Mazungumzo Usingizini

Mi kuna mwanangu, usingizini huwa anaongea sana. Utakuta sema A, sema Ba, sema Cha. Sasa ukimuuliza anasema mwalimu kashika fimbo kubwa sana na asiyetamka anamchapa
 
Hahahahaha...mimi kuna jamaa chuo alikuwa Akiangalia muvi ya kikorea baadae anairudia tena yote kama ilivyo.

Ukimsikiliza unaelewa muvi nzima bila hata kuiangalia.

Utaskia aigooooo..pehaaaa.....ugumjiii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hhahahaha aigooo umenichekesha sana mkuu
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
mimi ni mmojawapo huwa naongea sana vitu visivyoeleweka nikiwa usingizini,nilikuwa sijui mpaka pale nilipoanza kulala na ndugu zangu wakiamka asubuhi wananiambia nilikuwa naongea peke yangu huku wakinicheka na kukumbushia niliyokuwa naongea. vivyo hivyo wakati naingia sekondari ndo ikawa balaa nikilala na roommates usiku naongea mwenyewe usingizini mpaka kingereza ndani yake. wenzangu walikuwa wanachukia wengine wanacheka basi hivyo tu. mpaka sasa nimekuwa mkubwa lakini hii tabia naambiwa bado ninayo na anayeniambia ni mke wangu kuwa ni naongeaga peke yangu usiku usingizini au hata mchana nikilala.

ajabu ya hali hii ni kwamba hizi sio ndoto yaani nikiamka asubuhi huwa sikumbuki kabisa na hata mtu akinikumbusha huwa nakataa kuwa sijaongea. ila baada ya kuwa naambiwa hali hii na mke wangu huwa sibishi na siulizi nilikuwa naongea nini maana najua utakuwa nu upuuzi tu.

hali ya kushangaza ni kuwa ukiwa katika hali hii endapo mtu aliye macho akikuongelesha basi utajibu kwa maneno yasiyoeleweka. nimefanya uchunguzi nimegundua kuwa ni hali ya kawaida tu kibinadamu na kila mmoja ana kiwango chake naskia wengine huwa mpaka wanatoka kitandani anakwenda sebleni au chooni bila kujitambua.

yangu hayo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…