Orketeemi
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 4,905
- 12,103
MBEGU TULIYOIPANDA IMESTAWI VIZURI.
Kuanzia Jana jioni mpaka leo kuna habari ya kusikitisha kuhusu ajali iliyotokea Mwika- Rombo ambapo waliotoka katika sherehe za kuazimisha miaka 40 ya CCM walipata ajari na baadhi kufariki dunia. R.I.P
Baada ya kusambaa habari hiyo watu wengi walitoa maoni yao na kupitia maoni hayo nikashawishika kuamini kwamba " Mbegu tuliyoipanda imestawi vizuri"
Nimesoma comments za watu wengi na Kwa kweli zinasikitisha kuliko hata tukio lenyewe. Mathalani mtu anaandika " Afadhari maCCM yamekufa" Afadhari MaCCM yapungue Inasikitisha sana tena sana kwa watanzania wenzangu kufikia hatua hii.
Miaka mingi iliyopita usingeweza kuona maoni tofauti na kuwaombea marehem wapumzike Kwa amani, kuwaombea majeruhi wapone haraka lakini Kwa sasa hali ni tofauti watu wanaandika " Afadhari [HASHTAG]#MACCM[/HASHTAG] yamekufa"
Mtu mwenye maoni ya aina hiyo huwezi kumwita nyumbu, huwezi kumlaani wala huwezi kumlaumu zaidi zaidi utakumbuka Tanzania imetoka wapi na inaelekea wapi? Tanzania ile iliyokuwa inashikamana katika shida na raha imeenda wapi?
Tanzania ile iliyokuwa pamoja katika shida na raha imeondoshwa na watawala Kwa maslahi ya chama tawala , Tanzania ile imeondoshwa na tabia ya polisi wetu kuthamini zaidi utu wa watu wenye itikadi sawa za kisiasa na watawala
Kwamba mtu asiye mfuasi wa chama tawala anaonekana kuwa mtu daraja la pili ndani ya nchi yake (So sad). Imefikia hatua kama wewe sio wa CCM basi kupata haki ni kudra tu za mwenyezi Mungu, hali hii si nzuri.
Hebu fikiria ndugu yako ambaye hakuwa mfuasi wa CCM anauwawa tena na watu amabao wanafahamika kabisa lakini polisi wanatoa majibu mepesi kabisa kwamba waliomuua ni " Watu wasiojulikana" na wanaishia hapo.
Fikiria ndugu na jamaa wa marehem Alphonse Mawazo watakuwa na mioyo ya aina gani huko waliko wakikumbuka yaliyomkuta ndugu yao na watu gani walishangilia,, watawapenda hao?
Kumbuka anayofanyiwa mbunge wa Arusha mjini je familia yake inajengewa nini kisaikolojia inapoona baadhi ya watu wanashangilia kisa tu mh. Mbunge si mwana CCM.?
Chuki ya aina gani tunaijenga Kwa familia ya Lowassa Kwa kumtukana mtu wanayemheshim sana matusi ya nguoni , matusi ya yenye lengo la kuudharirisha utu wake bila kujali kwamba wapo watu huyu tunayemtukana ni baba yao, mkwe wao, mjomba n.k?
Kwa nini wanaCCM wanazikumbuka sana kauli kwamba kifo ni chetu sote pindi tu yanapowakuta wao?
Nitoe wito Kwa sisi sote kutafakari kwa kina kwamba nchi hii tunaipeleka wapi, UCCM na Uso CCM ni muhim kuliko Utanzania wetu?
Kila mmoja katika nafasi yake anajukum la kuikataa hali hii pasipo kunyoosheana vidole ili tuweze kuirudisha Tanzania ile ya enzi za vita vya Kagera.
MBEGU TULIYOIPANDA IMESTAWI TUSIIACHE IKAKOMAA.