Mbinu mpya za wanawake wa siku hizi wanaosaka ndoa kwa nguvu..Ni noma sana

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,924
3,904
Siku ya kwanza atakuja na chupi 2, moja anaifua anaacha bafuni,nyingine anavaa asubuhi anaondoka...
Siku ya 2 anakuja na khanga,anaivaa usiku,asubuhi anaianika nyuma ya mlango anaondoka...

Siku ya 3 anasahau pete na hereni juu ya meza anakwambia 'Hny nitunzie nimesahau hereni zangu mezani

Siku ya 4 anakuja na nguo 2 na vipedo vya kubadilisha na viatu pea 2,anavua high heels anaweka kwenye Shoe rack,asubuhi anaondoka na flat shoes kwenda chuo. Baada ya mwezi chumba chako kinakuwa na vitu kadha wa kadha,na ole wako uvihamishe alipoacha,kesi zinaanza...

Hao ndo Wanawake wa kileo,akija na begi zima si utamuuliza Vipi mwenzangu na utamkimbiza...Anahamia taratibu.. Mwisho wa siku dressing table yako iliyokuwa ina perfume na mafuta ya Rays inakuwa imejaa hereni na 'Foundation'...

My Brother,huna haja ya kuuliza,NDO KASHAHAMIA HUYO....
Kifuatacho utaambiwa,''Honey I miss my days',Zamani nilijua ni Simu za mkononi tu ndo zina Missed Calls, Siku hizi kuna Missed days,ukiambiwa hivi tu jua imekula kwako, inawindwa ndoa hapo...
 
Hao ni wanawake wasiojitambua na wanaenda kwa wanaume wasiojitambua,,,,mwanamke anayejitambua hayuko hivyo na mwanaume anayejitambua hawezi fanya upuuzi huo hapo juu.
Wapenda bei chee, na kuachana ni sekunde.
Unahatishaje kuoa/kuolewa?
 
Kuna kijana jirani yetu amekumbwa na mkasa kama unaosimuliwa na mtoa Uzi! Kijana alipoambiwa "sijona siku zangu" akaja juu akamwambia ondoka ukazitafute! Binti kang'ang'ania ndani! Piga piga na wewe! MTOTO hasikii akasema niulie humu humu!
Kijana akaamua kuikimbia nyumba kwa muda lakini haikusaidia! Sijui mwishoni itakuwaje!
 
Pia kuvaa kanga moja kutwa, kuchotea maji kwa jirani huvaa hiyo, kwenda kwa mangii hiyoo, kama ndo mambo yenyewe ndo hayo mahari mtajilipia wenyewe
 
Muda anafanya hayo yote alafu unamchekea ,what do you expect???

Kukaa kimya kimtaa mtaa tuna-assume umekubaliana na kila kitu
Mda mwingine inatokea tu..Ukiangalia wanaume wavivu kufanya kazi za nyhumbani basi unaona bora umepata msaada ila ndo hivyo mwisho wa siku ndo kama hivyo tena
 
Back
Top Bottom