Mbeya: Kichaa aua mmoja na kujeruhi wawili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,982
Na Thompson Mpanji, Mbeya

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Said Betwel(27),Mkazi wa Wigamba Kata ya Isanga Jijini hapa anayedaiwa ni mgonjwa wa akili ametiwa mbaroni baada ya kuwashambulia watu watatu na mmoja kumsababishia kifo.

Ametajwa majeruhi aliyefariki dunia wakati akipatiwa matibabu mara baada ya kukimbizwa katika hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya ni Rahabu Mwanjala(70),Mkazi wa mtaa wa Wigamba Kata ya Isanga Jijini Mbeya amefariki dunia baada ya kudaiwa kuchomwa na kisu.

Watu wengine wawili waliojeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya ni pamoja na Nelusigwe Michael Mwanjala(83) na Tupakisyege ambao walitibiwa na kuruhusiwa na kurudi nyumbani.

Aidha mtoto wa Tupakisyege ajulikanaye kwa jina Hilda Mulungu amesema kijana huyo alionekana kuwa na dalili za kuchanganyikiwa ambapo alianza kumkimbiza na kuokolewa na majirani baada ya kupiga kelele.

Hilda amesema kijana huyo aliondoka na kwenda nyumba jirani na kuanza kumshambulia marehemu kwa mawe na kitu chenye ncha kali na kumsababishia majeraha makubwa katika mwili wake.

“Kama haitoshi alimshambulia bibi mwingine aitwaye Nelusigwe na kumsababishia majeraha”amesema.

Mtoto wa marehemu ,Niganile Mwanjala(43) amesema baada ya kupata taarifa za wazazi wake alifika nyumbani na kuwachukua wazazi wake kisha kuwakimbiza hospitali.

Kwa upande wake, Lucas Mwakalonge ambaye ni ndugu ya ya mtuhumiwa huyo amesema kijana huyo alionekana kuchanganyikiwa tatizo lake lilidumu kwa miaka kumi na mara baada ya kupokea taarifa walifika eneo la tukio na kumchukua ndugu yao na kumpeleka hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya.

Fabian Mwakalonge ni kaka yake Said alisema mdogo wake amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa akili na amewahi kulazwa mara tatu katika hospitali ya rufaa.

"Siku ya tukio mdogo wangu alikuwa ni mkali lakini hatukujua kama angeleta madhara kwani mara zote humtokea lakini baadae hutulia,"amesema Fabian huku akionesha vyeti vya matibabu na barua ya Mtendaji ya kuomba msamaha wa matibabu.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kifo hicho na kwamba wamemkamata Said Betwel kwa mahojiano zaidi

Kamanda Matei amesema wagonjwa wa afya ya akili wanapaswa kupelekwa hospitali badala ya kuwaacha wakirandaranda mitaani kwani wakati wowote wanaweza kuleta madhara na kwamba uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hili ni tukio la pili katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja kwa watu wenye matatizo ya afya ya akili kusababisha mauaji.

Awali katika tukio la kwanza kijana huyo mei 19 mwaka huu alimchoma kisu begani bibi yake Tupakisyege Mwalingo(90) mita mia kutoka nyumbani kwa kijana huyo.

Hivi karibuni katika Kijiji cha Nkunga Kata ya Nkunga kijana mmoja alimchinja bibi yake na kutokomea na kichwa chake kwa siku mbili kabla ya kukamatwa na Polisi.
 
Ukiona kichaa anabagua wakumshambulia ujue huyo akili zishaanza kumrejea. Haiwezekani washambuliwe wazee tu
 
Hivi karibuni katika Kijiji cha Nkunga Kata ya Nkunga kijana mmoja alimchinja bibi yake na kutokomea na kichwa chake kwa siku mbili kabla ya kukamatwa na Polisi.
WE UKIONA MJI UNA MADHEHEBU YASIO NA IDADI, POMBE NDIO SODA, MARJUAN NDIO SIGARA, TEGEMEA MANYANG'UNYANG'U NA MATUKIO SAMPULI KAMA HIZI. WANAOISHI HUKO WANATIA HURUMA MH!
 
Back
Top Bottom