Mbeya derby:Prison vs Mbeya City

Mbeya derby:Prison vs Mbeya City

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
panapo majaliwa kesho nitakuwepo ndani ya sokoine stadium kushuhudia mtanange wa kukata na shoka kati ya Mbeya city (watoto wa jiji) na Tanzania Prison (wajela jela).

Kiufupi leo kutwa nzima hapa Mbeya mechi hiyo ndio inazumgumziwa sana na kila mtu ana morali ya kwenda kushuhudia kabumbu hilo huku Mbeya City wakionekana kupata spoti kubwa ya wanambeya.

Maeneo yote ya Mbeya kuanzia Igawilo,uyole,Sae,Ilomba,Mama John,Soweto,Kbwe mwanjelwa,Airport,Uhindini,Isanga,Ilemi,soko matola,majengo,Iyunga,Mabatini,Nzovwe na maeneo mengine yametawala rangi za zambarau na nyeupe kuonyesha kuwa wanaisapoti Mbeya City FC.

Wana Mbeya wengi wanaisapoti Mbeya City kama timu ya wananchi na kuichukulia kama ndio mwokozi wao ukilinganisha na Prison ambayo ipo chini ya Jeshi la Magereza,pia wana Mbeya wengi hawaipendi Prisoni na hii ni baada ya miaka ya nyuma Prison kuwahama Wana mbeya na kuhamia Dsm kabla hawajarudi tena mbeya kiyendo kilichowaudhi sana wana Mbeya.

Kwa kifupi mechi itakuwa kali sana na yenye ushindani huku Mbeya city wakipambana kuendelea kubaki katika nafasi za juu upande mwingine Prison wakitaka kujikwamua kutoka katika nafasi za chini.Historia inaonyesha ni Prison ndio waliwafunga Mbeya city katika ligi daraja la kwanza msimu wa 2012/13 (nisahihishwe kama nimekosea mwaka) mechi iliyopelekea Prison kupanda daraja na kuwanyima nafasi Mbeya city kuingia ligi kuu kabla hawajafinikiwa safari hii kuingia ligi kuu na kufanya maajabu.

Sasa je itakuwa ni zamu ya Mbeya City kulipa Kisasi au wataendelea kuwa wateja Prison?ikumbukwe mpaka sasa Mbeya City Fc haijafungwa hata mechi moja.

Stori zote tupige hapa na matokeo pia tupeane hapa.
 
the day has come..Mbeya city stand up
 
Prison wamepania sana , na wanaweza haribu radha ya mechi, kwani hata mechi na kagera walicheza chini ya kiwango eti waje wawatoe nishai Mbeya city , na inaweza kula kwao leo ,, ! Binafsi ntakuwepo na tunawaahidi wanjf wenzetu kuwapa updates zote za mechi ya leo , nshamuona Mlugo wa Mbeya city mjini leo.
 
ila natarajia mechi itakuwa ngumu na yenye ushindani,kila mmoja atataka kushinda akiwa katika ardhi ya nyumbani tena kwa wapinzani wa kutoka mji mmoja.
 
Ngoja tusubirie hicho kipute cha kukata na shoka...
 
Kwa leo itabidi niwasapoti tanzania prison ili mbeya city achapwe kwani hali aliyonayo inatia shaka ubingwa kwa YANGA.
 
Daaah washabiki wa tunduma wanaingia mchini kwa fujoooooooo ?? Hii mby city ishawapa wazimu??
 
jiji la Mbeya limepambwa kwa rangi ya zambarau na nyeupe,magari,bajaji,pikipiki yanapeperusha bendera za Mbeya City,kila kijiwe ni stori kuhusu mechi ya leo,binafsi ndio naelekea uwanjani,wana jf hususani sports forum tukutane pale for more updates
 
ila natarajia mechi itakuwa ngumu na yenye ushindani,kila mmoja atataka kushinda akiwa katika ardhi ya nyumbani tena kwa wapinzani wa kutoka mji mmoja.

nawatakiwa mafanikio Mbeya City
 
Prison team piga hao Mbeya city wakauze mitumba Mwanjelwa
 
jiji la mbeya limehamia sokoine stadium,watu ni wengi na hamasa ni kubwa sana kila mtu ana hamu na mechi ya leo
 
panapo majaliwa kesho nitakuwepo ndani ya sokoine stadium kushuhudia mtanange wa kukata na shoka kati ya Mbeya city (watoto wa jiji) na Tanzania Prison (wajela jela).

Kiufupi leo kutwa nzima hapa Mbeya mechi hiyo ndio inazumgumziwa sana na kila mtu ana morali ya kwenda kushuhudia kabumbu hilo huku Mbeya City wakionekana kupata spoti kubwa ya wanambeya.

Maeneo yote ya Mbeya kuanzia Igawilo,uyole,Sae,Ilomba,Mama John,Soweto,Kbwe mwanjelwa,Airport,Uhindini,Isanga,Ilemi,soko matola,majengo,Iyunga,Mabatini,Nzovwe na maeneo mengine yametawala rangi za zambarau na nyeupe kuonyesha kuwa wanaisapoti Mbeya City FC.

Wana Mbeya wengi wanaisapoti Mbeya City kama timu ya wananchi na kuichukulia kama ndio mwokozi wao ukilinganisha na Prison ambayo ipo chini ya Jeshi la Magereza,pia wana Mbeya wengi hawaipendi Prisoni na hii ni baada ya miaka ya nyuma Prison kuwahama Wana mbeya na kuhamia Dsm kabla hawajarudi tena mbeya kiyendo kilichowaudhi sana wana Mbeya.

Kwa kifupi mechi itakuwa kali sana na yenye ushindani huku Mbeya city wakipambana kuendelea kubaki katika nafasi za juu upande mwingine Prison wakitaka kujikwamua kutoka katika nafasi za chini.Historia inaonyesha ni Prison ndio waliwafunga Mbeya city katika ligi daraja la kwanza msimu wa 2012/13 (nisahihishwe kama nimekosea mwaka) mechi iliyopelekea Prison kupanda daraja na kuwanyima nafasi Mbeya city kuingia ligi kuu kabla hawajafinikiwa safari hii kuingia ligi kuu na kufanya maajabu.

Sasa je itakuwa ni zamu ya Mbeya City kulipa Kisasi au wataendelea kuwa wateja Prison?ikumbukwe mpaka sasa Mbeya City Fc haijafungwa hata mechi moja.

Stori zote tupige hapa na matokeo pia tupeane hapa.
Hongera jiji la Mbeya kwa kuonyesha mfano. Umiliki wa shule2 siyo mchezo. Wapi Mwanza City?
 
Back
Top Bottom