Huo ni Nadina.
Hao jamaa ni talented kweli kweli na wala siyo maigizo. Kama ni Vocal ni Vocal ya ukweli, mtu ananata na beats ananoga na kukolea kushingo.
Hapo hujaweka Beyanga, bado Nakei Nairobi (sisi tulikuwa tunaimba twende Nairobi, tukamwona baba Moi), uje uweke Nadina halafu malizia na Mazili Mazili pamoja na Shauri Yako. Aiseeeee Mama Mbilia Bel anajua sana uje ujumlishe na umbo lake na kasura kake kale kabla hajaanza kutumia mkorogo aise huchoki kumwangalia ndo maana mzee mzima Tabu Ley Rochereau alijichukulia kifaa.kweli kabisa Masuke mfano kitu kama boyaye kuanzia mpangilio wa sauti mpaka ala imetulia sana mpaka huwa najiuliza sana hivi hawa watu ilikuwa ni uwezo binafsi au walikuwa na maproducers wazuri sana?
nikusahihishe kidogo papa mopao wimbo wa monica aliimba ndala kasheba, kama utakukumbuka vizuri ilikuwa ni kesi ya kanga na muhusika alilimbilia zambia
Hivi Cindy wa Koffi anawafikia hawa manguli?
Ni jokes tu mkuu,nawajua vizuri Sana...haitoshi tu kukaa kimya watafute na uwasikilize ndo utajua walikuwa ni wanamuziki wa wa aina gani
Braza kwa sound kama mulugo vile katika ubora wake!! Ahahahha mpaka miti nayo inapiga soukous!?
Sidhani kana walikuwa na maproducer wazuri sana ila walikuwa talented sana. Mfano sauti ya Mbilia Bel katika nyimbo kama Nakei Nairobi, Beyanga nk haina mfano wake.
Kuna wimbo aliuimba mara mbili kwa lingala na baadae kiswahili sijui unaukumbuka mkuu? Nakumbuka maneno kadhaa ya wimbo huo kama "majani, vidudu.......kazi ya binadamu" .
nadina hiyoo
kati ya hao wawili wimbo karibu yangu ameimba nani?