Maziwa ya unga ya lato hayana ubora!

Maziwa ya unga ya lato hayana ubora!

Crocozilla

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
469
Reaction score
335
Naandika makala hii kwa masikitiko makubwa sana maana rais wetu anahaha kila siku kuhakikisha nchi yetu inakuwa ya viwanda. Akifanikiwa itasaidia kutuweka huru na hizi bidhaa dhaifu toka nje ya nchi.

Mfano nimenunua maziwa ya unga ya Lato ambayo yanaonyesha yametengenezwa 2016 na kwenye kopo lake yanaonyesha yataharibika 2018.

Cha kusikitisha leo ni 2017 maziwa ukitengenezea chai yanakuwa kama maziwa mgando yaliyowekwa kwenye maji moto. Nimeyahifadhi ili kuyapeleka TFDA kwa uchunguzi zaidi. Inauma sana sana maana pesa ya shida kweli!

d331181d9a2562c59a217644400d9971.jpg
3f53c646f8d4de5c9a83602d2008ffdc.jpg

ad192d7e643b57d11a564b30d36d7532.jpg
 
Pole sana aisee,
Ila leo ni tarehe 15/10/2017, utanunuaje kitu cha Mwezi wa tano mwaka Jana??
Yaani kitu kina karibia Mwaka na Nusu na ni aina ya Chakula unanunua vipi??
 
Sio machungu? Yaliwahi nikuta siku ya kwanza wanangu wamezaliwa mama Yao maziwa yalikuwa hayatoki mpaka Giza laingia nikaenda nunua Yale lactonini cjui, tukawapa watoto, walilia sana, hatukuja shida nini hadi cku ya tatu c nikayaonja? Dah unaijua mboga flani inaitwa mchunga? Ule unanafuu, kurudisha super market wakaniomba risiti, nikawapa, afu wakataka niletee za kuleta, kusema ukweli nilikuwa na hasira mno, nilichokifanya hapo wenyewe hawatosahau nahisi watakuwa wamekoma kuweka vitu vilivyopita muda wake
 
Kuna mazikwa kweli kwenye kopo?
Solution ni kununua maziwa halisi ya ng'ombe
 
Tuache kulalamika sana,,chochote kinachotengenezwa na binadamu,,kunakuwaga na error kidogo,,
 
Kuna mazikwa kweli kwenye kopo?
Solution ni kununua maziwa halisi ya ng'ombe
Maziwa ya n'gombe dar sio salama sana,wauzaji wanaongeza maji na wengine wanachanganya na ya unga wanaongeza blue band utaona kama cream wanangu waliharisha sana kupata ya n'gombe fresh labda jirani yako awe anafuga,lakini kununua kwa wenye baskeli tutaendelea kujuta.
 
Maziwa ya makopo robo tatu ni majanga tafuta fresh japo nayo wamejaza maji
 
Pole mkuu , me nanunua hiyo Lato kila mwezi ila naangalia sana expire date . Hiyo labda itakuwa manufacturing error au muuzaji kaya pack upya ili auze hata kama ni mabovu.

Maziwa ya kopo au ya unga yakitengenezwa vizuri ni mazuri kuliko ya kukamua ng’ombe (liquid) kwa sababu zifuatazo.

Maziwa ya ng’ombe yanakuwa machafu mda mwingi na ni vigumu kuyaamini Kama humjui muuzaji

Ng’ombe akila sumu basi na maziwa yana uwezekano wa kutoka na sumu, kuna pathogens/vidudu wengi sana Kama harmful bacteria ambapo kwenye processed milk hivi vidudu huondolewa kwa njia mbali mbali

Maziwa ya ng’ombe tena wa kisasa hayana madini ya kutosha Kama calcium , vitamin A, D n.k mengi sehem kubwa ni Maji

Kumbuka maziwa ya unga yako fortified ( yaan yamepimwa na kuongezewa madini katika usawa unaotakiwa)

Njia salama ya kutunza maziwa ni unga..

Kwa upande mwingine maziwa ya kopo ni expensive kidogo kulinganisha na ya mtaani pia yanaweza kukosa ladha ambayo unaweza kuwa umeizoea
 
daa me nilikuwaga nayapenda maziwa ya unga sana kazini nikiweka na kahawa naenjoy siku yaligeuzia kibao niliumwa tumbo cjui yale maziwa yalitolewa wapi hadi Leo nayaona kama kituo cha polisi hayo ya ng'ombe yakupima ndo kabisa sigusi at list tanga fresh kidogo nikizidiwa. otherwise mpaka kijijini kwetu ndo nakunywaga
 
Saa nyingine waweza laumu latto ila wewe ukawa mwenye tatizo au duka ulilonunua

Mara nyingi maziwa yanaharibika kutokana na storage

unaweza ukawa uluyafungua au mtoto aliyafungua akasahau kufunga vizuri yakapigwa na upepo

pili ulipo yanunua yawezekana mwenye duka aliweka stoo yenye joto kali
 
Back
Top Bottom