Mbeya: Polisi wamshilikia Mkazi mmoja kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu Covid-19 katika mitandao ya jamii

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Joyce Kephas Akyoo(31) maarufu kama "Manka" mkazi wa Stereo, kwa tuhuma za kusambaza taarifa za kupotosha kuhusu ugonjwa wa COVID19 katika Mtandao wa Kijamii

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ulrich Matei amesema mtuhumiwa alikamatwa Aprili 27, 2020. Baada ya kupata taarifa kuwa alisambaza taarifa za kupotosha. Mtuhuiwa alituma taarifa za kupotosha kuhusu CoronaVirus Machi 30, katika moja ya kundi la Whatsapp

Kamanda amedai kuwa mtuhuwa alituma picha za marobota ya nguo na alijirekodi sauti akieleza kuwa hayo ni mablanketi yaliyotumika kufunika maiti za waliokufa kwa COVID19 nchini China na yanaletwa Afrika kama msaada, na kuwataka watanzania wasikubali msaada huo

Kamanda amesema, taarifa hiyo ilikuwa ni upotoshaji na upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani
 
Atajua kuwa maharage nayo ni mboga!
 
Back
Top Bottom