MBEYA: Wawili mbaroni kwa kumuunguza mtoto kwa moto na kumsababishia maumivu

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili Judith Amoni Mwansansu (39) Mkazi wa Mwanjelwa na Aive Alex Swalo (17) Mkazi wa Mwanjelwa Mtaa wa Soko kwa kosa la kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto aitwaye Daines Kefas Mwansasu (06) Mwanafunzi wa Shule ya Awali – Mlimani na Mkazi wa Mtaa wa Soko hapa Jijini humo.

Taarifa ya tukio hilo imetolewa jana tarehe 1 Agosti, 2018 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei.

Akielezea kuhusu tukio hilo kwa wanahabari, Kamanda Matei amesema tukio hilo lilifanyika Jumanne majira ya saa tatu usiku ambapo jeshi la polisi lilipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa raia wema, ya kwamba mtoto huyo amejeruhiwa sehemu mbalimbali kwa moto.

“Inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio mhanga alikuwa ameenda kucheza na rafiki zake na aliporudi nyumbani majira ya jioni ndipo shangazi yake alimuadhibu kwa kumchapa na waya wa umeme sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha na maumivu makali mwilini. Inadaiwa kuwa tarehe 01.08.2018 majira ya asubuhi, watuhumiwa waliendelea kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto huyo kwa kumuunguza kwa moto sehemu za miguuni na kwenye makalio,” ameeleza Kanada Matei.

Kamanda Matei amesema kuwa “Mtoto amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kufanyiwa vitendo vya ukatili na shangazi yake akishirikiana na mtoto wake. Watuhumiwa wote wawili wamekamatwa kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo. Mhanga amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi ya kitabibu.”
 
Kuna watu hawakustahili kuwa Binadamu! Hivi unaona raha gani kumfanyia Binadamu mwenzako, tena mtoto, ukatili wa namna hiyo?
 
Atakayempenda na kumjali mtoto wako ni wewe mwenyewe baba au mama.
Usije ukathubutu kumpeleka akalelewe na ndugu (labda itokee tu) iwe shangazi iwe mjomba, iwe mamdogo au Mamkubwa nk kamwe hawezi kumuweka sawa na watoto wake.
 
Back
Top Bottom