Mbinu chafu wanayoitumia viongozi wengi wa Afrika na hufanikiwa

Chilemba wamela pamputi

JF-Expert Member
Jan 10, 2019
468
486
Habari wanajamvi, kuna mbinu matata ambayo viongozi wengi wa Afrika huitumia kutawala kirahisi saana na bila kukumbana na upinzani wa kiutendaji ndani ya serikali.

Mbinu hii kwa kiasi kikubwa au kwa asili imetokelea huko mashariki ya kati kwa wale wenzetu wakina Shabani.

Mbinu hii ni kama ifuatayo:

1. Unamfuata Waziri Mkuu unamwambia nitakuachia nchi baada yangu.

2. Unamfuata Makamu wa Rais unamwambia nitakuachia nchi baada yangu.

3. Unafuata Spika wa Bunge unamwambia ntakuachia nchi baada yangu.

4. Unamfuata Mkuu wa majeshi unamwambia nitakuachia nchi baada yangu.

5. Unamwendea Waziri wa Mambo ya Ndani unamwambia nitakuachia nchi baada yangu iwe siri yako.

6. Utamwambia IGP nitakuachia nchi baada yangu.

7. Unampigia simu Jaji Mkuu unamwambia ntakuachia nchi baada yangu.

8. Unawaambia majaji wa mahakama kila mmoja kwa muda wake kwamba nitakupatia ujaji mkuu baada ya huyu aliyepo.

9. Unawaambia ma RPC kila mmoja kwa wakati wake nitakuteua uwe IGP baada ya huyu. Iwe siri yako wewe fanya kazi.

10. Utamwambia Katibu mkuu wa chama unachokiongoza ntakuachia nchi baada yangu.

11. Unamwambia Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nitakuachia nchi baada yangu.

Na wengine wengi sambamba na hao. Kiukweli njia hii huwafanya watu wote wasahau weledi na kuvisimamia viapo vya kazi zao huku kila mtu moyoni mwake akiamini kwamba yeye ndiye kiongozi ajaye.

Watu hawa hufanya kazi kwa nguvu zote hata kama zitakuwa zinavunja sheria na kukiuka mipaka ya viapo vyao ili mradi wahakikishe unakuwa salama ili utizimize ahadi zao naadaye.

Kiukweli ni mbinu nzuri saana ingawaje huwaacha wengi na majonzi ya moyo.
Mtawala hufanikiwa saana kutimiza matakwa ya maono yake kwani kila mtu hucheza step alizo buni yeye.

Mwisho tuwe makini watawala wengi wa afrika huitumia mbinu hii kutawala kirahisi saana na pia tumuombe mungu atuepushe mbinu hii isifike nchini kwetu kwni ni mbinu ya hovyo saana. Hii huwafanya wasomi kuabika na kuonekana kama kituko mbele ya jamii.

Ndugu yenu,
Chilemba.
 
Back
Top Bottom