Mbeya: Ajali Miezi Miwili Zasababisha vifo 30

Mbeya: Ajali Miezi Miwili Zasababisha vifo 30

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2022
Posts
9,434
Reaction score
10,970
Watu 30 wamefariki dunia Kutokana na ajali za barabarani Mkoani Kwa muda wa miezi 2 Kwa mujibu wa habari iliyonukukiwa na gazeti.

Tukiwa tunaelekea mwishoni mwa mwaka, uzembe wa madereva na ubovu wa magari vimetajwa kuwa bado ni chanzo cha ajali za barabarani mkoani Mbeya ambapo usiku wa kuamkia leo, Alhamisi Novemba 28, watu kadhaa wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha magari sita, bajaji na pikipiki katika eneo lenye mteremko mkali mkoani humo.

Hii ni ajali ya nne kutokea Mbeya katika kipindi cha miezi miwili ambapo katika ajali hizo idadi ya waliokufa ni zaidi ya watu 30.

Unadhani nini kifanyike kudhibiti ajali hizi licha ya kuwepo kwa sheria na adhabu kali zinazotolewa kila uchao?

My Take
Watu wa Mbeya msipoachana na ushabiki maandazi wa Wanasiasa uchwara Cha Chadema ambazo haziwasaidii wanaowatumia basi mtaendelea kupuuzwa na Chama Kubwa kwenye miundombinu.

Poleni sana mliofariki na mliopatwa na ajali hizo.Wengine mnaingizwa kwenye mkenge ambao hamkuhusika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom