Mbeya: Gari la Wagonjwa lapata ajali Magimba, mmoja afariki

Mbeya: Gari la Wagonjwa lapata ajali Magimba, mmoja afariki

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,956
Reaction score
63,762
Mtoto mwenye umri wa miaka 10 wanafunzi wa darasa la pili amefariki dunia baada ya gari ya wagonjwa iliyokuwa ikimpeleka hospitali ya Rufaa mbeya kupata ajali maeneo ya magamba

======

MWANAFUNZI wa Darasa la Pili mwenye umri wa miaka 10, aliyekuwa akisoma Shule ya Msingi Bangwe Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi amekufa papo hapo baada ya gari la wagonjwa kupinduka wakati likimpeleka hospitali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alithibitisha ajali hiyo, lakini hakuwa tayari kutaja jina la marehemu huku akisisitiza kuwa wanamsaka dereva wa gari hilo aliyekimbia baada ya kutokea ajali hiyo.

Lakini kwa mujibu wa Meya wa Manispaa ya Mpanda, Willy Mbogo, gari hilo ni aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili DFPA 3273 ambalo lilikuwa na watu watatu; dereva, mtoto wa kiume, Holo Paliga na baba yake mzazi aitwaye Ngosha Paliga ambaye amenusurika kifo.

Kamanda Nyanda akizungumza kwa simu kutoka Mpanda, alisema ajali hiyo iliyohusisha gari hilo la wagonjwa mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, ilitokea juzi saa mbili usiku katika Kijiji cha Magamba nje kidogo ya Mji wa Mpanda katika barabara kuu inayounganisha miji ya Mpanda na Sumbawanga mkoani Rukwa.

“Gari hilo lililokuwa limembeba mtoto huyo ambaye alikuwa amepatiwa rufaa kutoka Hospitali ya Manispaa ya Mpanda iliyopo Mpanda Mjini kwenda Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya, lilipofika katika Kijiji cha Magamba umbali wa kilometa kumi kutoka mjini Mpanda, liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha mgonjwa huyo,” alibainisha Kamanda Nyanda.

Akifafanua, aliongeza kuwa devera wa gari hilo ambaye majina yake yamehifadhiwa, alikimbia muda mfupi baada ya kutokea kwa ajali hiyo na kukimbilia kusikojulikana.

“Uchunguzi wa awali wa kipolisi umebainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe na mwendo kasi kwa upande wa dereva ambapo gari lilimshinda kukata kona kali na kuacha njia kabla halijapinduka,” alisema.

Alisisitiza wanaendelea kumsaka dereva wa gari hilo ili sheria ichukue mkondo wake.
 
Back
Top Bottom