'Mbakaji’ apigwa hadi kufa akiwa na bunduki mbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Mbakaji’ apigwa hadi kufa akiwa na bunduki mbili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 25, 2010.

  1. kilimasera

    kilimasera JF-Expert Member

    #1
    Dec 25, 2010
    Joined: Dec 2, 2009
    Messages: 3,073
    Likes Received: 17
    Trophy Points: 135
    WANANCHI wa Kitongoji cha Salamiti, Tarafa ya Mtimbira, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, wamemsulubu mkazi wa Kitongoji hicho, Joseph Mbulimika ( 40) kwa kipigo hadi kumsababishia kifo alipokuwa katika jaribio la kutaka kumwingilia mwanamke huku akiwa na
    bunduki mbili ndogo aina ya gobori.

    Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo alisema hayo Desemba 24 ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea mwishoni mwa Novemba mwaka huu na wananchi hao walimuua kwa kutumia vitu vya aina mbalimbali usiku wa manane baada ya kubainika kutaka kumbaka mwanamke ambaye jina tunalihifadhi.

    Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, kuwa marehemu huyo ambaye wakati akimvamia mwanamke huyo alikuwa na silaha mbili aina ya gobori ndogo zilizotengenezwa kienyeji ambazo hutumia risasi za bunduki ya aina ya shot gun.

    Alisema kuwa marehemu huyo ambaye alikuwa akijulikana kwa jina maarufu ‘Mapembe’ alipotoka kwenye klabu cha pombe usiku huyo aliingia ndani ya nyumba ya mwanamke huyo kwa nia ya kumwingilia kwa nguvu, lakini mwanamke huyo aligundua kuwa alikuwa na silaha kiunoni mwake.

    Kwa mujibu Kamanda huyo, mwanamke huyo baada ya kuona hali hiyo alimwambia kuwa alihitaji kwenda kujisaidia na ndipo alipokwenda kutoa taarifa kwa majirani ambayo walifika na kumvamia na kuanza kumpiga hadi kumsababishia mauti yake.

    Alisema wananchi hao waliziona bunduki hizo mbili zilizotengenezwa kiustadi ambazo zinaweza kuhifadhiwa kiunoni na kufichwa na shati ama makoti makubwa bila kugundulika kuwa mtu huyo amebeba silaha.

    Hata hivyo, alisema kuwa silaha hizo zilichukukliwa na Polisi wa Kituo cha Mtimbira na kufikishwa Kituo Kikuu cha Mahenge na baadaye kuletwa Makao ya Polisi Mkoa wa Morogoro kuhifadhiwa.

    Kamanda huyo amewaomba wananchi wenye taarifa za wahalifu kuzifikisha katika vituo vya polisi ikiwa ni ya sehemu ya kuimarisha ushirikiano uliopo wa Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi.
     
  2. m

    mamakunda JF-Expert Member

    #2
    Dec 25, 2010
    Joined: Jul 4, 2010
    Messages: 371
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 35
    Inasikitisha sana kusikia kuwa bado watu wanatumia nguvu ktk mapenzi katika dunia hii ya watu waelevu. Anyway amevuna alichokipanda pengine inaweza kuwa fundisho kwa wengine.
     
  3. G

    Gad ONEYA JF-Expert Member

    #3
    Dec 25, 2010
    Joined: Oct 26, 2010
    Messages: 2,641
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 135
    Waafrika hawajifunzi kutokana na historia!
     
  4. Gama

    Gama JF-Expert Member

    #4
    Dec 25, 2010
    Joined: Jan 9, 2010
    Messages: 9,223
    Likes Received: 1,412
    Trophy Points: 280
    mamakunda, tayari umekwisha hukumu kuwa alitaka mapenzi kwa nguvu?, ushahidi huu kiduchu umekuridhisha kuwa ni mbakaji?, je kama yeye na mwanamke huyu walikuwa ni wapenzi kisha wakatofautiana na mwanamke akaamua kutumia nguvu ya jamii kumusurubu?. Hivi kweli mbakaji angempa nafasi ya kwenda kujisaidia kwanza harafu ndo waendelee na mpz?. Natamani huyu mama angehojiwa vizuri ili unynyasaji huu mpya uliozuka hapa moro usitishwe(ninaushahidi wa wanaume kibao waliofanyiwa hivi moro, kwa wale wakwale mnaotembelea moro mujihadhari na hii style hasa mkitofautiana bei)
     
Loading...