Mbaraka Mwinshehe Mwaruka

Mbaraka Mwinshehe Mwaruka

Nyimbo zake mpaka leo ukizisikiliza Utapenda kuendelea kuzisikiliza Mf kigeugeu matusi ya nini? Harusi imevunjika dk kleruu ester wangu dina uliapa nk
Kuna wimbo aliimba kuisifia Taifa Stars 1972, ni adimu sana lakini uko vizuri mno. Baadhi ya wachezaji ni Omar Mahadhi, Abdala Kibaden, Willy Mwaijibe, Makitoum, Zimbwe, Sunday na kitwana Manara nk.

Hakika Mbaraka bado ana jumbe nyingi katika nyimbo zake.
 


Soloist International Mbaraka Mwinshehe Mwaruka.

1970 aliporudi kutoka Expo akakuta maneno Dar es Salaam kuwa Morogoro Jazz imependelewa kuchaguliwa kwenda Osaka. Mbaraka akawaambia wenzake kuwa lazima warekodi nyimbo moja kama majibu kisha waende nyumbani Moro.

Wakarekodi katika studio za TBC ''Maonyesho Japani.''

Mle ndani Mbaraka was at his best guitar alilotia mle na ''melody'' yake si vitu vya kawaida.

Bahati mbaya sana ni kuwa recording ya TBC ilikuwa nzuri lakini ya Polydor ambayo ndiyo santuri yenyewe haikutoka vyema.

Kuna kitu katika muziki kinaitwa, ''chromatics,'' hii ni kama kupiga danadana katika soka. Ukijua danadana utakuwa na ''ball control,'' nzuri.

Sasa sikiliza hiyo ''chromatics,'' pale Mbaraka anaposema. ''Leo nalala Japan...'' nk.

Si wapigaji wengi wanaweza kusema huku vidole vikitembea kwenye, ''fret.'' Nilikuwa na hamu ya kuandika maisha ya Mbaraka na nilianza, ''interview,'' na marehemu Kurwa Salum, saxophonist wake na mtunzi wa nyimbo nyingi za Mbaraka ingawa jina lililotokea lilikuwa la Mbaraka.

Kurwa Salum alikuwa kila akija Dar es Salaam kutoka Morogoro alikuwa akija kunitembelea ofisini.

Wakati ule Kurwa Salum alikuwa kaacha muziki na akiuza mitumba Morogoro Sokoni.

Roho ilikuwa ikiniuma sana nilipokuwa nikimuona katika hali ile lya unyonge lakini alikuwa sala haimpiti.

Nilikuwa nikimstaajabisha sana Kurwa Salum nilipokuwa nikimwimbia ''chromatics,'' za saxophone lake kwenye nyimbo kama ile waliyoisifia timu ya Morogoro iliyochukua Taifa Cup.

Basi akicheka sana... Sikumaliza hii kazi nikaanza kitabu cha Abdul Sykes...In Shaa Allah atatokea mtafiti ataandika historia za hawa mabingwa wetu wa mindule.

Hadi leo Morogoro hawajawapa Mtaa Salum Abdallah wala Kurwa Salum. Katika band boys wa Morogoro Jazz kulikuwa na rafiki yangu wa utotoni Maneno Gisha.

Kurwa Salum ni Mmanyema.

Dah historia nzuri sana hii.
 
Back
Top Bottom