Mbezi Beach hakuna umeme toka asubuhi

Mbezi Beach hakuna umeme toka asubuhi

Sasa baada ya kukujibu ndo ungewauliza wanakataje bla taarfa? Ila chakushangaza umebaki kushukuru kwnye majukum yao,, next time utakatiwa wiki nzma af watakuja kusuruhisha humu JF af mambo yataisha, usiwe msahaulifu wa maumiv kimaendleo TANESCO sio baba zako
Mkuu Goodluck, mbali ya kuungalia upande mmoja wa shukurani zangu kwa TANESCO waliponijibu na kuonyesha uungwana wa kujibu malalamiko yangu, ni vyema pia ungealia upande wa pili wa hitimisho langu.

Nilimalizia kwa kusema; "TANESCO nawatakia kila la heri katika kuboresha zaidi huduma zenu".

Nafikiri nukuu hiyo hapo juu ndiyo ambayo inatoa "summary" kwa kile ambacho unahisi mimi nilipaswa pia kukizungumzia mbali ya kupewa jibu lile. Kuwatakia kila la heri katika kuboresha huduma zao inajumuisha kuhakikisha kuwa wanatimiza jukumu lao la msingi la kutoa umeme wa uhakika kwa wateja wao.

Vilevile hitimisho langu lilijielekeza katika mantiki kuwa pale linapotokea tatizo kama lile wanawajibika kutumia njia mbalimbali za kupashana habari ili waathirika wa kukosekana kwa nishati ya umeme wapate kutambua kwa wakati nini hasa ambacho kinaendelea.
 
Back
Top Bottom