Mbatia kuongoza POAC!

Mbatia kuongoza POAC!

Status
Not open for further replies.

Mwikimbi

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2008
Posts
1,762
Reaction score
835
sasa niwazi kuwa lile sakata linaloendelea ndani ya wizara ya madini na nishati linachukua sura mpya, wale mnaowaona wakipiga kelele ni kuwa si bure, vita yote hiyo nia ni kumngoa Zitto Kabwe na muda simrefu James Mbatia atateuliwa kuwa mwenyekiti wa POAC,
James Mbatia ni mwanasiasa mwenye utata mwingi kuhusu kile aanachosimamia, mfano:

1. ndiye aliyeongoza kampeni miaka ya nyuma ile ilyohakikisha CUF kule Zanzibar imekosa wabunge 6 wakati ule akitumiwa na CCM, na bado anajulikana kama mpinzani

2. alishiriki kikamilifu kuisambaratisha NCCR mageuzi wakati wa Mrema

3. alimfungulia kesi Halima Mdee kule Kawe huku akijua kuwa yeye alikuwa mshindi wa tatu, na kwa vyo vyote vile CCM wangekuwa beneficiary kama Mdee angeshindwa ile kesi.

4. alishiriki kumwengua David Kafulila uanachama na hivyo kuuweka ubunge huo mashakani

Ninazo habari za karibu kuwa mbatia anatumiwa na mafisadi walioko kwenye kambi za urais za CCM, wanampigia chapuo ili achukue nafasi ya Zitto huko POAC, ifikapo 2015 ameahidiwa kuwa atasaidiwa pesa za kampeni ili chama chake cha NCCR kipate wabunge angalua wengi kuliko CHADEMA na kuwa upinzani rasmi bungeni. FUATILIENI KWA KARIBU NA SIKU MOJA MTAKUMBUKA THREAD HII
 
chuki asubuhi, chuki jioni, chuki usiku
 
....
4. alishiriki kumwengua david kafulila uanachama na hivyo kuuweka ubunge huo mashakani

ninazo habari za karibu kuwa mbatia anatumiwa na mafisadi walioko kwenye kambi za urais za ccm, wanampigia chapuo ili achukue nafasi ya zitto huko POAC , ifikapo 2015 ameahidiwa kuwa atasaidiwa pesa za kampeni ili chama chake cha Nccr kipate wabunge angalua wengi kuliko cdm na kuwa upinzani rasmi bungeni. FUATILIENI KWA KARIBU NA SIKU MOJA MTAKUMBUKA THREAD HII
Mkuu hapo kwenye wekundu hakuna kiasi cha fedha kinachoweza kufanikisha hilo lengo.
 
Kama kawaida yenu CHADEMA, mtaendelea kumwandama Mwenyekiti wetu hata lini? Kama watu wenu wamekula rushwa, hangaikeni na hilo na mjue namna ya kulishughulikia, sio kusingizia eti ni njama zinazohusiana na POAC au 2015.

Nawashaurini badala ya kujitahidi kuchafua watu wasiokuwa wa vyama vyenu kwa hofu ya kwamba wanaweza kuwaondoa katika nafasi zenu, wahakikishieni watanzania kwamba mnao uwezo wa kuwashughulikia wala rushwa wanaobainika miongoni mwenu.

Hamjamsoma Dr. Lwaitama leo? "Mmeshindwa kujipambanua kisera badala yake mmechagua uzushi na mashindano ya matusi"
 
kesho mda kama huu mtakuwa mmebadilika na kumpigia makofi Zitto
 
Last edited by a moderator:
Kweli kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu. Mbatia alishirikiana na Zitto na Zoka 2010 kuiwezesha NCCR kupata wabunge 4 Kigoma, leo tena wamegeuka panya na paka. Safi sana.
 
Kweli kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu. Mbatia alishirikiana na Zitto na Zoka 2010 kuiwezesha NCCR kupata wabunge 4 Kigoma, leo tena wamegeuka panya na paka. Safi sana.

Acha kusikiliza uzushi wa Mwikimbi
 
mbatia, engineer aliyetaalamika katika masuala ya majanga, whatever that means!
 
Hatutashangaa kama atakuwa ni pandikizi. Kupandikiza ni mbinu-mkakati inayokubalika sana. Swali ni je na vyama vyetu vya upinzani vina mapandikizi ktk chama tawala?????. Hii ni muhimu ktk kuiba siri na taarifa muhimu, Ni vita hii.
 
Mimi nilijiunga CHADEMA nikijua ni wapinga rushwa,nadhani wengi tulijiunga kwa sababu hiyo,kwamba cdm ilionekana ni mbadala kwa siasa za tz,ninaumia sana nikisikia CHADEMA wakihusishwa na rushwa,

Kwa akili zangu ili CHADEMA iendelee kuwa maarufu hapa tz, isipoteze mvuto wake kwa wananchi, ni busara kumfukuza zitto uanachama kama kweli itathibitika kuwa anahusika pamoja na wenzake akina sendeka,unapingaje mafisadi wakati wewe ni fisadi pia?

CHADEMA wasiogope hakuna aliye maarufu kuzidi chama chenyewe
 
He he inaonyesha mwenye habari hii hana uhakika na anayosema kwani mwenyekiti wa kamati huchaguliwa kwa kupigiwa kura, pili kamati ya madini si ya poac then taarifa hii haina ukweli na mashiko, kuna mafisadi papa but wanaongoza kamati hebu tulizeni shanga kwanza uchunguzi umalizike
 
mkuu nieleweni, wakuu wa kamati huchaguliwa na wajumbe wa kamati husika, spika ndo huchagua wajumbe wa kamati, sasa utashangaa utakaposikia wale wajumbe waliochaguliwa na spika kuwa wajumbe wa POAC wamemchgua james mbatia kwa kauli moja kuwa mwenyekiti wao. nchi hii imesukwa na watu wasiozidi 10!!!!!
 
mkuu nieleweni, wakuu wa kamati huchaguliwa na wajumbe wa kamati husika, spika ndo huchagua wajumbe wa kamati, sasa utashangaa utakaposikia wale wajumbe waliochaguliwa na spika kuwa wajumbe wa POAC wamemchgua james mbatia kwa kauli moja kuwa mwenyekiti wao. nchi hii imesukwa na watu wasiozidi 10!!!!!
Mwikimbi Unazifahamu oversight committee?
Je unafahamu utaratibu wa kuwapata wenyeviti wa hizo committee? Tafadhali nijibu haya maswali yangu mawili kwanza kabla sijakuswalisha swali la nyongeza.
 
mkuu nieleweni, wakuu wa kamati huchaguliwa na wajumbe wa kamati husika, spika ndo huchagua wajumbe wa kamati, sasa utashangaa utakaposikia wale wajumbe waliochaguliwa na spika kuwa wajumbe wa POAC wamemchgua james mbatia kwa kauli moja kuwa mwenyekiti wao. nchi hii imesukwa na watu wasiozidi 10!!!!!
Nakwambia kwa mara nyingine, jadili namna chadema itakavyoshughulikia suala la rushwa endapo itabainika, acha kuzuazua mambo hapa. Kamati yenyewe ya POAC hata kuvunjwa haijavunjwa, wewe unatungatunga mambo yako yaliyojaa chuki binafsi na ushabiki wa kisiasa, kisha unayaleta hapa kuwaaminisha watu kwamba hicho ndicho kinachojili.
 
Hata mbatia apewe pesa vp nccr mageuzi 2015 watapoteza hata wabunge ambao wanao saizi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom