Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,981
- 45,902
Baada ya zile za kutumia tochi kuonekana kufeli, imeibuka mpya hiyo ambayo si vibaya kuifahamu hata nyie.Kutokana na trafiki kukaa eneo moja kwa muda mrefu bila kubadilishwa, wamekua wakijenga mahusiano na wenye vyombo vya usafiri na usafirishaji, ambapo wahusika huwapatia trafiki pesa siku za weekeend.
Kwa viwango tofauti, wasafirishaji pia huchanga viwango mbalimbali, ili wahusika wanapofika karibia na maeneo ya foleni katika junctions ambazo askari husika hufanya shughuli zake za kuongoza magari, humpigia simu, na mhusika huyaita magari yaliyopo eneo la mteja wake mpaka atakapo maliza kupita.
Unaweza kushangaa kwanini foleni ya eneo flani inakaa sana, na lingine magari yaitwa tu mpaka mnachoka kumbe wennzenu wanawezeshana kwa namna flani.Ni vyema, wahusika wakawa wanawabadili trafiki kila mara katika vituo vyao ilikupunguza mazoea na kutengeneza mianya ya rushwa kama hii.
Kazi kwenu wahusika, raia tunawasaidia tu ili na sisi tusaidike na kadhia ya foleni.