Mbegu za chia, matumizi yake na umuhimu wake

kahuru kar

Member
Dec 22, 2016
41
23
*Nawasalimu kwa majina matakatifu wana jamvi*
Nimekuwa nikifuatilia kwa muda sasa juu ya mbegu za Chia (CHIA SEEDS).
Kwa utafiti wangu nimegundua kuwa mbegu hizo n chakula bora mbadala na hakika zina faida nyingi sana.
Baadhi ya faida zake ni
1. Kusaidi kurekebidha mfumo wa damu (blood circulatory system), kwa kuondoa mafuta mgando (cholesterol) na hivyo kupunguza kabisa shinikizo la damu (Blood Pressure).
2. Kusaidia kuondoa kiasi cha sukari mwilini, kwa kuyeyusha stoo ya sukari mwilini (glycogen) ili itumike kwa urahisi mwilini. Hii usaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na kisukari (Diabetes) kwenye mwili.
3. Kuongeza hamu ya kula (hasa kwa wagonjwa na wamama wajawazito).
4. Chia ni Protini marithawa kabisa yenye uwiano mahusui kwa ajili ya seli hai za mwili hasa ikisaidia kuzalisha zaidi seli hai nyeupe za damu- hizi husaidia katika ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa, na pia seli hai nyekundu za damu- hizi usaidia sana kubeba hewa katika mwi.
4. Chia usaidia sana kuongeza OMEGA 3 mwilini.
5. Kwa wale wanene ambao wangependa kupunguza mwili wao kirahisi bila kutumia madawa mbadala, basi Chia seeds (mbegu za chia) zinawafaa sana.
Zipo faida nyingi sana, kutaja chache.

MATUMIZI YA CHIA
1. Chia (Kijiko kimoja au viwili ) huwekwa kwenye kikombe cha chai yoyote na ikikorogwa tu, inakuwa tayari kwa matumizi.
2. Chia inaweza kuwekwa kwenye glass ya maji ya baridi na kunywewa kama kawaida.
3. Unaweza kuongeza Chia seeds kwenye matunda na ukala kama kawaida tu bila usumbufu.
Matumizi mwngineyo ni kama upendavyo kula chakula chako chochote.

Pia chia haihitaji kupikwa wala kufanyiwa maandalizi mengine ya ziada ili kutumika.

CHIA SEEDS zinapatikana mara nyingi kwenye supermarkets au kwa maduka ya vyakula.
 
Napenda kuzitumia sana kwenye maziwa mtindi wakati wa jioni/usiku kabla sijalala au kwenye mbogamboga(salad)kidogo,.ni nzuri kwakweli...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom