so huyu jamaa alieniuzia atakuwa anavutia biashara tu, anyway ngoja niangalie iyo niliyopanda ukuaji wake.
ila nakumbuka hata Malila alishazungumzia kuhusu mbao ya mwa40
Ni kweli Mwarobaini unatoa mbao za fanicha nzuri. Tatizo lililopo ni aina ya mti/spishi hasa. Si kila mwarobaini unaweza kuvunwa mapema kila mahali. Ni kama Mitiki inavyosumbua watu, ni kweli inamea ukanda wa Pwani, je soil properties, au humidity au kiwango cha mvua kimewekwa wazi?
Mkuu hujasema umeotesha wapi hiyo miarobaini ya majaribio. Na mimi nielekeze nikachukue mbegu za huyo jamaa, plan ni kuotesha eka mbili mwaka huu Mkuranga. Na bei nipe kabisa nimfuate.
Miti nimepanda huko huko Mkuranga, nilinunua miche pale mbagala mwisho nafikiri, kuna bonde moja wanaotesha miti, ukiwa unatokea mjini wako upande wako wa kulia. Bei kwa mche no 500. Nimeotesha michache ya majaribio, nitatoa feedback
Habari za Songea??mwarobaini, melia azedarach na jamii zake. (mboyo)kwa kisukuma, (mburumatale) kikelewe, kijita, nijuavyo mimi miti jamii hiyo hapo juu unao kua haraka ni melia azedarach,ukiupanda sehemu nzuri utavuna baada ya miaka 8, na gogo la chini utatoa 1x8=8