SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 43,707
- 60,760
Nakumbuka tangu Lissu alipopatwa na mkasa wa kushambuliwa kwa risasi na watu wasiyojulikana pale Dodoma, mtu kutoka familia yake aliyekuwepo ni mke wake.
Watu watatu walioondoka na mgonjwa kwenda Nairobi ni mke wake, Mbowe na Msigwa, wote hao hawajarudi Tanzania, wamepiga kambi huko ni jambo jema.
Wanachama wa CHADEMA hususan wabunge wanapishana barabarani na angani kutoka na kwenda Nairobi kumusabahi Lissu na camera za video kama kawa zinatuonesha, huo ndio utu. Hata wasio wana chama wa CHADEMA(Hongera sana Mh. Zitto Kabwe, wewe ni Shujaa kwenye sakata hili la Lissu, kwa jinsi Lissu alivyosimamia wewe kusulubiwa, sijui kama ni wewe ndiyo ungekuwa ulimtenda Lissu, Kwa roho ya Lissu sijui kama angethubutu hata kutaka kujua umelazwa wapi. Wewe ni mkomavu wa kisiasa) nao wanamiminika Nairobi.
Mbali na Mke wa Lissu, mwanafamilia mwingine aliyebahatika kumuona Lissu baada ya kushambuliwa ni nani? Kama ni hamna, kuna maswali mengi ya kujiuliza:
1. Lissu hana ndugu wengine?
2. Ndugu wapo ila hawana uwezo wa kiuchumi kuwawezesha kufika Nairobi?
3.Hawa waliopiga Kambi Nairobi wana uchungu na Lissu kuliko Ndugu zake?
4. Lissu hana mahusiano mazuri na ndugu zake? (hii halina uzito sana sababu kwa mila zetu za kiafrika, wakati matatizo ndipo tofauti zote katika familia zinapozikwa.
5. Kuna kitu familia hii inafichwa?
Jamani tutumie matukio kujipatia umaarufu wa kisiasa lakini tukumbuke vitu vidogo sana vinavyoweza kutufanya tusieleweke mbele ya jamii.
Tuoneshwe kupitia camera na video ndugu wakimtembelea ndugu yao hospitalini kama ambavyo wanasiasa wanavyoonekana huko.
Kwa mtazamo wangu, Huruma kwa Lissu ingeongezeka zaidi kama ndugu zake wangeonekana wakisitika pamoja na ndugu yao. Hawa wanasiasa tutaishia tu kusema wamepata pa kupatia umaarufu. "WANAFANYA SIASA"
Mnawashwa washwa saaaana, nawahakikishieni damu ya Lissu itawatesa sana siku zote za maisha yenu mpaka mnaingia kaburini hizo theories zenu za kipumbavu ndiyo zinazidi kudhihirisha ushiriki wenu katika jaribio la kumuua Lissu. Hivi mpaka sasa hamjajistukia kuwa mnaropoka ropoka ikiwa ni ishara ya kuchanganyikiwa kwenu. Mlilolitaka halikuwa kwani ile ni damu isiyo na hatia, na kama Mungu aishivyo hamtabaki salama.