Mbatia kuongoza POAC!

Mbatia kuongoza POAC!

Status
Not open for further replies.
In fact wabunge wote wanaoteliwa na rais huwa hawawakilishi wananchi bali wanawakilisha serikali hiyo hiyo inayotakiwa kusimamiwa na bunge; wanaweza kuteliwa ili wawe mawaziri au wawe ni watetezi wa serikali wakati inapokamatwa koo na wabunge wengine. Kwa hiyo mbunge wa kuteuliwa kupewa madaraka ya kusimamia kamati za bunge ambazo kazi yake ni kuisimamia serikali, ni makosa makubwa sana kama ya 1+1=1
 
Mimi nilijiunga CHADEMA nikijua ni wapinga rushwa,nadhani wengi tulijiunga kwa sababu hiyo,kwamba cdm ilionekana ni mbadala kwa siasa za tz,ninaumia sana nikisikia CHADEMA wakihusishwa na rushwa,

Kwa akili zangu ili CHADEMA iendelee kuwa maarufu hapa tz, isipoteze mvuto wake kwa wananchi, ni busara kumfukuza zitto uanachama kama kweli itathibitika kuwa anahusika pamoja na wenzake akina sendeka,unapingaje mafisadi wakati wewe ni fisadi pia?

CHADEMA wasiogope hakuna aliye maarufu kuzidi chama chenyewe

Mkuu hapo kwenye RED ndipo tutapima tofauti kati ya CCM na Chadema!

Mara zote uw naamini wanasiasa ni kama vipande vya nguo vilivyokatwa katika jozi moja!

Ikumbukwe hata CCM wanasema watuhumiwa wao hawana ushaidi kuwa walipokea rushwa, hivyo haijathibitika kwa watu kama Chenge kuwa walichukua rushwa! Lol

 
Ninazo habari za karibu kuwa mbatia anatumiwa na mafisadi walioko kwenye kambi za urais za CCM, wanampigia chapuo ili achukue nafasi ya Zitto huko POAC, ifikapo 2015 ameahidiwa kuwa atasaidiwa pesa za kampeni ili chama chake cha NCCR kipate wabunge angalua wengi kuliko CHADEMA na kuwa upinzani rasmi bungeni. FUATILIENI KWA KARIBU NA SIKU MOJA MTAKUMBUKA THREAD HII

Hapo kwenye red ni ndoto za mchana
 

Je unafahamu utaratibu wa kuwapata wenyeviti wa hizo committee? Tafadhali nijibu haya maswali yangu mawili kwanza kabla sijakuswalisha swali la nyongeza.


Nothing is impossible under the sun except bringing the dead back to life....tena kwa Africa ndo rahisi kabisa.
Rules of the game tunazipanga wenyewe na mwenye nguvu anaweza kuzipinda ili anachokitaka kitimie....isitoshe rules zinaweza zikafuatwa na bado matokeo yakapangwa na yakatimia.
 
Pandikizi + Pandikizi Jipya = Chama cha Mafisadi
 
Kweli kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu. Mbatia alishirikiana na Zitto na Zoka 2010 kuiwezesha NCCR kupata wabunge 4 Kigoma, leo tena wamegeuka panya na paka. Safi sana.

mnh! kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo,na ni zaidi ya vile unawezaifikiria hata kama uko ndotoni!
 
​semeni yoote lakini 2015 chadema inachukua nchi poleni kwa maumivu makali ukweli unauma bana
 
kesho mda kama huu mtakuwa mmebadilika na kumpigia makofi Zitto
Amezidi kunichefua aliposema yeye ndiye tumaini la wanyonge na vijana wote bila kujali itakidi zao kisiasa. Naichukulia hiyo kama ishara ya mtu mwenye ujivuni na kibri (arrogance), na hiyo haijawahi kuwa sifa ya kiongozi bora.
 
Ni mtazamo na tafsiri yako. Ni vema tukaiheshimu. Siamini kuwa ni lazima POAC iongozwe na Mh. Kabwe. Bila shaka yeye mwenyewe anajua kuwa baada ya haya yaliyotokea ni vema apokelewe na mtu mwingine. Awe Mbatia au yeyote yule. Muhmu ni wajumbe wa kamati kuwa makini na smart katika kutekeleza na kusimamia majukumu yao.
 
2. alishiriki kikamilifu kuisambaratisha NCCR mageuzi wakati wa Mrema

Kama Mbatia alishiriki kikamilifu, lakini ukweli bado unabaki pale pale kwamba Marando na Lamwai ndio walikuwa key players wa kuisambaratisha NCCR! Baada ya kufanikisha hilo, Lamwai akazawadiwa ubunge kupitia CCM na Marando akazawadiwa ubunge EA!!
 
Thread hii kama zilivyo threads nyingine zote zenye maneno machafumachafu dhidi ya Mbatia na NCCR-Mageuzi, ni sehemu ya mkakati ya kipumbavu ya wa wanaCHADEMA ya kuhakikisha wanakichafua chama kingine chochote nchini kinachoonekana kuwa na uwezekano wa kupata nguvu miongoni mwa vyama vya upinzani.

Mtaendelea kuandika sana upuuzi wenu huu, lakini kila siku mnaowakashfu wataendelea kubarikiwa, badala yake laana itawajia iliyo sawa na ukubwa wa kashfa mnazowarushia wengine.
Poleni sana.
 
Hizi tuhuma zilianzishwa kwa mkakati maalumu. Mkakati ulikwama mara Tundu Lissu alipotaja majina! Wanaodhani alikua anatafutwa Zitto tu, wanajidanganya, ilikua ni mkakati wa kuwachafua wabunge wa CDM.

Kumbuka akina Mnyika walikua ktk kamati iliyovunjwa kwa tuhuma za rushwa.

Kama kawaida ya CCM wangetumia wahariri wa baadhi ya magazeti kuwachafua wabunge wa CDM,hasa Mnyika kwamba wamekula rushwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom