Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Mazishi ya Mbunge Viti Maalum Dkt. Elly Macha leo mkoani Arusha.
Viongozi mbalimbali walihudhuria akiwemo Mwenyekiti wa Chadema Taifa ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe Mbowe,Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Mhe Lowassa, Mhe Spika wa Bunge Job Ndugai na Naibu wake Tulia Ackson. Na pia baadhi ya Wabunge na mawaziri walishiriki.
==========UPDATES.
SEHEMU YA HOTUBA YA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB) NA MWENYEKITI WA CHADEMA TANZANIA MHE. FREEMAN MBOWE (MB) KWA NIABA YA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI, KWA FAMILIA YA DR. MACHA (RIP), BUNGE, SERIKALI NA WATANZANIA WOTE, WAKATI WA KUMUAGA MAREHEMU KWENYE VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA.
"Ni wiki tatu zimepita tangu tulipopata Kwa mara ya kwanza taarifa mbaya, taarifa za huzuni, za kuondokewa na Dr. Macha ambapo kwetu CHADEMA alikuwa mjumbe wa kamati kuu, inahitaji muda mwingi sana kumtafakari na kumjadili Mama Macha.
Msiba kila siku kwetu ni darasa na Kwa namna ya kipekee niwashukuru Spika, Naibu Spika, na Katibu wa Bunge Kwa namna walivyoubeba msiba huu na Serikali Kwa ujumla wake akiwepo Balozi Dr. Asha Rose Migiro.
Nitoe shukrani Kwa wabunge kupitia makundi mbalimbali, mmekuwa wepesi sana kutufariji si tu Kwa Michango, lakini Salamu, Mama Macha licha ya kuwa mlemavu lakini hakutukwaza na tunapendana na kuheshimiana Kwa kuogopa Kifo.
Tutumie kifo kama Funzo, mapenzi haya yasiwe mapenzi ya mashaka, Urafiki huu usikome baada ya kumlaza Mama Macha, wabunge, ofisi ya Bunge na Serikali kwenye Upendo, uvumilivu na ushirikiano, jambo lolote linageuka kuwa jambo jema na jambo baya linageuka kuwa jambo zuri.
Mama Macha amewasaidia watu wengi sana wakiwamo Yatima, na tuwaombee uvumilivu. Mama yake mzazi tumuombee uvumilivu Kwa kumwona anayemtegemea sana akiwa amemwacha. Amefanya mengi ya kimiujiza, ametuacha tukitafakari thamani ya maisha yake, Asante Mungu Kwa uhai wa Mama Macha."