Ewe mama, ewe baba kama hakuna tatizo la msingi hakikisha mwanao ananyonya maziwa ya mama tu miezi sita ya mwanzo. Hii ni kwa manufaa ya afya yake ya sasa na ya baadae. Tuache mazoea, eti kisa wazazi wetu walitukuza ivo, kumbuka mfumo wa maisha umebadilika tofauti na enzi zile za wazazi wetu. Mama onesha upendo wako kwa kumnyonyesha mwanao maziwa yako tu miezi sita ya mwanzo, baba urijali wako utadhibitika utaposimamia hili likatekelezeka. Inawezekana sana.