Mbatia kulipa mil. 9/- kumpinga Mdee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbatia kulipa mil. 9/- kumpinga Mdee

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 29, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Rehema Mohamed

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewataka walalamikaji katika kesi ya kupinga uchaguzi iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James
  Mbatia na wenzake dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kawe Bi. Halima Mdee kulipa jumla ya sh. milioni 9 kama gharama ya dhamana ya kesi hiyo.

  Uamuzi huo umetolewa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Bw. John Utamwa wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.


  Bw. Utamwa alisema kuwa kila mlalamikaji atatakiwa kulipa sh. milioni 3 kwa kila mshtakiwa badala ya milioni 5/- kama sheria inavyosema. Wanaoshtakiwa katika kesi hiyo, ni Bi. Mdee, Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.


  Awali Bw. Mbatia aliiomba mahakama hiyo impunguzie kutoka sh. milioni 5 na badala yake alipe milioni moja kwa kila mshtakiwa kama dhamana ya kesi hiyo na wenzake kuomba kusamehewa kulipa fedha hizo, ambapo Bw. Utamwa alisema maombi hayo hayakuonesha sababu ya msingi ya kuwa hawana uwezo wa kulipa dhamana iliyopangwa kisheria.


  Alisema kuwa mawakili wa pande zote mbili walionesha nia ya kupunguzwa kwa kiasi hicho cha fedha za dhamana ambapo walipanga walalamikaji walipe kati ya sh. milioni 1 hadi 2.5.


  Alisema kutokana na maombi yaliyowasilishwa kwake aliamua kupanga kiasi cha sh. milioni 3 kwa kila mlalamikaji kama malipo ya dhamana ya kesi hiyo.


  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17, mwaka huu itakapotajwa tena ambapo kiasi hicho cha fedha kinahitajika kulipwa kabla ya tarehe hiyo, ili iendelee kusikilizwa.


  Bw. Mbatia kupitia mawakili wake, Bw. Mohamed Tibanyendera na Bw. Aloyce Komba, Novemba 25, mwaka jana walifungua kesi ya madai namba 111 kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 31, mwaka jana yaliyompa ushindi Bi. Mdee.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mbona Mhe. Mbatia ulisema wapinzani muache malumbano na mjenge nchi kwa faida na mustakabali wa watanzania; Je hiyo (kesi) haimo ktk orodha ya kuacha malumbano na utata wa kufanyiana visa wenyewe kwa wenyewe?.
   
 3. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwache mbatia....nadhani anataka kuumbuka zaidi. uchaguzi ukirudiwa asifikiri atashinda, aliachwa mbali sana! Kituo nilichosimamia (UCLAS) mbatia alipata 12% wakati Mhe. Mdee 72%, mbona ccm hawalalamiki? au wamekutuma wewe Mbatia? ...Any way ni haki yako. Pambana, maana ni aibu zaidi kwa Mwanamume (?) tena mwenyekiti wa chama kubwagwa na mdada kijana.
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Haya Mambo yanashangaza kweli kweli maana

  MPENDAZOE aliomba kupunguziwa gharama Mahakama IKAKATAA, HAWA Ngumbi ( UBUNGO CCM) Mahakama IMEKUBALI ombi la kupunguziwa, MBATIA ( Kawe- NCCR_Mageuzi) AMEKUBALIWA

  Je Kuna Kitu kinatengenezwa juu ya Haya Majimbo Matatu ya Dar Es Salaam?
   
 5. J

  Joblube JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nani kakuambia Jemsi Mbatia ni mpinzani
   
 6. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Au ni mwanaume wa ukweli.........:smile-big:
   
 7. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  mpaka anatoa kiasi chote hicho inaonekana ana data za kutosha.kesi kama hizo mahakama inatakiwa izisikilize kwa mfululizo na ndani ya wiki moja majibu yapatikane
   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Matia analalamika kuwa Mdee alisema maneno ya kumuumbua kuwa yeye ni Shoga. Hivi atathibitishiaje mahakama kuwa yeye sio Shoga? Na kwani ukijulikana na kuambiwa kuwa u shoga ni kuumbuka?
   
 9. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  aombe atoe tea-go badala ya m9.
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Amechelewa nafasi ya Nape ilikuwa inamfaa, Duhh:tape:
   
 11. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  wewe tuko unaamini nini kati ya hayo matuhuma? na je ndiyo heading ya kesi? au ni mambo ya uchaguzi? maana kama ni kweli hiyo business mbona itakuwa balaa, hadi viongozi?
   
 12. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanaosemaga jamaa ni shosti yaezakuwa wana hoja.

  hivi inakuwaje mshindi wa pili kanyamaza; mshindi wa tatu (mbatia) analalama?
   
 13. logbes

  logbes Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  namsikitikia Mbatia mwe mwe baba wa watu anataka kuumbuka tena
   
 14. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Hoja fikirishi hizo mkuu! hata mimi nimejiuliza kulikoni?
  Yaani Mpendazoe hakupunguziwa kabisaaaa!!
  Mhakama zetu zishaanza kujitia aibu tena...
   
 15. k

  kiloni JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mtoto wa watu!!!!
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu Mbatia si PUNGA hili au ??
   
Loading...