'Mazoea' kwa wanandoa ni chanzo cha ndoa kuingia doa?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Habari wakuu,

Nimekuwa msomaji wa uzi nyingi sana humu JamiiForums hasa MMU.

Twende kwenye hoja;

Nimegundua kuwa ktk ndoa kumekuwa na kitu 'mazoea' yani mfano ni tofauti kabisa na kipindi cha uchumba.

Kipindi cha uchumba mnakuwa mbali hivyo hupelekea kukumbukana.

Mnapokuwa ktk ndoa mnakuwa karibu mara nyingi na hivyo kufanya umjue vyema mume au mke wako na kuzoea kila kitu kwake.

Wakati mwingine wanandoa wanakuwa sio wapenzi tena na kugeuka kuwa kaka na dada.

Hii husababisha mwanaume kutafuta mchepuko huko nje na kuanzisha mahusiano..na huko anafurahia maana hajauzoea mchepuko.

Nawasilisha hoja..

Karibuni kwa mjadala..
 
Ulichokisema ni kweli kabisa mama... muhimu ni kutengeneza vitu vinavyowapa furaha ya kudumu na sababu za kuwa pamoja...sio ngono pekee.. maana kuna watu wameoana lakini kinachowaunganisha ni ngono tu... labda na watoto..

Wanandoa wenzangu nawashauri tafuteni vitu vinavyowaunganisha.... mfano fanyeni michezo pamoja(sports/games), mazoezi pamoja, jiungeni clubs muwe wanachama (reading clubs, arts clubs), mjitahidi kusafari pamoja(adventures hata zile fupi fupi) etc

Kwa ufupi muwe wabunifu tu mtaenjoy... ikibidi tafuteni movie za kihindi ziwafundishe mahaba!Lol
 
ndio maana hata asali ukila sana unaikinai, same applies huko kwenye ndo bora uwe single ukihitaji unatafuta chap chap:D
 
lakini wazee wetu wameishi maisha ya ndoa mpaka miaka 35 ya ndoa...
tujifunze kwao...mbona inawezekana...!!..kama ni kuzoeana basi level hizo ni mbali kweli kweli...!!
 
Jukumu la kuhakikisha mume hakinai ni ubunifu wa mwanamke, mke akimuonyesha mume wake ubunifu na mume atainyesha utundu kwa mke wake wake,
Pia mke unapaswa kujipenda na kupendeza siyo kwakuwa umeshaolewa ndiyo ujiachie utoke mpaka michikizi na usafi duni, mume anatoka nje.
 
Hayo ndio madhara ya mapenzi ya kifilipino,
hapo ili mapenzi yadumu inabidi kuwe na na mikiki mikiki kila mwisho wa wikiiii!
Mapenzi lazima yawe hot hot, sio kilasiku mnabembelezana na kuleteana maua(huo ubwege)
Mnatakiwa kila baada ya siku mbili mnaanzisha tifu alafu mnakokotana mnakwenda kuyamaliza ufukweni au hotel flani hivi
 
Jukumu la kuhakikisha mume hakinai ni ubunifu wa mwanamke, mke akimuonyesha mume wake ubunifu na mume atainyesha utundu kwa mke wake wake,
Pia mke unapaswa kujipenda na kupendeza siyo kwakuwa umeshaolewa ndiyo ujiachie utoke mpaka michikizi na usafi duni, mume anatoka nje.
Acha uvivu jukumu la ndoa ni la pande zote mbili, ubunifu kila siku afanye mwanamke unadhani hachoki afu na wewe je,..huwezi kubuni?!
 
Watu waridhike na walivyonavyo na wajue kuzoeana ni lazma watu mnaishi wote mazoea yatakosekana vipi..ni hali ya kuikubali.,
 
Acha uvivu jukumu la ndoa ni la pande zote mbili, ubunifu kila siku afanye mwanamke unadhani hachoki afu na wewe je,..huwezi kubuni?!
Mimi jukumu langu ni kunishawishi kisha nikupe utundu wangu, sasa umetoka kuoga univalie pensi la jeans na gauni ulale nalo + kupishana lugha na visirani automatic najua hakuna sex, lakini univalie night dress nyegesi inayoonyesha maungo yako au khanga moja nyegesi nitaona unachelewa kupanda kitandani.
 
Maisha ni zaidi ya tendo la ndoa,visirani umeambiwa wanavyo wanawake tu?Kuna wanaume anaamka asubuhi kanuna na gubu juu
Ili mahusiano yanawiri pande zote mbili waweke juhudi
Akiweka juhudi mke tu alafu mume haoni umuhimu huyu mke atachoka,mume pia awajibike kuona nini kinamfurahisha mkewe na akifanye,
Likewise mke amfurahishe mumewe
 
Ndiyo maana kwa wenzetu waarabu mke hafanyi kazi kazi yoyote zaidi ya kujiremba, hina na akijua mumewe karibu anarudi anajifukiza udi, mume akirudi anapokelewa na lugha nzuri, kama ana stress zinaisha, ndiyo maana wanazaa haraka haraka, mke yuko kwaajiri ya kumtumikia mume tu.
 
Maisha ni zaidi ya tendo la ndoa,visirani umeambiwa wanavyo wanawake tu?Kuna wanaume anaamka asubuhi kanuna na gubu juu
Ili mahusiano yanawiri pande zote mbili waweke juhudi
Akiweka juhudi mke tu alafu mume haoni umuhimu huyu mke atachoka,mume pia awajibike kuona nini kinamfurahisha mkewe na akifanye,
Likewise mke amfurahishe mumewe
Kabisaaa, wafurahishane
 
Space space space,hobby hobby hobby hobby,kuoana haina maana ndo muwe pamoja kila mda km ambvyo tunafundishwa ilo ndo tatizo
 
Back
Top Bottom