Mbaraka Mwinshehe Mwaruka: Soloist International

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,264
MBARAKA MWINSHEHE MWARUKA: SOLOIST INTERNATIONAL

Katika miaka ya 1980 nilitaka kuandika maisha ya Mbaraka Mwinshehe.

Nilianza utafiti kwa kufanya mazungumzo na jamaa wa Morogoro ambao waliishi na kwenda shule na Mbaraka.

Mmoja katika marafiki zangu ambao walinipa habari zake alikuwa Mbaraka Salum ambae alikuwa kipa wa Sunderland (Simba) sote tukiwa wakati huo waajiriwa wa East African Cargo Handling Services (EACHS).

Mwingine alikuwa Ramadhani Mdengo na yeye pia tulikuwa sote bandarini.
Ramadhani alinieleza kisa cha Mbaraka kutunga ile nyimbo, "Expo 70."

Mbaraka na Morogoro Jazz Band walipotua Dar-es-Salaam wakitokea Osaka, Japan wakakuta manung'uniko kuwa wamependelewa kuchaguliwa kwenda kwenye maonyesho ya Expo 70.

Mbaraka akawaambia wenzake wasirudi Morogoro hadi wamerekodi nyimbo Radio Tanzania.

Naam. Watu walipoisikia "Expo 70," hawakuwa na la kuongeza.

Alikuwapo na Ali Mwenda na mwisho Mohamed Haruna. Mohamed Haruna na Mbaraka walikuwa marafiki wakubwa sana.

"Mimi nilikuwa silipi kiingilio pale Morogoro Community Centre walipokuwa wakipiga Moro Jazz.

Nilikuwa nafika pale mapema na nikijua Mbaraka ataingia ukumbini muda gani.

Hapo muziki utakuwa ushaanza lakini Mbaraka anakuwa hajafika. Mara Mbaraka anafika na taxi anashuka mkononi kashika gitaa lake.

Mabaunsa wanapangua watu lango kuu Mbaraka apate kupita bila bughdha. Nitamwita kwa sauti, "Raks!"

Mbaraka atageuka kuniangalia kisha ataniashiria nimfuate.

Katikati ya dansi huku muziki ukiendelea zinatembea ala tupu na guitar la Mbaraka linatawala ukumbi, Mbaraka atashuka jukwaani kunifuata niliko huku anaendelea kupiga guitar tutazungumza kisha huyo atarudi jukwaani atamaliza nyimbo au ataingia kuimba.

Kichwa kikinivimba ukumbi mzima Mbaraka ukumbi mzima ananiona mimi peke yangu.

Nilipata simanzi kubwa sana Mbaraka alipotoka Morogoro Jazz Band."

Mohamed Haruna akanieleza kisa kilichomfanya Mbaraka atunge, "Jogoo la Shamba."

Kuna kijana fundi cherehani alitaka kumpiga Mbaraka.

Mdogo wake Mbaraka akaingia kati kumhami kaka yake na akamshughulikia yule kijana vilivyo.

Kila nikiwa na mazungumzo na hawa rafiki zangu nikiwa peke yangu naandika notes za mazungumzo yetu.

Nakumbuka Ramadhani kunieleza kuwa Mbaraka alikuwa na kawaida usiku hali ya hewa ikiwa imetulia alikuwa anafungua radio yake anatafuta stesheni za Congo kusikiliza muziki wa bendi za huko.

Siku zile radio zote zikirusha matangazo kwa Medium na Short Wave FM ilikuwa bado.

Mwenda siku moja nilimuuliza kuhusu Kurwa Salum mpiga saxaphone wa Morogoro Jazz.

Kwa masikitiko makubwa Mwenda alinifamisha kuwa Kurwa Salum yupo Morogoro sokoni amefungua biashara ndogo ya nguo za mitumba ameacha muziki kabisa.

Nilikwenda Morogoro kumtafuta Kurwa Salum.

Nilielekezwa kwake lakini mpashaji wangu habari kuona kuwa napata shida ya kuelewa anapoishi Kurwa Salum akanielekeza msikiti ambao Kurwa Salum akisali sala ya Alfajir.

"Ukienda kusali Fajr hapo utamkuta."

Nilisali pale msikitini lakini nilipomuuliza Kurwa Salum baada ya sala alikuwa keshatoka nje ya msikiti.

Nikaelekezwa nyumbani kwake.
Nilimkuta.

Kwa muda mfupi asubuhi ile nilizungumza na Kurwa Salum kama mtu tuliyefahamiana kwa miaka mingi.

Urafiki wangu na Kurwa Salum ulianza hapo.

Tukazungumza maisha yake na Morogoro Jazz Band na miaka yake na Mbaraka na muziki wao waliopiga pamoja na nyimbo walizotunga.

Akawa Kurwa Salum kila akija Dar es Salaam atanitafuta na tutazungumza mengi katika utunzi wa nyimbo alizopiga na Mbaraka kabla hajatoka na kuunda Super Volcano.

Kurwa Salum wakati mwingine akinihadithia wapi walipokuwa na mazingira yake.

Alinihafithia vipi alitunga nyimbo ya "Tambiko la Wahenga."

Kurwa Salum anasema walikuwa safarini sasa wako nyumba ya kufikia wageni yeye na Mbaraka wakawa wamekaa wanazungumza.

Nyimbo hii ikamjia kichwa akaanza kumwimbia Mbaraka.

Mbaraka akachukua guitar na kuanza kupiga akifuata sauti ya Kurwa Salum.

Hadithi hizi zilinivutia sana.
Nilikuwa nikimshangaza sana Kurwa Salum kwa yangu mengine.

Nilikuwa nazijua "chromatics" kadhaa za saxaphone alizopiga na Mbaraka akiwa kwenye "lead guitar."

Basi mimi nitampigia kwa mdomo saxophone yake. Kurwa Salum alikuwa akicheka lakini kainama anatingisha kichwa.

Nikipatia na nikipita mle mle alimopita tofauti nilikuwa sina ala mkononi.

Najua nilikuwa namtia simanzi na huzuni moyoni kwake namkumbusha ujana wake na namkumbusha Mbaraka.

Miaka ilikuwa imekwenda na Kurwa utu uzima ulikuwa umeshabisha hodi kwake.

Kurwa Salum alinifahamisha kuwa nyimbo nyingi zilizokuwa zimeandikwa jina la Mbaraka kama mtunzi ukweli mtunzi hakuwa Mbaraka ila yeye.

Ile kampuni waliokuwa wakirekodi walimwambia watauza sana kama jina la Mbaraka litawekwa kuwa mtunzi.

Wakati Mbaraka alipokuwa hai hapakuwa na matatizo yoyote katika kugawana fedha.

Matatizo yalikuja baada ya kifo cha Mbaraka.

Ile kampuni waliokuwa wakirekodi muziki wa Morogoro Jazz walimwambia hawawezi kumlipa kwa kuwa mkataba ni kati yao na Mbaraka ambae ndiye mwenye hati miliki.

Katikati ya utafiti nikaamua kuacha utafiti huu wa kitabu cha Mbaraka.

325568362_955116622121514_383747914631249350_n.jpg
 
Natamani WAZEE wetu wenye umri kama wako wangekuwa na TUNU ya uandishi kama yako
Na wangekuwa mtandaoni wangetupasha habari nyingi sana za zamani na nzuri
Hakika ZAMANI ilipendeza

ALLAH akupe umri mrefu afya njema HEKIMA ZAIDI na utimilifu upate kutuhabarishia HABARII nyingi zaidi
Hakika uandishi wako ni kama FIRAMU inayopita kichwani na kutengeneza taswila ya MOROGOLO ya zamani ilivyokuwa
na maisha mazuri ya ZAMANI yalivyopendeza hatukuwa na kitu/vitu Lakini tulifurahia
Hakika yalipendeza
FB_IMG_1673084585996.jpg
 
Natamani WAZEE wetu wenye umri kama wako wangekuwa na TUNU ya uandishi kama yako
Na wangekuwa mtandaoni wangetupasha habari nyingi sana za zamani na nzuri
Hakika ZAMANI ilipendeza

ALLAH akupe umri mrefu afya njema HEKIMA ZAIDI na utimilifu upate kutuhabarishia HABARII nyingi zaidi
Hakika uandishi wako ni kama FIRAMU inayopita kichwani na kutengeneza taswila ya MOROGOLO ya zamani ilivyokuwa
na maisha mazuri ya ZAMANI yalivyopendeza hatukuwa na kitu/vitu Lakini tulifurahia
Hakika yalipendezaView attachment 2481378
Mzimu,
Amin
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom