfano Vodacom, wao wanajua wewe mwenye kujibiwa unatumia anuani gani ya binafsi ukiwa ndani. Hiki kitu kwa lugha ya kitaalamu wanaita Network Address Translation.

Sasa tuje kuangalia ni jinsi gani faragha yako inaweza kuingiliwa na tutamalizia kwa kutaja mbinu moja au mbili katika nyingi ambazo unazoweza kutumia katika kulinda unachofanya kisihusishwe na anuani yako ya faragha au ya umma. Hapo juu nimedokeza kwamba , anayekupa huduma ana uwezo wa kujua wewe unatumia anuani gani kwa ndani na kitu gani huwa unafanya kwenye mtandao. Mfano ukiingia Jamii forums, wao wana uwezo wa kuona anuani gani ya umma unatumia. Na watajua hiyo anuani ni ya kampuni gani. Kama wanataka kufuatilia zaidi wanaweza wakaenda kwa mtoa huduma wako na kumbu kumbu ya vitu ulivyovifanya wakapatiwa utambulisho (identity) wako halisi, sababu wanaokupa huduma wanaufahamu. Sijui kisheria limekaaje kama linawezekana au haliwezekani lakini mimi lengo langu ni kukuonyesha jinsi linavyowezekana kitaalamu. Utekelezaji wa sheria unategemeana na matakwa ya wawili wanaojadiliana katika upatikanaji wa utambulisho wako.

Mapendekezo yangu rahisi ya jinsi ya kujilinda ni kutumia vitu vinajulikana kitaalamu kama VPN, Proxy na vinginevyo. Pia zipo web browser ambazo zinakuwezesha wewe kutembelea mitandao na kulinda faragha ya utambulisho wako. Mfano ni browser inaitwa TOR.

Kwa leo ningependa kuishia hapa na ningependa kukaribisha maoni, maswali n.k.

Mr ICT Guru
www.facebook.com/mrictguru/
Instagram: mrictguru

tor ina leak data vizuri tu.Hzo relay unazoziona kuwa packets zako zina bounce bounce tu unakuwa unafurahi ip address yako ina change kutoka tz mpaka russia unadhan nani ni admin wa hzo system ? Alf as a matter of fact ile relay node ya mwisho ya kwenye tor network ambayo packet yako ina exit tor mpaka kwenye website husika data haziwi encrypted na guess what asilimia kubwa ya hzo exit node kama wa wale wa ku access USA based sites ni za NSA kwa hyo solution yako cyo efficient. Pia unasahau kuwa computer ni system na kuna components nyingi tu zina atumia IP address yako ku communicate na computer zengine. Tor only works with user based sofware lakini sytem components kama services za microsoft yani TOR haihusiki kabisa.Browser ndo kabisa feedback reports
 
Em mi nianzie kuuliza hapa umesema kuficha au kuweza kuzuia kuona unachofanya kwene mtandao yani Browser, Hio tor inafanya vyote Automatically au kuna setting inabidi uzifanye....
Na vipi kwa simu unaweza kutumia software gani nashukuru nimeona android ni orbot vip kwa other version na pia kwa hiyo orbot unaweza ukaifafanua kidogo....Asante
 
tor ina leak data vizuri tu.Hzo relay unazoziona kuwa packets zako zina bounce bounce tu unakuwa unafurahi ip address yako ina change kutoka tz mpaka russia unadhan nani ni admin wa hzo system ? Alf as a matter of fact ile relay node ya mwisho ya kwenye tor network ambayo packet yako ina exit tor mpaka kwenye website husika data haziwi encrypted na guess what asilimia kubwa ya hzo exit node kama wa wale wa ku access USA based sites ni za NSA kwa hyo solution yako cyo efficient. Pia unasahau kuwa computer ni system na kuna components nyingi tu zina atumia IP address yako ku communicate na computer zengine. Tor only works with user based sofware lakini sytem components kama services za microsoft yani TOR haihusiki kabisa.Browser ndo kabisa feedback reports
Sijaongelea kuhusu efficiency. Ila kuwa na privacy ya kiasi fulani na kutokuwa na privacy kabisa ipi ni bora? Hakuna system ambayo ipo secure kwa asilimia mia. Concept ya security inajengwa na trust ya users. A system that is perceived to be secure by one person may not be perceived as secure by another person. Tuongelee tu layman wa kawaida ambaye anataka tu kuongeza faragha yake na tusiongelee mtu ambaye ni high profile. Kwa mtu wa kawaida a software like TOR inaweza ikampa privacy kutoka kwa watu ambao sio sophisticated. The data may be leaked by TOR. LAkini mtu kama wewe wa kawaida una mbinu zozote za kua access hizo data, tuache stori za NSA na hao Big fish. Tuongelee kampuni kama ya Voda. Can it access that information? Au can jamii forums know you identity? Hapo ndo ilipo concept yangu ukizingatia watu wengi humu wanatumia ID za kujificha. Je ikatokea siku moja Jamii Forums ikapewa amri ya ku release IP? wangapi watasalimika walio nyuma ya Fake IDS? Kwa nini tu tusijaribu kijilinda hata kama ni kwa sehemu ndogo kuliko kutojilinda kabisa?

Na solution ambazo wewe unasema ni efficient ni zipi? Are they free available kwa mtu wa kawaida? Let's just be realistic kwa kujaribu ku discuss in relation to our context.
 
Nice ila trace kupitia ip address kwa Tz bado sana ila vpn ipo safe sana na kuna apanzo za change ip kila baada ya dk kadhaa na kwa watumiaji wa android unaweza tuMia vpn na fake gps .

Kuwa na privacy ya kiasi flani ni sawa sawa na kujifunika nguo mbele huku watu wanakuona uko uchi nyuma.Local companies zinashirirkiana na big companies kwahyo usidhan tu ya kuwa local security ya kujilinda na voda na jamii forums inatosha.Endelea kutafuta solution nzuri ila hapo juu ume blunder kabisa no reasonable argument
 
Nice ila trace kupitia ip address kwa Tz bado sana ila vpn ipo safe sana na kuna apanzo za change ip kila baada ya dk kadhaa na kwa watumiaji wa android unaweza tuMia vpn na fake gps .

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu Tanzania bado hawajawa sophisticated kwenye Ku trace IP kwa hiyo ni rahisi kuwa elude for the time being. Na sasa hivi nadhani ambacho jamii forums wanapigana nacho ni hili suala la IP address za watumiaji wa ID mbali mbali.
 
Ni software gani hiyo?
Fake gps app ipi playstore unauwezo wakuchange gps ya phone yako ikasome eneo lolote utakalo ww ila unatakiwa unable mock location check hizi picha mix na vpn:
8f9110beb4dc449e53345cc5a9b38acf.jpg
c344121f86e2ecf717447ea1d5fd6cdd.jpg
06478b1d787c5423eb6a84093350d652.jpg
 
Back
Top Bottom