Wanajamvi nimeona leo tujadili mazuri ya CCM ambayo wameyafanya ili tuone upande mwingine wa shilingi maana hapa kila kitu kina pande mbili.
1. Uomoja kitaifa
2. Amani na Utulivu
3. Kuondoa udini
5. kuukema ukabila
6. Daraja la Kigamboni coming soon
7. kukubali upinzani
8. Ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wote ambapo collateral ni deposits zao za NSSF na PFPF PPF
9. Ujenzi wa babrara nchi nzima
10. Ujenzi wa Udom na vuo vikuu vingi vya kumwaga.
11.
12.
13.
14.
Yaani wewe umeongea kinyume kabisa umoja gani wa kitaifa uliko kwasasa...Wazanzibar wanataka nchi yao, tulisikia kisiwa kimoja huko mwanza kilijitangazia nchi yake na hata huko singida kuna sehemu walijitangazia nchi yao huo ndiyo umoja wa kitaita kwanini watu walifikia kujitangazia nchi yao ndani ya nchi, je huko Loliondo si kuna nchi ndani ya nchi.
2. watu wameuwawa sana na jeshi la polisi mfano Arusha kwenye maandamano, Arumeru vijana wanne walokotwa wakiwa wameuliwa kwa kunyongwa na mauwaji mpaka leo yanaendelea, huko mara mauwaji kila mara....
3. udini umeshamili kuliko kipindichocho kama una bisha sikiliza redio Imani.
4. Udini unakemewa kinafiki huku CCM ikijaribu kutumia ukabila na udini kuwa gawa watanzania.
5.Daraja kama watajenga siyo kitu cha kujivunia kiivyo ukizingatia ni mifuko ya jamii ambazo ni haki yetu licha ya kwamba tuna lipa kodi lakini imeshindwa kulisaidia taifa wameingilia kwenye mifuko hii kutukamua.....
7. kukubali upinza si kwa mapenzi ya kikwete ni ya mataifa makubwa ukizingatia kila kukicha anaenda kuombaomba...
8.....hili silijui
9.barabara zilianza kujengwa kipindi ya kuuza mashika ya umma kipindi cha mpaka kikwete akaingia na chuki zake binafsi akamwondoa Magufuli madokeo yake ikawa ujenzi wa kilomita 1 bil 1.6 kutoka milioni 700 kama sikosei lakini naona sasa hivi Magufuli karudi amepuguza kwa kasi ya jabu hivyo kama kikwete angekuwa makini angechuguza na nina uhakika kuna watu wange nyea debe.
10.Vyuo vya kumwaga hebu tuwekee hapa na vilianza lini kujengwa.