Mbegu za sunflowers (alizeti)

kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
365
wanandugu naomba kuuliza, mbegu za sunflowers (alizeti) zinapatikana wapi na aina/variety gani ni bora na za kampuni gani. na bei ni kiasi gani?

nimeenda Farmers Center na Farmbase pale ilala nimezikosa. hawana taarifa wapi naweza kupata hizo mbegu!!.

nitashukuru sana msaada wenu..
 
Mkuu kama kunamtu unaemfaham Singida zina patikana kwa wingi. anaweza ktuma kwenye Basi sikumoja tu unazipata
 
Kwasasa sifahamu bei itakuwa kiasi gani,ila mbegu nzuri na yenye kutoa mafuta mengi ni Rikoda/recoda,kutokana na ganda lake kuwa jembamba na kiini ni kikubwa.
inapatikana arusha kama kuna mtu unafahamiana naye Arusha anaweza kwenda maduka ya pembejeo akaulizia aina hiyo.
Pia wana ofisi zao pale viwanja vya nane nane Njiro.TASO
 
Unapatikana wapi.,kwa sababu kama ni Arusha hapokuna makampuni mengi ya mbegu za alizeti! kwa maeneo mengine ya Tanzania pia unaweza kupata mbegu ( dominant ni record). Kitu cha msingi katika kuchagua mbegu za alizeti ni capital uliyonayo na aina ya udongo na kilimo unachotaka kufanya (Modern/traditional), Kama ni modern na una capital ya kutosha unaweza kutumia mbegu (Hybrid) ambazo zinahitaji matunzo ya hali ya juu kidogo, Pia unaweza kutumia Quality seeds kama hizo records au Kenya fedha au kuna mbegu ambazo ni Quaity Declared Seeds (QDS) hizi zinapatikana kwa wingi zaidi na bei yake ni nzuri
 
Back
Top Bottom