Izato
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 5,084
- 11,005
Leo Alhamisi tarehe 26-08-2021 toka saa 03:00 asubuhi umeme umekatika maeneo ya Mbezi Beach na maeneo mengine ya jirani. Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa pengine zaidi ya ile tuliyoizoea siku zote ya kusema kuwa kuna zoezi endelevu la kubadilisha nguzo za umeme.
Lazima tuseme ukweli ya kwamba katika siku za utawala wa JPM shirika la umeme lilikuwa na utaratibu wenye kueleweka pindi umeme ukikatika. Angalau wadau wote wa umeme walipewa taarifa kuhusu chanzo cha tatizo ambalo limepelekea kukosena kwa nishati hii muhimu.
Sasa tunashuhudia kamchezo kale ka zamani kakirudi taratibu. Hakuna msemaji wa Tanesco ambaye anasukumwa kutoa taarifa pale tatizo kama hili linapotokea.
Ona sasa pamoja na uchovu wote wa kazi, pamoja na hamu ya kuangalia tamthilia ya KULFI sasa ni giza tororo huku wahusika wameuchuna