Mazombi Znz yaanza kuvuruga Amani

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,011
Kuna kikosi zanzibar kinajulikana kama mazombi wameanza kupiga na kutesa wananchi na kuwatisha wananchi.

Jeshi la police lipo kimya, matukio haya yamekuwa yakilalamikiwa na wananchi na polisi kukanusha kutokuwa na taarifa.

Vikosi hivi vinaongozwa na Waziri mmoja wa SMZ ambaye ndio mwenye jukumu la vikosi hivi ya kiharamia.

Kwa wapenda amani lazima tulaani na tunamuomba Rais wa Jamhuri ya muungano John Magufuli aliingilie mara moja kwani yeye ndio mwenye jukumu kama Amiri Jeshi Mkuu.
1454094157694.jpg
1454094168317.jpg
1454094179238.jpg
1454094191632.jpg
 
Ukishakula nyama ya mtu huwezi kuacha kamwe~Nyerere
Kinachoendelea znz ni kibri kile kile cha mwaka 2000 damu ilimwagika na ICC hakupelekwa mtu.
Believe me or not Safari hii ataenda mtu,Maradhi ya kibri ni mabaya kuliko virusi vya ZiKa
 
Hili la zanzibar litawaletea laana mby watawala wetu mkuu
Yetu macho japo hatupendi mabaya kutokea
 
linapokuja swala la zenji mdomo wangu unapata kigugumizi kusema kweli...! ndio maana nazipita hizi nyuzi kama sizioni .. na sipendi mtu ani tag
 
Hili swala lingekua lina maana kwenye serikali hii Maalim Seif angekua ameshahojiwa na polisi juu ya anachokijua alisema kwenye ile hotuba yake juu ya hivi vikundi na sehemu vilivyopo ,Lakini serikali yetu iko Radhi kuzuia Maiti isizikwe mpaka mahakama iruhusu ila sio kufuatilia mambo kama haya
 
Hao mazombi ni wanajeshi ?? Maana naona Land Rover ya kijani na kuna mtu kashikilia SMG ???
 
Mleta mada umenikumbusha wimbo wa ZOMBIE wa fela kuti. Alikuwa anawaimba askari wanaotumwa kutesa raia na wanatekeleza bila kufikiria wanafanya nini. Kama misukule.
 
Hili swala lingekua lina maana kwenye serikali hii Maalim Seif angekua ameshahojiwa na polisi juu ya anachokijua alisema kwenye ile hotuba yake juu ya hivi vikundi na sehemu vilivyopo ,Lakini serikali yetu iko Radhi kuzuia Maiti isizikwe mpaka mahakama iruhusu ila sio kufuatilia mambo kama haya


I Salute you Che!
 
Madaraka ni kitu cha
ajabu sana. Ukimwangalia
Dr She in sura yake
unapata picha kuwa no
MTU mcha
Mungu,mwadilifu,mwenye
huruma ambaye hata
kuchinja kuku wa kitoweo
inaweza kuwa mtihani
kwake.
Ijumaa ukimuona
alivyokunja miguu
msikitini mbele za Mola
wake utauona ukaribu
wake na Mola wake na
kuwa pengine njia ya
kwenda peponi ni nyeupe
kwake.
Lakinimadaraka
yanamgeuza mtu huyu
hata hawezi kufikiri tena
juu ya hatari ya hiki
wakifanyacho na hatima
ya maisha ya watu, wake
kwa waume na watoto.
Hebu akienda leo msikitini
amwombe mola wake yeye
ndiye amuongoze nini
afanye tofauti na
anavyoambiwa na chama
chake. Hukumu yake
haitaihusisha NEC au CCM
siku ile ikifika/
 
linapokuja swala la zenji mdomo wangu unapata kigugumizi kusema kweli...! ndio maana nazipita hizi nyuzi kama sizioni .. na sipendi mtu ani tag
Wewe kama Mimi suluhushu la migogoro yote ya ZNZ ilikuwa katiba ya Warioba. Wao wakaipuuza wakidai serikali ya Mapinduzi haitolewi kwa makaratasi ya kura! Leo hii dhambi hiyo inawatafuna
 
Back
Top Bottom