Mbeya: Askari Polisi wa wawili wafukuzwa kazi kwa kushambulia wanafunzi

Waliwachukua Wanafunzi wawili wakajifungia nao ndan baada ya 'Msuguano' wakawarudisha bwenini nadhani hili RPC kalificha kunusuru wasifunguliwe kesi ya ubakaji
 
Utaileza nn familia yko na tayar kla ktu washajua [HASHTAG]#shame[/HASHTAG]
 
Tatizo Mwenye nchi anawapa kichwa sana na askari kujiona wapo juu ya sheria..
 
Hao polisi wangepelekwa kusimamia mitihani shule kama Makongo halafu wakaleta huo ujinga unadhani nini kingewapata?
 
Habari ipo hivi;

Askari PC Petro wa FFU Mbeya na PC Lucas wa Pol. (W) Mbalizi, walipanga kulinda mitihani shule ya secondary Isuto. Sasa usiku wa kuamkia jana tarehe 05 wakiwa shuleni hapo ambapo shule hiyo ina bweni la wasichana tu, waliwachukua wasichana wawili wanafunzi wakaingia nao ofisini. Askari mmoja chumba kimoja na binti na mwingine chumba kingine na binti. Wakawa wanawataka watoto hao kimapenzi lakini walikataliwa.

Baada ya kuwalazimisha kwa muda mrefu ikashindikana ndipo wakawafungulia milango warudi bwenini. Na tayari ulikua usiku mwingi. Baada ya watoto kwenda bwenini wakakuta bweni limefungwa wenzao hawataki kuwafungulia. Bahati nzuri kuna dilisha lilikua wazi basi wakatumia dirisha hilo kuingia ndani. Baada ya kufika ndani wenzao wakaanza kuwazomea kitendo kilichozaa kelele nyingi usiku huo.

Sasa hawa askari baada kuona vile wakaenda bwenini wakawatoa wasichana wote nje wakaanza kupiga sana fimbo na adhabu nyingine kama kichura n.k. Wale watoto baada ya kuona mtiti mkubwa wakakimbia na kurudi makwao usiku huo. Ndipo taarifa zikasambaa ikawa tatizo kubwa.

Afande OCD Mbalizi alifika eneo la tukio asubuhi ya jana tarehe 05 na kamati ya mitihan ya Wilaya. Askari hao wamekamatwa na kufunguliwa kesi ya shambulio. Taratibu nyingine za kijeshi zinaendelea na shule wamepeleka askari wengine. Afande Marijani nae yupo kwenye helkopta anakuja kwa jambo hilo nadhani kwa ni ishu nyeti sana ukizingatia mitihani hii ni ya taifa.

Ombi langu: Tuzingatie maadili ya kazi yetu kwani tumejipaka matope sana na askari tumeonekana hatuna maana kabisa.

Nawaomba taarifa hii ibaki humu kwetu kama ambavyo siku zote tunakua wasiri tafadharini sana. Sitegemei kuikuta nje tena. Na mpaka kufikia leo asubuhi ya tarehe 8/11/2016 wamefukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.
Michezo hio uwa inafanyika sana , sema ilikuwa hairipotiwi tu
Tena baadhi ya shule wanafunzi wa kike ndio wanaamua kulala na Polisi kwa lengo la kuwalegeza ili wacheze michezo michafu kwenye mitihani yao
 
Back
Top Bottom