Dim Ray
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 320
- 249
Habari za alasiri wana JF tumshukuru Mungu kwa kutupa uhai. Tujilinde na corona.
Niende moja kwa moja kwenye mada, siku ya leo mida ya saa 9 alasiri nilikuwa narejea nyumbani, nilikuwa naelekea stendi ya daladala, ghafla nikasikia mtu akiniita weee kaka kugeuka nikaona mabinti wawili wamekaa pembezoni mwa barabara mmoja ananyonyesha mwingine yupo tu, lakini kabla hawajaongea chochote kuna mtu mwingine alikuwa ashatukaribia mdada yule ambaye hakuwa na mtoto akasema "tusaidie hela ya nauli" hapo ndo nikagutuka nami nikasema sina, wako vizuri physically, mentally hata mavazi waliyovaa sijui kwanini walikuwa wanaomba hela.
Unaweza sema walikuwa na matatizo lakini siku hii hii ya leo nikiwa maeneo ya Posta hapa Mbeya mjini kuna mdada wa makamu aliniambia kaka samahani naomba mia nikamjibu sina, hii ni kwakuwa nilikuwa naenda kulipia benki na nilikuwa na nauli na pesa ya kulipia benki tu, na hii imetokea mida ya saa 5 asubuhi.
Kiukweli tabia ya kuomba omba hela ni risk unaweza ukakutana na watu wenye roho mbaya wakakufanyia hata unyama pili ni kuji "disrespect" .
Hao mabinti wawili niliowataja mwanzo nilikutana nao barabara inayotokea Iyunga ikielekea Coca-cola karibu na chuo cha MUST.