Mbeya: Daud Mwenye changamoto ya Afya ya Akili auawa

Mbeya: Daud Mwenye changamoto ya Afya ya Akili auawa

Kahama- shy

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
2,059
Reaction score
2,921
Wakazi Wa Mtaaa Lumbila Kata ya lwambi jijini wamesherekea vibaya Sikukuu ya Pasaka baada ya Kumka Asubuhi na kukuta kijana Daud Adamson Mwaitebele(23) aliyekuwa na tatizo la afya ya akili na changamoto ya kusikia ameuawa na watu wasiojulikana na mwili wake kukutwa shamba la mahindi mita chache kutoka nyumbani kwao usiku wa kuamkia aprili 20,2025.

Mama mzazi wa marehemu Agnes Lusua amesema marehemu marehemu Daudi alitoka nyumbani majira ya saa 3:00 asubuhi Aprili 19,2025 alikuwa ametumwa kwenda kuuza kuni lakini hukurejea na mjomba wake ndiye aliyerejea na mauzo ya kuni shilingi elfu moja hadi alipopata taarifa za kifo chake.

Balozi wa Mtaa wa Soko Varelian Swai amesema marehemu hakuwa na tabia mbaya wamekuta watu wamemkanyaga na mwili wake ukiwa emeharika.

Matukio ya mauaji yameanza kuibuka tena Mkoani Mbeya pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Jeshi la Polisi kudhibiti vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.

 
Huyo mjomba wake ilikuwaje akarejea na pesa ya mauzo ya kuni akamuacha mpwa wake huko?
 
naomba mwananchi ahojiwe bila kutajwa jina kutakuwa na shida mahali si bure!
 
Back
Top Bottom