Mbatia aibua madudu mitihani darasa la 7!

Mbatia aibua madudu mitihani darasa la 7!

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,613
Reaction score
6,735
MBUNGE wa kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ameibua madudu mapya katika sekta ya elimu, ambao umebaini kwamba kwenye mitihani ya majaribio ya darasa la saba, baadhi ya maswali ya kuchagua, hayakuwa na majibu.

Mitihani hiyo ya majaribio ya programu maalum ya matokeo makubwa sasa, kwa mujibu wa Mbatia ilifanywa na wanafunzi wa darasa la saba hivi karibuni katika masomo ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza katika wilaya 40 nchini.

Katika uozo huo ambao ameutaja kama kuwakatisha tamaa wanafunzi katika somo la Hisabati, Mbatia alisema maswali sita yalibainishwa na wataalamu wa Hesabu kuwa hayana majibu huku swali moja likiwashinda maprofesa waliofanya mtihani huo.

Alisema katika swali moja, namba 33 walimu wa hisabati katika shule kubwa za msingi walishindwa kulifanya na baadaye kubainika kuwa ni swali la mwanafunzi anayechukua fani ya uhandisi katika vyuo vya elimu ya juu.

Mabatia alisema katika mitihani hiyo, kunamakosa mbalimbali ya lugha pamoja na usahihi wa masuala mbalimbali, ikiwemo programu hiyo kuainishwa kama matokeo makubwa sasa huku jina la wizara likiandikwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.

Alisema katika mtihani huo wa hisabati,ambao wanafunzi wa darasa la saba walitakiwa kufanya kwa saa mbili, mtaalamu wa aligebra aliufanya kwa saa 2:10 na profesa saa 2:03 huku yeye akifanya kwa saa 2:19.

“Matokeo haya ni kuwakatisha tamaa na kuwaua wanafunzi kabla ya kufanya mitihani, ni lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuokoa mapigo haya ya moyo wa Taifa ambayo yakizimika, Taifa linakufa,” alisema.

Mbatia alitoa mapendekezo yake ili kuokoa janga hili la elimu ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Tume ya Kudumu ya Elimu, itakayoshughulikia kuhakikisha ubora wa elimu nchini. Tume hiyo kwa mujibu wa Mbatia, inatakiwa kuwa na mamlaka ya kuhakiki utendaji wa taasisi mbalimbali za elimu, ambazo hadi sasa zimeonekana kutotimiza vyema wajibu wake.

“Ninaamini kwamba,tume hiyo itakapoundwa itasaidia kubainisha wazi nini falsafa na malengo hasa ya utoaji wa elimu nchini, kulingana na wakati tulionao, jambo ambalo halitakuwa geni kwani katika uongozi wa awamu ya kwanza, kulitungwa falsafa na miongozo mbalimbali,”alisema

Alisema kwa mamlaka aliyonayo Rais na na kwa mujibu wa katiba na kwa kadri anavyoona inafaa, anaweza kuunda tume na kuipatia majukumu ya utendaji stahiki, ikiwemo kutoa idhini ya matumizi ya mitaala mingine.

Pia alipendekeza tume hiyo ihariri na kupitia vitabu vya kiada kwa shule nchini na kufanya utafiti za kisayansi kuhusu masuala mbalimbali ya elimu kwa lengo la kuinua ubora wa elimu.

Akizungumza na gazeti hili, Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bunyanzu Ntambi alikiri kuwa jinala wizara limekosewa katika mitihani hiyo. Alipoulizwa kuhusu uozo uliopo katika mitihani hiyo ya majaribio, alisema atafuatilia na atatoa taarifa kwa gazeti hili baadaye.

HabariLeo
 
Mbatia na yeye asitafute umaarufu au asipige kelele ktk swala la vitabu tu au mitihani tu. Aende Mufindi huko akaone shule haina madawati wamebumba udongo ndo madawati wanakalia wanafunzi na kuandikia. We unadhani hapo itapatikana elimu kweli?

Alafu Hawa viongozi wa chama cha madawa wanajisifu eti miaka 50 ya uhuru eti wamefanya makubwa. Makubwa wapi au makubwa katik swala la ufisadi na kushindwa kisimamia serikali na mashirika yote vzr ndo maana twaona tumekua lango la madawa na tumekua lango la bidhaa feki yani tumekua hivyo hivyo.
 
...tuko bize kuzidua vipindi vya Big Rezati Nao kwenye tv,hayo ya mitihani sio kipaumbe chetu kwenye raini yetu ya uchapuzi ya chama chetu cha madawa ya kulevya...
 
Mbatia na yeye asitafute umaarufu au asipige kelele ktk swala la vitabu tu au mitihani tu.
mbatia hatafuti sifa bali ndiye mpinzani pekee w serikali aliyesoma vzr Tanzania anajua elimu n nn n wp kwny makosa ,,,
hao wngn wny secondary za kilatino za hk Italy hawajui shida za mtoto w kitanzania wao n kelele n maandamano
 
MBUNGE wa kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ameibua madudu mapya katika sekta ya elimu, ambao umebaini kwamba kwenye mitihani ya majaribio ya darasa la saba, baadhi ya maswali ya kuchagua, hayakuwa na majibu.

Mwambieni Mbatia kuwa ukipenda boga LAZIMA upende na maua yake. Yeye ni kibaraka wa CCM na yuko tayari siku zote kuisaidia CCM halafu halafu anajifanya kuibua na kushangaa uzembe kama huu!!!
 
kwa hiyo elimu ya mbatia inaishia kuchunguza elimu ya msingi tu kla siku ndiyo mifano yake jamaa naye huyu.
 
mbatia hatafuti sifa bali ndiye mpinzani pekee w serikali aliyesoma vzr Tanzania anajua elimu n nn n wp kwny makosa ,,,
hao wngn wny secondary za kilatino za hk Italy hawajui shida za mtoto w kitanzania wao n kelele n maandamano

huu ndo ukweli kuhusu cdma!
 
Hii nchi ya ajabu sana! Mtihani kama huo anatunga tu mtu mmoja wala hakuna wa kucheki na kuidhinisha?
 
Bila elimu ya msingi elimu nyingine itatoka wapi? heko kwa hilo Mbatia
 
mbatia hatafuti sifa
bali ndiye mpinzani pekee w serikali aliyesoma vzr Tanzania anajua elimu
n nn n wp kwny makosa ,,,
hao wngn wny secondary za kilatino za hk Italy hawajui shida za mtoto w
kitanzania wao n kelele n maandamano

yani upeo wako wa kufikiri ndio unafikia hapo??? Kwa akili yako unadhani mbatia ndio the most educated mpinzani???
Vipi kuhusu prof. Lipumba, prof. Safari, prof. Baregu, dr. Slaa, dr. Kitila, zitto, etc etc
Jipange dogo sio unaropoka tu hovyo hovyo..
 
CCM oyeeee.
Halafu kwa ujinga huu mseme maisha bora kwa kila Mtanzania yatawezekana.
Maisha bora bila elimu bora ni unyani
 
Chama cha madawa ni kushindana kufuturisha wasanii tuu na kuwashau maskini waliowapa kura, kipindi wanaenda kuwadanganya na tisht na kanga!!

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Mbatia na yeye asitafute umaarufu au asipige kelele ktk swala la vitabu tu au mitihani tu. Aende Mufindi huko akaone shule haina madawati wamebumba udongo ndo madawati wanakalia wanafunzi na kuandikia. We unadhani hapo itapatikana elimu kweli?




Yale madawati wenyewe wanayaita Adobe. Kwa kweli inasikitisha, inatia uchungu. Halafu unasikia kwenye majukwaa eti shule zitapewa kompyuta, maajabu!
 
Back
Top Bottom