Mbabazi: Uganda inahitaji ''Magufuli'' wake

Mbabazi: Uganda inahitaji ''Magufuli'' wake

Tuseme labda uko sawa lkn swali langu ni kwamba ni kwa nini wote au wengi wanafikiri kwamba ni Raisi bora hasa nje ya mipaka ya Tanzania? Kwa maana siyo mara ya kwanza kusikia watu wa nje ya Tanzania wakitamani kuwa na Raisi kama Magufuli na wengi wanamtumia kwenye Kampeni zao kuanzia Zambia, Malawi, Ghana mpaka Afrika Kusini kuna article nimesoma wakimtaka J. Zuma ajifunze ktk kwa Raisi Magufuli tena niliona wanafunzi wameshika poster wakiandamana AK na na jina la Raisi Maguguli sasa Je ni kwa nini? Labda kuna kitu wewe unakiona kumhusu Raisi Magufuli ambacho wengi wetu ndani na nje ya Tanzania hatukioni?
Kwa sababu mtu mwenye kiu ya kuona maji sehemu ambayo hamna maji hata akiona taswira inayotokana na jua kali kupiga ardhi ya jangwa (mirage) atakimbilia na kutumaini ni maji.

Hili halijaanza leo. Miaka ya 1990s dunia nzima ilikuwa inamuandika vizuri sana Museveni, angalia leo wanavyomsema.

Kuna article moja kwenye Wall Street Journal la Ijumaa au Jumamosi wameandika hiyo habari ya Museveni alivyowabadilikia watu.

Magufuli hatakuwa wa kwanza kuwahadaa watu.

Hao wanasiasa wa Afrika wote wanatapatapa tu, wakiona jina lolote jipya linaweza kuwapa kick wanalitumia.
 
M7 amesema atamminya nanii zake (korodani) Mbabazi
MBABAZI : UGANDA INAHITAJI “MAGUFULI” WAKE

Akiongea katika ndahalo wa wagombea urais nchini Uganda, mgombea wa Chama cha The Democratic Alliance (TDA), Waziri Mkuu wa zamani Amama Mbabazi amesema kuwa kwa sasa Uganda inahitaji Rais kama Dk. John Pombe Magufuli wa Tanzania.

Alipopewa muda wa kueleza maneno yake ya mwisho katika mdahalo huo uliofanyika usiku wa Jumamosi na kuhudhuriwa na wagombea nane, Amama Mbabazi alisema “Sio suala la upinzani kushika madaraka bali ni kuhusu kumpata mtu sahihi kwa ajili ya Uganda mpya. Tuna bahati kuwa hapa nchi jirani na sisi kuna mtu anaitwa JPM, yaani John Pombe Magufuli wa Tanzania.

Hivi sasa Uganda inahitaji mtu kama Magufuli ambaye ameonyesha wazi kwa matendo kuwa ataipeleka mbali Tanzania,Ni Rais anaonekana mzalendo sana.

Huku Rais anauyemaliza muda wake, Yoweri Museveni akisikiliza kwa makini, Mbabazi alisema “Sielewi ni kwanini Waganda tunakuwa wazito kujifunza kutoka madarakani. Ni lazima tufanye mabadiliko ili tuachane na mawazo mgando.”
 
Kwa sababu mtu mwenye kiu ya kuona maji sehemu ambayo hamna maji hata akiona taswira inayotokana na jua kali kupiga ardhi ya jangwa (mirage) atakimbilia na kutumaini ni maji.

Hili halijaanza leo. Miaka ya 1990s dunia nzima ilikuwa inamuandika vizuri sana Museveni, angalia leo wanavyomsema.

Kuna article moja kwenye Wall Street Journal la Ijumaa au Jumamosi wameandika hiyo habari ya Museveni alivyowabadilikia watu.

Magufuli hatakuwa wa kwanza kuwahadaa watu.

Hao wanasiasa wa Afrika wote wanatapatapa tu, wakiona jina lolote jipya linaweza kuwapa kick wanalitumia.


Lakini kwa Museveni sidhani kama ilikuwa ni mirage kila mtu alimsifu Museveni na walikuwa na sababu ya msingi kabisa ya kufanya hivyo kulingana na Historia ya Uganda wakati huwo, ni nchi ambayo ilikuwa haijawahi kuona utulivu tangu Uhuru, Museveni alilifanikisha hilo, alileta stability Uganda, kukawa na economic growth nzuri tu na ya kuridhisha hivyo ni kweli kabisa kwamba Museveni alikuwa ni success story by African standard wakati huwo!

Hivyo basi ingawaje sipingani na wewe inawezekana kuna unaloliona ambalo wengine hatulioni khs Magufuli lkn mimi kwa uzoefu wangu wa wanasiasa wa Tanzania na Kiafrika kwa ujumla naweza kusema kwamba Magufuli ni real deal na sababu ya kusema hivi kwangu mimi ni moja tu na wala siyo kwa sababu ya kufagia br. au safari za kushtukiza na mengineyo bali ni kwamba Magufuli anaelewa ni nini tatizo letu kama nchi, Magufuli anaelewa ni kwa nini hatuendi mbele na anaelewa ni nini tufanye ili tutoke hapa, hivyo kwangu mimi hii quality kubwa sana kwani ndiyo mwanzo wa kutatua tatizo, ni lazima kwanza ujue tatizo lilipo na kubwa kuliko yote Magufuli anajiamini, anaamini kwamba TUNAWEZA, kwa mara ya kwanza ktk maisha yangu nimemsikia Raisi wa Kiafrika akiongea kwa kujiamini kabisa kwamba hatupaswi kuwa omba omba bali tunapaswa kuombwa sasa huyu ni mtu anayejiamini sana ananikumbusha nilisoma kuhusu Kennedy aliposema we choose to go the moon and do other things not because they are easy but because they are hard... Test yangu yangu ya kwanza kwake ni bajeti yetu ijayo!
 
Wamchukue huyu magufuli wa Tanzania sisi tutamchukua lowassa wetu

Huoni hata aibu na Lowasa wako????

Akili imegandiana na Lowasa!!!!

kuna chochote cha kumkumbukia Lowasa, huoni akina, Mnyika, Lissu na akina Mdee Lowassa hayuko tena vinywani mwao???

Shame on you....
 
Back
Top Bottom