Mbaroni akituhumiwa kumpiga, kumuua mdogo wake kwa mpini

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando, aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea Jumatatu wiki hii saa 12 jioni. Mtuhumiwa anadaiwa kumuua mdogo wake Makumbi Kigula.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni makumbi kutokwenda kwa kaka yake alipomwita ili wafanye mazungumzo ya kifamilia ambayo hayakuwekwa bayana baada ya mtukumiwa kurejea safarini kutoka Mwanza.

Baada ya kutokwenda wakati walikubaliana, alisema Makumbi alikwenda siku iliyofuata nyumbani kwa kaka yake hali iliyomfanya akasirike na kuchukua uamuzi huo.

Kutokana na hali hiyo, alisema Kigula akisaidiana na mmoja wa watumishi wake wa ndani walimkamata kijana huyo na kumfunga kamba mikononi na miguuni kisha
kaka mtu kuanza kumwadhibu kwa kutumia mpini wa jembe ambao alimpiga nao sehemu mbalimbali za mwili, ikiwamo kichwani huku damu
zikimtoka puani ndipo majirani walipoingilia kati.

Baada ya majirani kuingilia kati, walimpeleka katika zahanati ya kijiji iliyoko kijijini hapo, lakini alifariki dunia jana.

Kamanda Kyando alisema polisi walifika kijijini hapo na kumkamata mtuhumiwa ambaye bado anashikiliwa kwa mahojiano kabla ya kufikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine, Polisi wanamshikilia dereva Josephat Salya mkazi wa Sumbawanga mjini kwa tuhuma za kumgonga kwa gari mtoto Eliud
Steven (5) mkazi wa kijiji cha Kipundu Kala, Namanyere wilayani Nkasi.

Tukio lilitokea juzi saa 10:05 jioni katika kijiji hicho wakati mtoto huyo akiwa anatembea barabarani.

Kamanda Kyando alisema dereva huyo alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 790 DEM T aina ya Tata Truck, mali ya Assif Ashraf. Alimgonga mtoto huyo na kufa papo hapo.

Alisema chanzo cha ajalia ni uzembe wa dereva kushindwa kujali watumiaji wengine wa barabara, hivyo kukosa umakini akiwa
barabarani.

Chanzo:
Nipashe
 
Huyo dereva ataachiwa ila huyo alieacha hasira zichukue akili yake
Ana kazi sana huko gerezani
 
Back
Top Bottom