jijiletublog
Member
- Jul 23, 2020
- 31
- 74
Miradi iliyotekelezwa na inayotekelezwa kwa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2019/2020 katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya ni pamoja na ujenzi wa stendi ya Mbalizi kiasi cha shilingi milioni 150 zilizopelekwa na serikali ya awamu ya tano, SAT.
mradi wa ujenzi wa zahanati katika shule ya wasichana Galijembe milioni 60 zilipelekwa, zahanati hii ni faida kwa wanafunzi, walimu na wananchi kwa ujumla kwani inawarahsishia kupata huduma za afya kwa wakati.
Ujenzi wa ukamilishaji wa soko la tunduma road, Ujenzi wa machinjio ya muda Utengule Usongwe jumla ya shilingi milioni 25 zilipelekwa. Kukamilika kwa ujenzi wa maeneo haya kunawaongezea wananchi fursa ya kufanya biashara katika mazingira salama ikiwa ni kwa wote, wfanyabiashara wakubwa na wadogo.
Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi moja katika shule ya sekondari Usongwe kiasi cha shilingi milioni 10 zilipelekwa. Pongezi ziende kwa raisi wetu JPM na serikali yake ya awamu ya tano Pamoja na watanzania kwa ulipaji wao wa kodi kwani ndiko mafanikio yalikotokea.
Halmashauri ya wilaya ya Mbeya, chini ya uongozi wa raisi JPM katika kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani imeamua kugharamia ujenzi wa soko la Tunduma Road lenye jumla vichanja 521 ili kuwawezesha wafanyabiashara wa eneo hilo kufanya biashara katika mazingira mazuri.
SAT, chini ya uongozi wa raisi JPM imewezesha utoaji wa ruzuku ya msingi kwa walengwa wa TASAF katika vijiji 105 katika kata 28, ambapo jumla ya Tshs. 1,135,452,000.00 zililipwa kwa walengwa 9,460.
Shule ya sekondari wasichana Galijembe iliyopo katika Tarafa ya Tembela, Kata ya Tembela katika kijiji cha Galijembe ilianza kujegwa na wananchi kwa kushirikiana na wadau wafanya biashara kuanzia mwaka fedha 2008 ilipo anza kujegwa shule hii hadi mwaka huu 2019/2020, ujenzi wa shule hii umetumia jumla ya shilingi TSHS. 794,453,610.04 milioni. Pongezi kwa SAT kwa kushirikiana na wananchi katika kulifanikisha suala hili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 27 Aprili, 2019 alifungua barabara ya lami ya Mbeya – Chunya na aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami ya Chunya – Makongolosi, zote zikiwa ni sehemu ya barabara kuu ya Mbeya – Makongolosi – Rungwa yenye urefu wa kilometa 528. Ujenzi wa barabara ya lami ya Mbeya – Chunya yenye urefu wa kilometa 72 umegharimu shilingi Bilioni 140 na ujenzi wa barabara ya Chunya – Makongolosi uliopangwa kukamilika Januari 2020 uligharimu shilingi Bilioni 62.7, fedha zote zimetolewa na Serikali ya Tanzania, chini ya uongozi wa JPM.
UJENZI WA MELI
SAT, chini ya ungozi wa raisi JPM, imehakikisha Ujenzi wa meli tatu zinazogharimu kiasi cha shilingi bilioni 20.1 katika bandari ya Itungi. Ujenzi huo wa meli unatekelezwa na kampuni ya kitanzania Songoro Marine umejumuisha ujenzi wa meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000 za mizigo kila moja na meli ya abiria na mizigo yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo.
Ujenzi wa meli mbili za mizigo za MV Njombe na MV Ruvuma ulikamilika mwezi Julai, 2017 na kusajiliwa na Mamlaka ya udhibiti wa shughuli za vyombo vya majini, (TASAC) na kuanza safari zake za awali kwenda Mbamba Bay Ruvuma na Nkhata Bay nchini Malawi mwezi Septemba, 2017 kwa MV Njombe na Januari, 2018 MV Ruvuma. Na meli ya MV Mbeya II hatimaye ilianza safari zake tarehe 5 october , 2020.