Mazingira yangu ni yapi?

Mazingira yangu ni yapi?

Swami linalotangulia Mazingira yangu ni yapi ni ... Jirani yangu ni nani? Tulipofundisha kwenye dini zetu kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe wengi walidhani jirani ni yule unayepakana naye mahali unapoishi.. Lakini sivyo! Jirani yako ni yule anayekuwa karibu nawe popote.. Iwe kazini, michezoni, safarini, sehemu za starehe. Ibadani nknk.

Tunapoaswa kutunza mazingira yetu.. Haimaanishi pale tunapoishi tuu, au makazini kwetu nk.. Mazingira yetu ni sawa na jirani .. Ulipo yupo, ulipo yapo..popote ulipo wakati wowote hayo ndio mazingira yako.. Yatunze.. Usijione uko kwenye gari hivyo uchafu wako uutupe nje.. Na kudhani huko hakukuhusu! Ni makosa makubwa kufikiri hivyo.

Dhana ya utunzaji mazingira ni pana sana na serikali haijawekeza vya kutosha kwenye hii kaliba.. Jamii imepotoshwa kwa kuzoezwa kuwa utunzaji wa mazingira ni kupanda miti na kwenda kusafisha fukwe za bahari au kwenda kufyeka, kulimia na kuokota uchafu maeneo ya jumuiya kama hospital nk huku mkipigwa picha na kutangazwa kwenye vyombo vya habari.. Huko sio kutunza mazingira huko ni kufanya usafi.

Kama vile unavyojipenda wewe mwenyewe basi na mazingira yako unapaswa kuyapenda hivyo hivyo.
Kutunza mazingira ni zaidi ya kupanda miti.. Kutunza mazingira kunaanza nawe mwenyewe mahali unapoishi, mahali unapokuwa, mahali unapopita.. Mpangilio mbaya wa vitu ndani ya nyumba yako huo sio utunzaji wa mazingira.. Ni uchafuzi..

  • Kurundika mavitu yasiyotumika tena ni uchafuzi wa mazingira
  • Kujisaidia sehemu zisizo stahili ni uchafuzi wa mazingira
  • Kutofuata utaratibu wa vitu popote ni uchafuzi wa mazingira
  • Kutupa chochote mahali pasipo pake ni uchafuzi wa mazingira
  • Kupenga kamasi, kutematema mate, makohozi nk ni uchafuzi wa mazingira

Mamlaka zetu zimejaa watu wasiojiweza na kujitambua... na badala ya kuwekeza kwenye elimu na ufahamu wa mazingira ninini na yanatunzwaje. Zinakimbilia kuweka sheria zenye adhabu kali na zinazotoa mianya ya rushwa na upigaji kwenye ngazi zote kuanzia kwenye viwanda na maeneo ya wafanyabiashara mpaka chini kabisa mitaani

Mwekezaji anapata cheti cha mazingira lakini hakidhi vigezo..Halmashauri zimeweka sheria ndogondogo na kuajiri wanamgambo wachovu wa fikra na ufahamu kuzisimamia.

Wamewatengenezea mianya ya kunyanyasa watu na kula rushwa. Kutozingatia kanuni za mipango miji hilo pekee ni uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa baraka za mamlaka.. Barabara za waenda kwa miguu na sehemu za maegesho na dharura zimejaa wafanyabishara ndogondogo ambao kimsingi hawapaswi kuwa hapo

Maeneo yanabadilishwa matumizi kiholela kabisa na ukiangalia inapingana kabisa na sheria za mipango miji...huu ni uchafuzi mkubwa wa mazingira unaonyamaziwa na mamlaka za nchi...!
Hakuna juhudi zozote za kuwekeza kwenye elimu ya utunzaji wa mazingira.. Na ikitokea ni siasa tupu na ujinga mwingi... Sheria na kampeni za kuwa na dust bins kwenye vyombo vya usafiri sijui vimeishia wapi
Mazingira ni maisha
Mazingira ni afya
Mazingira ni mafanikio
Bila afya hakuna maisha na bila maisha hakuna mafanikio
Mazingira yako ndio afya na maisha yako..ndio ustawi na mafanikio yako.. Yatunze yakutunze!
Heshima kwako Mshana Jr.
Kuna hili suala la Mabadiliko ya Tabianchi na Athari zake kwa mazingira yetu. Nanukuu:-
"Hakuna juhudi zozote za kuwekeza kwenye elimu ya utunzaji wa mazingira.. Na ikitokea ni siasa tupu na ujinga mwingi... Sheria na kampeni za kuwa na dust bins kwenye vyombo vya usafiri sijui vimeishia wapi
Mazingira ni maisha
Mazingira ni afya
Mazingira ni mafanikio
Bila afya hakuna maisha na bila maisha hakuna mafanikio
Mazingira yako ndio afya na maisha yako..ndio ustawi na mafanikio yako.. Yatunze yakutunze!"
Mwisho wa kunukuu
e.g. Kama ni kupanda miti - basi ipandwe miti inayoendana na hali iliyopo kwa mfano tupande miti ya Asili inayostahimili ukame na mioto kichaa (ref. ilivyotokea Huko Rombo) ile miti iliyokuwepo i.e. iliyopandwa kwa mazoea haikuhimili moto-Asili uliotokea.
  • kama ni kilimo basi yapandwe mazao yanayostahimili ukame na sio kupanda tu kwa mazoea.
  • Kama ni ufugaji ; tufuge aina na idadi ya mifugo kulingana na uwingi wa malisho yaliyopo na iwe pia ni mifugo yenye tija zaidi.
Kwa kifupi ni kwamba nasi Wanadamu tuliopo kizazi hiki tubadilike na kuachana na kufanya mambo kwa mazoea- "Business as Usual" Matumizi ya rasilimali zetu yazingatie mabadiliko ya Tabianchi tunayoenda nayo ili kuweka uwiano sawa kwetu sisi na kwa vizazi vijavyo.
 
Kongole nyingi kwako ndugu
Mshana Jr kutoka moyoni kabisa nathubutu kusema wewe ni Mmoja wa WAZALENDO wa kweli wa taifa hili,
Achana na wale wachumia tumbo waliojificha Kwenye kivuri Cha siasa uchwara za kiuwendawazimu!

Nadiriki kutoa pongezi za dhati Kwa mchango wako umeandika kiuzalendo Sana mpaka umenifanya nitafakari mambo mengi Sana yanayoendelea hapa Nchi ikiwemo na Serikali kushindwa hata kupangilia miji na vijiji na kusabisha yote Hayo uliyoyaandika hapa maana naamini Kama wangekua makini Kwenye Hilo swala Hayo ya utunzaji mazingira yangekuja automatically!

Niishie hapa aaaaagh!
 
Asante sana Dumas the terrible [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Heshima kwako Mshana Jr.
Kuna hili suala la Mabadiliko ya Tabianchi na Athari zake kwa mazingira yetu. Nanukuu:-
"Hakuna juhudi zozote za kuwekeza kwenye elimu ya utunzaji wa mazingira.. Na ikitokea ni siasa tupu na ujinga mwingi... Sheria na kampeni za kuwa na dust bins kwenye vyombo vya usafiri sijui vimeishia wapi
Mazingira ni maisha
Mazingira ni afya
Mazingira ni mafanikio
Bila afya hakuna maisha na bila maisha hakuna mafanikio
Mazingira yako ndio afya na maisha yako..ndio ustawi na mafanikio yako.. Yatunze yakutunze!"
Mwisho wa kunukuu
e.g. Kama ni kupanda miti - basi ipandwe miti inayoendana na hali iliyopo kwa mfano tupande miti ya Asili inayostahimili ukame na mioto kichaa (ref. ilivyotokea Huko Rombo) ile miti iliyokuwepo i.e. iliyopandwa kwa mazoea haikuhimili moto-Asili uliotokea.
  • kama ni kilimo basi yapandwe mazao yanayostahimili ukame na sio kupanda tu kwa mazoea.
  • Kama ni ufugaji ; tufuge aina na idadi ya mifugo kulingana na uwingi wa malisho yaliyopo na iwe pia ni mifugo yenye tija zaidi.
Kwa kifupi ni kwamba nasi Wanadamu tuliopo kizazi hiki tubadilike na kuachana na kufanya mambo kwa mazoea- "Business as Usual" Matumizi ya rasilimali zetu yazingatie mabadiliko ya Tabianchi tunayoenda nayo ili kuweka uwiano sawa kwetu sisi na kwa vizazi vijavyo.
Kwa kifupi ni kwamba nasi Wanadamu tuliopo kizazi hiki tubadilike na kuachana na kufanya mambo kwa mazoea- "Business as Usual" Matumizi ya rasilimali zetu yazingatie mabadiliko ya Tabianchi tunayoenda nayo ili kuweka uwiano sawa kwetu sisi na kwa vizazi vijavyo.[emoji1545][emoji1545][emoji1534]
 
Tunazo kampuni rasmi za usafi zilizopewa kutunza, kuhifadhi na kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali mijini.. Hizi kampuni ni kichekesho na ni kichefuchefu mpaka unajiuliza
Je wenye hizi kampuni wana weledi na uzoefu wa kutosha kwenye hii kazi muhimu sana?
Je wana vitendea kazi na nguvu kazi ya kutosha?
Je wanaowapa hizi tenda wanajiridhisha uwezo wa wanaowapa kazi ama ndio 10% inaamua kila kitu?
Maana haiwezekani uchafu uzolewe barabarani na kutupwa juu ya bustani zilizoko pembezoni na katikati ya barabara .. Mwisho wa siku bustani zinageuka matuta makubwa ya uchafu uliogandiana
Still watu hawachukuliwi hatua na ikija tenda nyingine wanapewa![emoji848][emoji2827]
 
Back
Top Bottom