Mbeya wahoji uadilifu viongozi wa UKAWA

Babu seya ni mojawapo ya wengi waliokosa Haki ambao wapo magerezani, mtashuhudia maajabu yakiwemo ya Balali kurejeshwa Tanzania, Magufuli kudaiwa zile billion 251 alizolipa makandarasi hewa pale wizara ya Ujenzi pia ukawa wataidai chenji ya vivuko Rada, vivuko, mabehewa Feki, sukari, bomba la Gesi, mgodi wa buzwagi, mgodi wa meremeta, escrow, EPA, chenji iliyobaki baada ya bunge la katiba iliyokataliwa nk

Hujamalizia na MENO ya TEMBO,mpaka watu wameona haiwezekani mpaka kulitwisha JESHI letu uchafu wao.Ni aibu kubwa.
 
Jamani Thread zingine wala si za kuchangia mtu eti anakosoa anakosoa nn?anajaribu kuweka hisia zake na mihemko yake eti wana mbeya wanashangaaa!apeleeee ke hukooo ushabiki VIMA
 
Mgombea wa ccm kuingizwa chumba cha zeluzelu !! huyo sugu alikuwa anamaanisha nini kwa hiyo kauli yake?
 
pwanikwetu,avatar yako inaniambia wewe si Mkaazi wala muendaji wa Mbeya.

Kwa miaka mitano tu ya Joseph Mbilinyi kuwa Mbunge wa Mbeya mjini tumeona mabadiliko makubw akuliko miaka 20 ya Mbunge wa CCM.

Pili hata ukawape Pesa Joseph Mbilinyi anakubalika si kwa vijana tu hata wazee,kwa wakaazi wa Mbeya tunajua historia na siasa za Mbeya !Kuna watu wanaitwa waMwene hawa ndugu wakishakukubali ujue umepata zari la mentali.

Pole labda kama Mbeya unayoisemea wewe ni Msoga kwenye shule za chini ya mti,na Rais anatoka huko,Mbunge Mtoto wa Rais....mkawadanganya na matrecta kila kata,safafri sijui mtawadanganya na nini???
 
raia mwema limenunuliwa kwa kaz maalumu.

raia mwema la sku hizi=raia tanzania=uhuru=jambo leo=mkakati.

yaaaani ni

porojo
mipasho
udaku
matusi
vijembe na
upotoshaji tupu
 
Watu wa Mbeya walishajitambua, hawadanganyiki kama huamini jaribu kucheki na mheshimiwa Weston Zambi.
 
nickname
31st March 2011 16:54
#1 JF Senior Expert Member Array


Join Date : 20th December 2009
Location : Dar es Salaam
Posts : 460
Rep Power : 688
Likes Received19
Likes Given13


[h=2]
icon1.png
Mbowe aiuza CHADEMA kwa Lowassa[/h]
Kuna mpango wa Mwenyekiti wa Chadema Mh.Freeman Mbowe wa kulipwa mamilioni ya fedha ili Viongozi wa Chadema waache kumsema Mr. Monduli kuwa ni fisadi.

Mh.Zitto Kabwe anajitahidi kwa kila hali kuzuia mpango huo

Na Mwandishi wetu | Gazeti la Sauti Huru

Mmoja kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi(jina tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya siri na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe ili kuingia ubia na chama hicho.

Inaelezwa kuwa ,lengo la kigogo huyo ni kukiziba mdomo chama hicho kisimrushie makombora ya ufisadi kama walivyowahi kumrushia siku za nyuma.

Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa kigogo huyo wa CCM amekuwa na mawasiliano ya siri na ya karibu na Mbowe huku vikao vingi vikifanyika ndani ya hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Arusha (jina tunalo)

Imebainika kuwa ndoa hiyo ya siri ni ya wanasiasa hao wawili,lakini ikilenga uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kigogo huyo wa CCM amemuahidi Mbowe kwamba wataunda "serikali ya umoja wa kitaifa" endapo Mbowe atasaidia kuacha kumuandama kwa tuhuma za ufisadi na kuwadhibiti viongozi wengine wa chama chake, kutofanya hivyo kwenye maandamano na mikutano yao ya hadhara, pamoja na kwenye mahojiano na vyombo vya habari.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa tayari kigogo huyo amempa mwenyekiti huyo wa CHADEMA kiasi kikubwa cha fedha ili chama hicho kinapoendelea na kampeni yake ya bomoa-bomoa mafisadi yeye asiguswe kabisa, kama hatua ya kumfikisha ndoto yake ya kutaka chama tawala kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya urais.

Chanzo chetu cha uhakika kikiongea na Sauti Huru kwa sharti la kufichwa jina lake kimedai " huu mpango unafanywa kwa siri kubwa na ninajua hata mhusika (anamtaja) akijua habari hii imetoka atafadhaika sana"


Habari zaidi zinadai kwamba kigogo huyo amefikia hatua hiyo baada ya kusoma alama za nyakati na kuona kwamba uwezekano wa mwenyekiti wa chama chake kumuunga mkono ni mdogo, hivyo hatoweza kupenya katika kinyang'anyiro cha uraisi 2015.

" Huyu bwana amesoma alama za nyakati ,ameona kabisa uwezekano wa kuungwa mkono na mwenyekiti wake(wa CCM) ni mdogo sana hivyo ni lazima atafute njia nyingine hata kama njia hiyo itakuwa na madhara kwa chama chake", kilieleza chanzo hicho na kufafanua;

"Si kwamba hajui mwenyekiti atalalia wapi, anajua lakini yuko tayari hata kukisaliti chama ili wote wakose,hivi ninavyoongea nanyi watu hawa wana mawasiliano ya kila mara juu ya suala hili ila Mbowe kaweka ngumu kuwa lazima waandikishiane ajue kabisa endapo (kigogo huyo atafanikiwa kuingia madarakani basi wataunda government of unity(serikali ya umoja wa kitaifa)".

...Aidha imefafanuliwa kwamba habari hizi zimeweza kumgusa hata Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, lakini kwa namna ya pekee Zitto ameweza kudhoofisha mkakati huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni 'unafiki kwa Mbowe'

"Mtakumbuka siku za hivi karibuni Zitto alishutumiwa na chama chake kwa madai ya kuwa na uhusiano wa mashaka na Idara ya Usalama wa Taifa. Chadema wamekuwa wakidai kwamba Zitto anatoa siri za chama chao nje na hata kumuundia kamati ya wazee kumshauri?" alihoji.

Aliendelea:" Kilichotokea katika kamati hiyo siku walipokutana na Zitto ilikuwa tofauti kabisa, Zitto akawabadilishia mada pale alipowaambia wazee,'jamani ugomvi wangu na Mbowe ni pesa za chama, anatumia chama hiki hiki kupata fedha toka nje ya nchi na ndani ya nchi, lakini ninapojaribu kumkosoa kuwa tabia hiyo si nzuri kwa mwenyekiti wa chama ananijia juu,nyie mnajua kuwa amepokea fedha mamilioni kutoka kwa(anamtaja kigogo huyo) kwa ajili ya kutunyamazisha tusipige kelele za ufisadi dhidi yake?' "

"Hivi hamjui tayari anafanya mazungumzo na mtu wa CCM kwa ajili ya power sharing ya mwaka 2015?"

Kwa mujibu wa habari hiyo ni kwamba kigogo huyo atafanya kila liwezekanalo CCM imteue kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi; lakini anajua hilo litawezekana endapo kelele za ufisadi dhidi yake zitamalizika.

"Huyu mtu ni mjanja sana na kwa sasa ana nguvu na mtandao mkubwa ndani ya CCM unaoweza kumfanya ateuliwe na chama kuwa mgombea, si hilo tu anajaribu hata kutafuta nguvu nje ya nchi ili endapo akikataliwa aweze kuwa na cha kuieleza jumuiya za kimataifa,"

"Na kwa hatua aliyofikia ni kwamba endapo hatoteuliwa hasa kutokana na ufisadi wake,yuko tayari hata chama chake kipoteze nafasi ya uraisi kitu ambacho kinaonyesha kuwa hana sifa za kiuongozi isipokuwa ni tamaa ya utawala."

Source: Gazeti la Sauti Huru

My Take:
Wale viongozi wa Chadema na wakereketwa waliopo humu JF watuthibitishie hii habari kama ni kweli.​

Last edited by nickname; 31st March 2011 at 18:13.
 
Nafikiri huyu mtu aliyeleta huu uzi hajitambui na haelewi. Watanzania sio wa kudanganya tena! miaka CCM iliyokaa madarakani inatosha hatuitaki tena hata iweje! kwa muda wote wamefanya nini? miaka 54 ni mingi sana, tunadanganywa huduma kwa mama mjamzito bure ukienda kliniki ya hospitali ya wilaya unaambiwa hakuna hata SP (dawa ya kukinga malaria) eti tukanunue pharmacy! nini maana ya huduma bure???? Ndugu yangu napenda kukuambia kwamba HATUDANGANYIKI KWA VYOVYOTE VILE. Wewe endelea kubaki na ccm yako sisi tunasonga mbele.. Shida
 
Ukitaka kukwazana na hawa jamaa ongea ukweli unaowahusu,lazima utatukanwa tu. Yaani wao hujiona ni malaika,kila wakifanyacho ni kizuri. Ukiongea baya lao watakwambia unatumiwa,duuuuuh........!!.

Hapo hakuna ukweli wowote...swala la ufisadi kama ni kulihubiri limeshahubiriwa sana na vyama vyote vya upinzani haswa CHADEMA, ccm nao wakaona ndio mtaji wakaanza nao kuimba wimbo huo, japo wao ndio watuhumiwa na hawakuchukua hatua yoyote.

Kwa hali ilivyo jambo halitakiwi kuhubiriwa tena bali kufanyiwa kazi. Historia inaonyesha CCM ni kiwanda cha kutengeneza mafisadi na kamwe haiwezi kupingana(kupambana) na ufisadi.
 
Ukitaka kukwazana na hawa jamaa ongea ukweli unaowahusu,lazima utatukanwa tu. Yaani wao hujiona ni malaika,kila wakifanyacho ni kizuri. Ukiongea baya lao watakwambia unatumiwa,duuuuuh........!!.

Ni kweli, mkuu. Hawana hoja kabisa ila wamejaa matusi tu!!!!!!!
 
Back
Top Bottom