Mbinu Mpya za kuipa CCM Ushindi wa Kishindo

Mbinu Mpya za kuipa CCM Ushindi wa Kishindo

Basil Lema

Member
Joined
Jan 20, 2013
Posts
86
Reaction score
277
Wakuu Amani iwe nanyi

Nimekamata barua kutoka kwa mmoja wa watendaji wa kata ya Longuo. Barua hii inatoa maagizo kwa wakazi kwenye regista mpya. Kwa kujibu wa barua hiyo ni wale tu walioandikishwa katika regista hiyo ndiyo watakaopiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2014.
Mwisho wa kuandisha ni Tr. 31/1/2014.

Wakuu ikizingatiwa kwamba wanaojuazoezi hili ni maafisa watendaji, madiwani na wenyeviti wa vijiji na mitaa na kwa kuzingatia kwamba CCM ndo wenye madiwani na wenyeviti wengi wa vijiji, basi uandikishaji huu ambao ni wa siri utafanyika kwa namna ambayo utakinufaisha Chama Cha Mapinduzi.

Shime wapenda haki na demokrasia tushirikiane kupiga kelele ili haki itendeke. Inakuwaje kuwa na madaftari mawili ya wapiga kura?
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    595.8 KB · Views: 858

Mkuu shukurani kwa taarifa.

Nadhani pale CDM makao makuu watakuwa na habari!
Any way kuna haja ya CC
. Kurugenzi ya Habari
 
Hii nchi mpaka tupigane mapanga ndipo heshima itakapo kuwepo,yaani vitu vinavyofanywa na hii serikali ni vya kihuni kihuni tuuu!!!Mh.Lema anasema dawa yao ni kuwa muhuni zaidi yao.Huo waraka wa Halmashauri hauna chochote ni utapeli tuuu
 
Chezea CCM weye walipo Mrudisha Mangula nikajua hapa lazima wataurdia strategy zao za miaka ya 1995-2005. Ila Watanzania wa sasa wabishi hao subirini muone.
 
Ccm bwana bado mna ndoto za alinacha mbinu zoote mlizokuwa mkizitumia tushazijua jaribuni tena kuiba kura zetu muone kilichomkuta kibanga.
 
hakuna mtalaamu wa kuikuza hio karatasi tuisome kwa uzuri?
 
Mimi majina ya akina lema sina imani nayo tena hata kama ataandika kitu kizuri kiasi gani.
 
Ccm bwana bado mna ndoto za alinacha mbinu zoote mlizokuwa mkizitumia tushazijua jaribuni tena kuiba kura zetu muone kilichomkuta kibanga.
Mkuu wezi wanajulikana wanaiba wake za watu na magari kama ukitaka kuwajua vizuri ni pm nikwambie zaidi ili kuwajua zaidi.
 
Sante sana mkuu, nimechoka sana na hivi vitu "orodha hii ya wakazi pamoja na mambo mengine ndiyo itakayotumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014..kwa maana hio mkazi asiyekuwepo katika rejista hii hataruhusiwa kupiga kura"
Hiyo uione mkuu

attachment.php
 
Ndugu zangu hili jambo ni la kweli kabisa jana jioni wamekuja nyumbani kwetu na kuandika majina ya watu wote waliotimiza 18+ lakini nilibaki na maswali mengi kwa sababu ile ni kazi ya tume ya uchaguzi!
 
Mnakurupuka ku comment bila ya kupata ukweli wa hiyo taarifa?
barua haina hata muhuri what if mtoa mada alijiandikia mwenyewe halafu akai post.
Au ndio akili za kina CCDMM
 
Hizi habari ni za kweli na ni mbinu chafu ya CCM na serikali yake kutaka kujinufaisha na Chaguzi za Serikali za Mitaa 2014, Kura ya Maoni 2014 kuhusu Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu 2015!!!

Hii inaweka wazi na kuimbua CCM na Serikali yake kwa kukaa kimya kuhusu UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA. Tumesikia juzi EU wametoa kiasi cha Bilioni 80 ambapo katika Fedha hizi kuna za maandalizi ya Uchaguzi wa SM na Uchaguzi Mkuu 2015! Sasa kwanini hawataki kutumia sehemu ya fedha hii Kuboresha Daftari la Wapiga kura???Kwa hesabu za chapchap kuna kiasi cha Watanzania milioni 5.3 wenye sifa za kupiga Kura ambao hawajaorodheshwa kwenye Daftari. Idadi hiihii inalingana na kiasi cha Watu waliosemwa kumpigia kura Rais Kikwete kuingia Ikulu mwaka 2010 kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi!!!

CHADEMA na vyama vingine vyote vya siasa wanatakiwa kulifuatilia jambo hili kwa karibu na kwa umakini mkubwa na kuhakikisha kwamba halifanyiki hata kwa yodi moja! Kama litaruhusiwa kufanyika basi Watanzania wakae wakitegemea kuwa UPINZANI KUINGIA IKULU ITAKUWA NI NDOTO!
 
Ndugu zangu hili jambo ni la kweli kabisa jana jioni wamekuja nyumbani kwetu na kuandika majina ya watu wote waliotimiza 18+ lakini nilibaki na maswali mengi kwa sababu ile ni kazi ya tume ya uchaguzi![/QUOTE

Uchaguzi wa seriali za mitaa hausimamiwi na tume ya uchaguzi ndugu yangu. Unasimamiwa na TAMISEMI kwa hiyo ni kweli wao wana dhamana hiyo ya kusimamia uchaguzi huo. Na ni kweli kuwa daftari la majina ya wakazi wa eneo husika ndio register muhumu kwa uchaguzi huo. Ni kweli pia kwamba umuhimu mkubwa haujawekwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na hili limekuwa tatizo kubwa la ukuzaji wa demokrasia hapa nchini. Uchaguzi wa serikali za mitaa husaidia sana katika uchaguzi mkuu wa Taifa. Ila kwa kuwa vyama vya siasa vingi vya siasa haviwekezi kwenye uchaguzi huo isipokuwa CCM ambayo inajua nafasi ya uchaguzi huo kwenye uchaguzi mkuu wa Taifa.
Nadhani ni wakati muafaka sana uchaguzi wa serikali za mitaa kuondolewa kwenye wizara ya TAMISEMI kwani wizara hiyo haijawahi kulipa zoezi hilo uzito unahitajika. Inawezekana hizo ni miongoni mwa mbinu chafu ambazo hazisemewi.
 
mimi nafanya kwenye serikali za mitaa.suala hili si la kweli.
 
Back
Top Bottom