Mbatia: Wabunge wengi hawajui kilichowapeleka Dodoma

Mbatia: Wabunge wengi hawajui kilichowapeleka Dodoma

Gefu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
6,929
Reaction score
2,567
Mara kadhaa mijadala mbalimbali bungeni imekuwa ikitawaliwa na itikadi za vyama vya siasa badala ya hali halisi ama kuangalia jambo husika kama lina maslahi ya taifa au la.

Wabunge wengi wa CCM wako tayari kuikandamiza hoja nzuri na yenye maslahi ya taifa ilimradi tu imewasilishwa bungeni na mbunge wa chama cha upinzani.

Mwandishi Wetu amezungumza na Mbatia ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na rais kuhusu mijadala kutawailiwa na ushabiki wa vyama badala ya kuangalia umuhimu wa hoja iliyowasilishwa mezani na imewasilishwa na mbunge wa chama gani.

Mbatia anaanza kwa kusema kuwa wabunge wengi hasa wa CCM pengine hawajui wajibu wao bungeni ama kwa makusudi wanaacha kutimiza wajibu wao na kubaki kuwa washabiki wa serikali.

Anasema wabunge hao wao wamekuwa wakikaa muda wote kuangalia namna ya kulinda serikali pindi inapobanwa na wabunge bungeni na kuacha jukumu la msingi la kuisimamia kutekeleza majukumu yake.

"Wajibu wa mbunge ni kuisimamia serikali lakini wengine kwa makusudi wameacha wajibu wao na kujivika jukumu la kuilinda na kuitetea serikali, wananchi waliwachagua wakaisimamie serikali ili iwaletee maendeleo lakini wamewageuka wananchi wanaitetea serikali kana kwamba ndiyo iliyowapeleka mle," anasema Mbatia.

"Wajibu wa kwanza wa mbunge ni taifa lake, jimbo lake na dhamira yake binafsi, lazima jambo linalohusu maslahi ya taifa linapowasilishwa lijadiliwe bila kuangalia itikadi za vyama vya siasa, hoja yangu ilikuwa na maslahi kwa taifa lakini kwa kuwa iliwasilishwa na mpinzani ikapuuzwa,"

"Baadhi ya wabunge wakaleta UCCM wao kwenye hoja ambayo kimsingi inamaslahi kwa taifa zima, kama elimu bora niliyokuwa nazungumzia si kwa watoto wangu tu ni taifa zima la Tanzania, kwenye hoja yangu hakuna sehemu niliyoandika chama changu cha NCCR lakini inashangaza watu wakaweka mbele vyama vyao," anabainisha.

Mbatia anasema kwa bahati nzuri wale wote waliokuwa wakimpinga katika mkutano wa Bunge uliopita wameumbuliwa na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne maana ni janga la taifa.

Mbatia anasema katika hali ya kushangaza hata Spika na Naibu Spika badala ya kufanya majukumu yao wamegeuka watu wa kuikingia kifua serikali.

Anasema wawili hao nao walisimama kidete kudhoofisha hoja yake kana kwamba haikuwa na msingi wowote wala maslahi kwa taifa.

"Spika anaikingia kifua serikali lakini hiyo siyo kazi yake, kazi yake ni kusimamia vikao vya Bunge na kuhakikisha anasimamia demokrasia bungeni na wala si kupendelea wabunge wa CCM na serikali," anasema Mbatia.

Anasema baada ya kuikalia kooni serikali ilikwenda na kuchakachua mitaala na kuwasilisha bungeni nyaraka feki ili tu kujivua aibu iliyosababishwa na hoja yake.

"Walikwenda wakafanya ujanja ujanja ilimradi nionekane kwa jamii kwamba nimedanganya Bunge lakini walicholeta si mitaala ile, kwa ujasiri kabisa nasema walicholeta bungeni ni uchafu mtupu," anasema

Mbatia anasema baada ya kuwasilishwa kwa mitaala hiyo ya kuchakachua baadhi ya wabunge walijipanga wakidhani wataweza kumwondoa kwa madai ya kulidanganya Bunge lakini waliishia kupata aibu ndani ya ukumbi huo.

"Baada ya kuwasilishwa kwa hayo makaratasi waliyoita mitaala Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwang'alah akatoa hoja kwamba Bunge linifukuze kwa kusema uongo lakini mwishowe aliishia kwa kupata aibu, aliungwa mkono na wabunge wasiozidi watano tu," anasema.
Mbatia anasema ukweli ndani ya moyo wake ni kwamba kama kweli serikali ingethibitisha kwamba inayo mitaala angejiuzulu ubunge na kuendelea na shughuli zingine.

"Nilisema yale bungeni nikiwa na uhakika na ninachokisema maana nimefanya utafiti kwa miaka 18, sasa baadhi ya wabunge waliingia kichwa kichwa wakadhani mimi nimeropoka tu kwa kutaka sifa, wakapinga na kunizodoa lakini mwisho wake haya matokeo ni aibu kwao sijui watajificha wapi," anasema

Aidha, anasema wabunge wengi wa CCM walikuwa wanajua ukweli kuhusu hoja yake na ndiyo sababu hawakuwa na ujasiri wa kumuunga mkono mbunge wa Nzega aliyetaka afukuzwe bungeni.

"Kinachoiumiza nchi hii ni unafiki, watu walinishambulia ndani ya ukumbi wa Bunge kana kwamba ninachosema hakina maslahi kwa taifa lakini hao hao mkikutana kwenye korido za Bunge wanakupa mkono wa pongezi kwamba hoja yako ni ya msingi sana, huo ni unafiki wa hali ya juu sana na kuna baadhi ya mawaziri walinipongeza lakini wakiwa ndani ya ukumbi wanazungumza unafiki tu," anasema

Anasema kutokana na ubovu huo wa mitaala na mfumo mzima wa elimu fedha nyingi zinazotolewa na serikali zinaishia kujenga nyumba za vigogo badala ya kutumika kuendeleza elimu.

"Kuna mabilioni yameliwa ambayo yangeweza kununua vifaa vya elimu na kujenga shule, sasa wabunge wengine hawafanyi utafiti wao ni kupinga kila anachosema mpinzani, lakini anapiga makofi tu bungeni hata kwa mambo ya kijinga yanayosemwa na serikali," anasema.

Mbatia anashangaa ujasiri wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawamba wa kuendelea na kazi wakati asilimia 90 ya watahiniwa wakiwa wamefeli.

"Ili kuokoa jahazi mfumo mzima uondolewe, tuanze na kinara Waziri mwenyewe asipojiuzulu basi Rais amfukuze kazi maana hii ni aibu ya karne, Waziri anawezaje kuendelea nakazi wakati hakuna cha maana anachofanya," anahoji Mbatia
Mbatia anasema Rais Jakaya Kikwete lazima aunde tume ya kuangalia mfumo mzima wa elimu na ije na mapendekezo ya namna ya kuuboresha.

"Elimu ilipoyumba miaka ya 80, Nyerere aliunda tume iliyoongozwa na Jacksoni Makwetta kuchunguza na kutoa mapendekezo sasa wakati huu mambo hayaendi tunaogopa nini

Lakini Mbatia alipinga na kusenma kilichowasilishwa siyo alichokidai bungeni, mtalaa alioudai ulikuwa wa mwaka 1997 hadi mwaka 2005 wakati uliowasilishwa ni wa mwaka 1998 hadi 2008 ambao unasema ni kwa ajili ya Tanzania Bara.

"Huwezi kusema Mtalaa wa Elimu ya Sekondari ni wa Tanzania wakati huu uliopo unaonyesha ni wa Tanzania Bara wakati hata mtihani unaofanyika wa darasa la saba ni wa Tanzania.

"Kasoro nyingine ni kwamba katika vitabu vya mwongozo inatakiwa kuwa na Alama Ubora (ISBN) kwa kuidhinishwa na Bodi ya Maktaba, sasa mtalaa wa jana hauna hayo yote"
Kikao cha Bunge kilichomalizika hivi karibuni kilikumbwa na machafuko makubwa zaidi kutokea katika historia yake. Sakata lile lilisababishwa na Spika Anne Makinda na Naibu Spika, Job Ndugai, kuzuia hoja za wabunge wa upinzani kuendelea kujadiliwa bungeni, bila shaka kuinusuru serikali.

Huko nyuma, wabunge wa upinzani walipoona hoja zao hazipewi nafasi au kujadiliwa kwa uzito huku wakidhihakiwa, walisusa na kutoka nje ya Bunge. Walipofanya hivyo, wenzao wa CCM waliwazomea na kuwasindikiza kwa kugonga meza.

Kikao cha Bunge kilichomalizika hivi karibuni, wapinzani waliona hakuna haja ya kususa kama ilivyokuwa huko nyuma. Badala yake waliamua kusimama na kumzomea Spika ama Naibu wake ili kudai haki ya hoja zao kusikilizwa na kupatiwa majibu stahiki.

Kuona hivyo, Spika Anne Makinda akaikabidhi Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo, Hassan Ngwilizi kuchunguza sababu ya songombingo ile, waliosababisha na hatua za kuchukuli Kamati ilitoa taarifa yake bila kueleza kwa undani kiini cha songombingo ile.

Badala yake iliwataja wabunge wanne wa Chadema -- John Mnyika, (Ubungo), Joshua Nasari (Arumeru Mashariki), Tundu Lisu (Singida Mashariki) na Pauline Gekul wa Viti Maalum – kuwa chanzo kwa kumzomea Naibu Spika. Hata hivyo Kamati haikueleza hatua za kuchukuliwa!

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo waliishutumu Kamati hiyo kuwa haikuwatendea haki wabunge iliowataja kwani haikueleza kiini cha wao kuzomea. Hili pia lilisemwa na baadhi ya wabunge wa CCM wasiokuwa ndumakuwili kuwa wabunge wa Chadema hawakutendewa haki kwa kutosikilizwa.

Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, alisema wazi wazi kwamba wabunge hao hawakutendewa haki kwani hawakuitwa kuhojiwa.

Chanzo; Nipashe
 
Mbatia umepatia. Wassira, Pinda, Festus Limbu wa Magu, Mansoor wa Kwimba, Makinda, Ndugai na wengine kibao hawajui kabisaaaaaa!
 
Serikali ya CCM haijui inachokifanya hapa DUNIANI(Hawajui ni kwanini wapo hapa Duniani)
 
Hoja ya Mbatia bungeni ilikuwa nzuri sana, nashangaa CCM kuamua kuitupa chini. Mbatia anafanya kazi aliyotumwa na waliompeleka bungeni kwa umakini wa hali ya juu, na ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja. Haikuwa ajali JK kumteua Mbatia. Yote ni mikakati ya kujaribu kupunguza nguvu ya CDM.
 
Mara kadhaa mijadala mbalimbali bungeni imekuwa ikitawaliwa na itikadi za vyama vya siasa badala ya hali halisi ama kuangalia jambo husika kama lina maslahi ya taifa au la.

Wabunge wengi wa CCM wako tayari kuikandamiza hoja nzuri na yenye maslahi ya taifa ilimradi tu imewasilishwa bungeni na mbunge wa chama cha upinzani.

Mwandishi Wetu amezungumza na Mbatia ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na rais kuhusu mijadala kutawailiwa na ushabiki wa vyama badala ya kuangalia umuhimu wa hoja iliyowasilishwa mezani na imewasilishwa na mbunge wa chama gani.

Mbatia anaanza kwa kusema kuwa wabunge wengi hasa wa CCM pengine hawajui wajibu wao bungeni ama kwa makusudi wanaacha kutimiza wajibu wao na kubaki kuwa washabiki wa serikali.

Anasema wabunge hao wao wamekuwa wakikaa muda wote kuangalia namna ya kulinda serikali pindi inapobanwa na wabunge bungeni na kuacha jukumu la msingi la kuisimamia kutekeleza majukumu yake.

“Wajibu wa mbunge ni kuisimamia serikali lakini wengine kwa makusudi wameacha wajibu wao na kujivika jukumu la kuilinda na kuitetea serikali, wananchi waliwachagua wakaisimamie serikali ili iwaletee maendeleo lakini wamewageuka wananchi wanaitetea serikali kana kwamba ndiyo iliyowapeleka mle,” anasema Mbatia.

“Wajibu wa kwanza wa mbunge ni taifa lake, jimbo lake na dhamira yake binafsi, lazima jambo linalohusu maslahi ya taifa linapowasilishwa lijadiliwe bila kuangalia itikadi za vyama vya siasa, hoja yangu ilikuwa na maslahi kwa taifa lakini kwa kuwa iliwasilishwa na mpinzani ikapuuzwa,”

“Baadhi ya wabunge wakaleta UCCM wao kwenye hoja ambayo kimsingi inamaslahi kwa taifa zima, kama elimu bora niliyokuwa nazungumzia si kwa watoto wangu tu ni taifa zima la Tanzania, kwenye hoja yangu hakuna sehemu niliyoandika chama changu cha NCCR lakini inashangaza watu wakaweka mbele vyama vyao,” anabainisha.

Mbatia anasema kwa bahati nzuri wale wote waliokuwa wakimpinga katika mkutano wa Bunge uliopita wameumbuliwa na matokeo ya mtihani wa kidato cha nne maana ni janga la taifa.

Mbatia anasema katika hali ya kushangaza hata Spika na Naibu Spika badala ya kufanya majukumu yao wamegeuka watu wa kuikingia kifua serikali.

Anasema wawili hao nao walisimama kidete kudhoofisha hoja yake kana kwamba haikuwa na msingi wowote wala maslahi kwa taifa.

“Spika anaikingia kifua serikali lakini hiyo siyo kazi yake, kazi yake ni kusimamia vikao vya Bunge na kuhakikisha anasimamia demokrasia bungeni na wala si kupendelea wabunge wa CCM na serikali,” anasema Mbatia.

Anasema baada ya kuikalia kooni serikali ilikwenda na kuchakachua mitaala na kuwasilisha bungeni nyaraka feki ili tu kujivua aibu iliyosababishwa na hoja yake.

“Walikwenda wakafanya ujanja ujanja ilimradi nionekane kwa jamii kwamba nimedanganya Bunge lakini walicholeta si mitaala ile, kwa ujasiri kabisa nasema walicholeta bungeni ni uchafu mtupu,” anasema

Mbatia anasema baada ya kuwasilishwa kwa mitaala hiyo ya kuchakachua baadhi ya wabunge walijipanga wakidhani wataweza kumwondoa kwa madai ya kulidanganya Bunge lakini waliishia kupata aibu ndani ya ukumbi huo.

“Baada ya kuwasilishwa kwa hayo makaratasi waliyoita mitaala Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwang’alah akatoa hoja kwamba Bunge linifukuze kwa kusema uongo lakini mwishowe aliishia kwa kupata aibu, aliungwa mkono na wabunge wasiozidi watano tu,” anasema.
Mbatia anasema ukweli ndani ya moyo wake ni kwamba kama kweli serikali ingethibitisha kwamba inayo mitaala angejiuzulu ubunge na kuendelea na shughuli zingine.

“Nilisema yale bungeni nikiwa na uhakika na ninachokisema maana nimefanya utafiti kwa miaka 18, sasa baadhi ya wabunge waliingia kichwa kichwa wakadhani mimi nimeropoka tu kwa kutaka sifa, wakapinga na kunizodoa lakini mwisho wake haya matokeo ni aibu kwao sijui watajificha wapi,” anasema

Aidha, anasema wabunge wengi wa CCM walikuwa wanajua ukweli kuhusu hoja yake na ndiyo sababu hawakuwa na ujasiri wa kumuunga mkono mbunge wa Nzega aliyetaka afukuzwe bungeni.

“Kinachoiumiza nchi hii ni unafiki, watu walinishambulia ndani ya ukumbi wa Bunge kana kwamba ninachosema hakina maslahi kwa taifa lakini hao hao mkikutana kwenye korido za Bunge wanakupa mkono wa pongezi kwamba hoja yako ni ya msingi sana, huo ni unafiki wa hali ya juu sana na kuna baadhi ya mawaziri walinipongeza lakini wakiwa ndani ya ukumbi wanazungumza unafiki tu,” anasema

Anasema kutokana na ubovu huo wa mitaala na mfumo mzima wa elimu fedha nyingi zinazotolewa na serikali zinaishia kujenga nyumba za vigogo badala ya kutumika kuendeleza elimu.

“Kuna mabilioni yameliwa ambayo yangeweza kununua vifaa vya elimu na kujenga shule, sasa wabunge wengine hawafanyi utafiti wao ni kupinga kila anachosema mpinzani, lakini anapiga makofi tu bungeni hata kwa mambo ya kijinga yanayosemwa na serikali,” anasema.

Mbatia anashangaa ujasiri wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawamba wa kuendelea na kazi wakati asilimia 90 ya watahiniwa wakiwa wamefeli.

“Ili kuokoa jahazi mfumo mzima uondolewe, tuanze na kinara Waziri mwenyewe asipojiuzulu basi Rais amfukuze kazi maana hii ni aibu ya karne, Waziri anawezaje kuendelea nakazi wakati hakuna cha maana anachofanya,” anahoji Mbatia
Mbatia anasema Rais Jakaya Kikwete lazima aunde tume ya kuangalia mfumo mzima wa elimu na ije na mapendekezo ya namna ya kuuboresha.

“Elimu ilipoyumba miaka ya 80, Nyerere aliunda tume iliyoongozwa na Jacksoni Makwetta kuchunguza na kutoa mapendekezo sasa wakati huu mambo hayaendi tunaogopa nini

Lakini Mbatia alipinga na kusenma kilichowasilishwa siyo alichokidai bungeni, mtalaa alioudai ulikuwa wa mwaka 1997 hadi mwaka 2005 wakati uliowasilishwa ni wa mwaka 1998 hadi 2008 ambao unasema ni kwa ajili ya Tanzania Bara.

“Huwezi kusema Mtalaa wa Elimu ya Sekondari ni wa Tanzania wakati huu uliopo unaonyesha ni wa Tanzania Bara wakati hata mtihani unaofanyika wa darasa la saba ni wa Tanzania.

“Kasoro nyingine ni kwamba katika vitabu vya mwongozo inatakiwa kuwa na Alama Ubora (ISBN) kwa kuidhinishwa na Bodi ya Maktaba, sasa mtalaa wa jana hauna hayo yote”
Kikao cha Bunge kilichomalizika hivi karibuni kilikumbwa na machafuko makubwa zaidi kutokea katika historia yake. Sakata lile lilisababishwa na Spika Anne Makinda na Naibu Spika, Job Ndugai, kuzuia hoja za wabunge wa upinzani kuendelea kujadiliwa bungeni, bila shaka kuinusuru serikali.

Huko nyuma, wabunge wa upinzani walipoona hoja zao hazipewi nafasi au kujadiliwa kwa uzito huku wakidhihakiwa, walisusa na kutoka nje ya Bunge. Walipofanya hivyo, wenzao wa CCM waliwazomea na kuwasindikiza kwa kugonga meza.

Kikao cha Bunge kilichomalizika hivi karibuni, wapinzani waliona hakuna haja ya kususa kama ilivyokuwa huko nyuma. Badala yake waliamua kusimama na kumzomea Spika ama Naibu wake ili kudai haki ya hoja zao kusikilizwa na kupatiwa majibu stahiki.

Kuona hivyo, Spika Anne Makinda akaikabidhi Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo, Hassan Ngwilizi kuchunguza sababu ya songombingo ile, waliosababisha na hatua za kuchukuli Kamati ilitoa taarifa yake bila kueleza kwa undani kiini cha songombingo ile.

Badala yake iliwataja wabunge wanne wa Chadema -- John Mnyika, (Ubungo), Joshua Nasari (Arumeru Mashariki), Tundu Lisu (Singida Mashariki) na Pauline Gekul wa Viti Maalum – kuwa chanzo kwa kumzomea Naibu Spika. Hata hivyo Kamati haikueleza hatua za kuchukuliwa!

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo waliishutumu Kamati hiyo kuwa haikuwatendea haki wabunge iliowataja kwani haikueleza kiini cha wao kuzomea. Hili pia lilisemwa na baadhi ya wabunge wa CCM wasiokuwa ndumakuwili kuwa wabunge wa Chadema hawakutendewa haki kwa kutosikilizwa.

Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, alisema wazi wazi kwamba wabunge hao hawakutendewa haki kwani hawakuitwa kuhojiwa.

Chanzo; Nipashe
Mbatia acha kutafuta sifa
 
Yani CCM utafikiri inaongozwa na mbumbumbu! Hoja za Dr. HK na Mwigulu ni hoja dhaifu, lakini wakazishabikia wee, wakaacha hoja za maana za Mbatia na Mnyika, hapa ndipo nafika nawaona wabunge wa CCM kama janga la Taifa hili.
 
mbatia ni jembe, ipo siku moja tu maji yatatenganishwa na mafuta!
 
Mara zote huwa nawaza pasipo majibu, hawa wabunge wa CCM, sio wote ila majority kuwa huwa wanamwakilisha nani? Au wamelogwa na nani? maana hajui wajibu wao kabisa na imekuwa ni style ya wabunge wote wa CCM. Angalia mfano Mbuge wa CCM anayejaribu kuisimamia serikali na kusimamia maslahi ya wananchi huyo huitwa mtovu wa nidhamu na huyo lazima ajadiliwe kwenye vikao vya chama kwa kusimama upande wa wananchi tu.

Ulizeni akina Deo Filikunjombe, Kangi Lugola, Samwel Sitta(2005-2010), utajua CCM haipo kwa ajari ya maslahi ya wananchi wa Tanzania na ndio maana wanawaza hata kutonesha LIVE vipindi vya bunge ili wakatimize uupuzi/uovu wao dhidi ya wananchi.
Mbatia amesema kweli tupu, na hakika huwezi kupingana na ukweli daima ona sasa siku chache baada ya kutupwa kwa hoja yake matokeo ya form 4 yanavyofumua uvundo mwingine.
Wabunge wa CCM amukeni, mnakufa na kuiua serikali yenu maana hapo ilipo imelemaa balaa, mtaiziki ingali hai
 
Wabunge wa CCM, ukiacha ufisadi wao na kushibisha matumbo yao, ni wasaliti na wauaji wa maendeleo na maisha ya wananchi wa Tanzania. Hoja za wapinzani ambazo zina maslahi na tija kwa taifa, wanazikataa na kuzomea. Matokeo ya kidato cha nne yamethibitisha alichosema Mh. Mbatia.

Akili za wabunge wengi wa CCM ni kutetea uovu, uzembe, wizi, ufisadi ...nk unaofanywa na serikali yao. Nakumbuka maneno ya Dr. Slaa aliposema CCM ni janga la Taifa. Wengine walipuuza tahadhari hii. Sasa tunavuna tulichopanda. Nape na wenzake wamejificha na hawasemi lo lote kuhusu matokeo haya ya kidato cha nne, badala yake wanazungumzia elimu ya viongozi wa CHADMA. Tusishagae sana sana kwa sababu ni small minds.
 
Pamoja na udhaifu wa Mbatia kama anao lakini haki yake tumpe.Alichosema ni dhahiri kinachotokea Bungeni leo.Bunge letu limekuwa kama kilabu cha gongo au pombe za kienyeji maana nafuu hata ya baa kunakanidhamu kidogo.

Wabunge wetu hasa wa chama chetu kisikivu kama kweli kina masikio sijui, sijui pia kama tuliwachagua kwa makosa,au walihonga kwa kupindukia na sasa wanatukomoa,maana mishahara wanayopata ni kama hongo kwa wabunge kwani hawawatetei wala kuwatendea haki waliowatuma wanogopa kunyang'anywa ugali mdomoni.

Na mwisho kabisa Watanzania sijui tupo wasahaulifu au tupo wajinga au tupo wazembe au hatuna elimu ya kutosha hata sielewi,miaka hamsini mbunge anaendelea tu kuchaguliwa ukiuuliza amakufanyia nini eti ni wa chama tawala,Je watanzania wenzangu kwa hili tutafika?Tukiambiwa kupiga kura tunaingia mitini,kwa nini usitumie haki yako ya msingi?Na wengi wa walalamikaji hata kupiga kura hakupiga,inaudhi na kusikitisha sana.Jamani tuamke!

Kama Spika wabunge nadhani ana miaka arobaini yupo bungeni hivi hakuna wenye uwezo ni wao tu?Tujifunze kutokana na makosa,kufanya kosa si kosa tatizo ni kulirudia lile kosa.
 
Tunawataalam weng sana wa mitaala, km pr. osaki. mbatia uko sahihi, nakuunga mkono, ebu tuachane na mtaala, fuatilia kwa ufupi sera ya elimu(ETP=edn training policy) utabaini mapungfu meng sana.Tatizo lingne ni wara ye2 ya elim. . .
 
Wanafuata posho & kugonga meza ili miswada ipite bila kijadiliwa.
Sasa kama wanalala halafu mtu anakurupuka usingizini anasema naunga mkono hoja.
Hata kama hajui kinachojadiliwa wakati huo.
 
Kaka wapo wengi sana, hao uliwtataja ni baadhi tu.............yaani kwa magamba....wabunge wanaojua wajibu wao ni wawili tu: Filikunjombe na Lugola, waliobaki ni ma-mbulula
 
Mh Mbatia wabunge wa CCM wanajua sana kilichowapeleka bungeni tatizo lao ni wachumia tumbo wanaotumikia mfumo mfu wa chama chao na kwa hiyo kujikuta wanalazimika kuutetea mfumo huo kwa njia yoyote ile iwayo and as long as it takes; kwani vinginevyo watazamishwa au watazama na mfumo wao wote;

Do they want to commit suicide? definitely capital NO;

Deo Filikunjombe na Nimrod Mkono walitia saini memorundum ya Zitto Kabwe ya kumn'goa Pinda......... fast forward!! wakatupiliwa mbali kugombea ujumbe wa NEC!!
 
Yani CCM utafikiri inaongozwa na mbumbumbu! Hoja za Dr. HK na Mwigulu ni hoja dhaifu, lakini wakazishabikia wee, wakaacha hoja za maana za Mbatia na Mnyika, hapa ndipo nafika nawaona wabunge wa CCM kama janga la Taifa hili.

Nadhani wanashinikizwa na uongozi wao,hasa mnadhimu wao lukuvi,maana hawaeleweki wanachochangia wala kuhoji..
 
Back
Top Bottom