Mbinu za ccm kuua upinzani

PAFKI

Senior Member
Sep 30, 2011
116
38
Mungu awabariki,Napenda nizungumze wazi nionavyo mimi na wenye akili wataniunga mkono kwa hili,Hebu kumbukeni CCM ilitumia mbinu gani kuidhoofisha NCCR, CUF na sasa CHADEMA pindi vinapotokea kuwa na nguvu za wananchi,
1. Nakumbuka CUF waliitangazia udini na mapanga ikaonekana ni wahuni na wanahatarisha maisha ya watanzania baadae wakatengeneza serikali ya kitaifa Zanzibar na sasa unaona kilichotokea.
2. Sasa wameanza CHADEMA ina udini,vikundi na mengine mengi tu lengo ni kukifanya wananchi wakichukie
Sasa basi popote muwapo waelimisheni wananchi kinachoendelea na kilichowahi kutokea kwa wengine,hii inaniuma sana mm na ningekuwa na uwezo ningewaelimisha ili hawa mafisadi na chama chao watupishe wa2achie nchi ye2.
 
yes hz ni mbinu zao ila wanajisahau wanajiingiza wenyewe kwny udini ie. Dc Igunga na uislamu, wanajitahd sn kuidhoofisha cdm lln wamechelewa kwani watanzania wameamka na hawapumbazwi tena
 
chadema kamwe hakitakufa kwa ajili ya ccm,hata hivyo wananchi weng wameshajua ipi mbich na ipi mbifu dont give up CHADEMA!
 
Kwa hizo mbinu za kilongi 'old tricks' hawampati mtu,kumbuka leo ni karne ambayo hata kipofu anaona na kiziwa anasikia,enzi za ugoro zimeisha watu wanakula unga,enzi za fulani zimeisha sahivi ni watu wanasemaje...enzi hizo kuna shule moja wilayani lakini leo ni kila kata....kwani ni mangapi yamesemwa kwa CDM? Kwani mangapi wamefanyiwa CDM?sasa la udini tu?walisema uchaga,wakawaita wahuni,wakasema cha msimu,wakasema ukanda,wakasema udini,wakasema mke wa mtu n.k ....watasema na watafika mahala wataacha tu,usihofu sie wengine tulikunywa maji ya bendera ya Tanganyika,unaijua?

Tatizo ccm hawataki kuelewa,watanganyika wamechoshwa na chama hiki,washangae pamoja na skendo zote hizo CDM ina watu mpaka hatujuani hata kwa idadi
 
What goes around comes around! Upepo wa kudai haki katika nchi za kiarabu baada ya kukandamizwa kwa muda mrefu kwa hakika ipo siku utavuma tu kuelekea Tanzania.Kama ccm wanadhani vitisho na kutumia mabavu ndio njia ya kuzima midomo ya wanaopigania haki kwa hakika wamechemka.
 
Back
Top Bottom