Mbatia: Ichukieni CCM kwa vitendo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbatia: Ichukieni CCM kwa vitendo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waridi, Mar 9, 2012.

 1. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Chanzo: Tanzania Daima

  Mbatia: Ichukieni CCM kwa vitendo


  na Mwandishi wetu, Tandahimba


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]MWENYEKITI wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amezidi kuwasha moto mkoani Mtwara, baada ya kuwataka wananchi wa mkoa huo kuichukia kwa vitendo CCM.
  Alisema kuwa hata kama CCM bado wana nia ya kuendelea kutawala nchi, katika kipindi hiki wananchi hawana sababu ya kuendelea kukiunga mkono kwa kuwa kimekuwa chanzo cha kudorora kwa uchumi wao.
  Mbatia aliyasema hayo mjini Tandahimba mkoani Mtwara juzi wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika moja ya mikutano yake ya kukijenga chama mkoani hapa.
  “CCM siyo chama cha kucheka nacho, lazima muonyeshe chuki za waziwazi, lazima sasa muwaambie CCM basi kwa sababu kimeshindwa kutimiza wajibu wake.
  Nawaambieni ukiona kitu kinakuudhi kama CCM, kemea, kama ukishindwa kukemea basi chukia, onyesheni kwa dhati kwamba mnaichukia. Unaweza kuwadanganya watu wachache kwa wakati wote lakini kamwe huwezi kuwadanganya watu wote kwa wakati wote,” alisema Mbatia.
  Kwa mujibu wa Mbatia, siku ya mwisho Mungu atawahukumu wanadamu kutokana na matendo yao waliyotenda duniani na kwamba hivyo hivyo atawahukumu Watanzania kwa kuendelea kuiunga mkono CCM wakati haina sifa ya kuendelea kuwa madarakani.
  “Kuanzia sasa CCM ijue kwamba tuko tayari kuishtaki kwa Mungu kutokana na matendo yake na kama hatatusikia, basi tuko tayari kwa mapambano hadi tutakapopata haki zetu,” alisema.
  Katika hatua nyingine, aliitaka serikali itamke wazi kuwa imeshindwa kuwatafutia soko la korosho wakulima wa Mtwara kwa kuwa haiwezekani kila mwaka wakulima hao wanapata hasara wakati zao hilo ndilo wanalolitegemea.
  Naye Katibu Mwenezi wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali, aliwashangaa wakazi wa Tandahimba kuwa maskini wakati hawana sababu ya kuwa katika hali hiyo.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Ameanza kuwageuka bwana zake.
   
 3. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mbatia simwamini hata siku moja. Kauli zake, mawazo yake na matendo yake huwa tofauti kabisaaa
   
 4. L

  LazaroSMtindi Senior Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwongo mkubwa huyo. Likija suala la ufisadi, atasema kila mtu ni fisadi ili kumfurahisha Manywele na RA. Useless politician! LONG LIVE KAFULILA!!
   
 5. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Anza kutathmini matendo yake kufuatia kauli hii
   
 6. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Naona umetumia uhodari wako wote kujadili hoja alizozitoa. Heko!
   
Loading...