Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Mwanamume ambaye hakutambulika jina lake mara moja amenusurika kifo baada ya kupata kipigo kwa raia wenye hasira kali kwa tuhuma za kuiba Pesa kwenye duka la Jumla jijini Mbeya.
Wananchi waliomkamata kijana huyo ambaye alikiri kuhusika tuhuma hizo za wizi alisema alikuwa na wenzake ambao walikimbia pasipo fahamika huku akionekana kuiuzongwa na wananchi waneneo hilo ambao wanadai kuwa marakadhaa kumekuwapo vijana wanaofanya uhalifu na kurudisha maisha nyuma.
Muda mfupi baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani humo lilifika na na kuokoa maisha ya kijana huyo ambayo yalikuwa hatarini na kumpakiza kwenye gari na kuondoka naye kwaajili ya mahojiano zaidi na kufahamu sababu za yeye kusadikiwa kuiba pesa duka la jumla.
Hata hivyo haikufahamika nikiasi gani cha fedha kilichokuwa kikiibiwa na Kijana huyo aliyekuwepo na wenzake katika duka hilo.
Chanzo: ITV