Mazingira yangu ni yapi?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
177,297
2,000
Swami linalotangulia Mazingira yangu ni yapi ni ... Jirani yangu ni nani? Tulipofundisha kwenye dini zetu kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe wengi walidhani jirani ni yule unayepakana naye mahali unapoishi.. Lakini sivyo! Jirani yako ni yule anayekuwa karibu nawe popote.. Iwe kazini, michezoni, safarini, sehemu za starehe. Ibadani nknk.

Tunapoaswa kutunza mazingira yetu.. Haimaanishi pale tunapoishi tuu, au makazini kwetu nk.. Mazingira yetu ni sawa na jirani .. Ulipo yupo, ulipo yapo..popote ulipo wakati wowote hayo ndio mazingira yako.. Yatunze.. Usijione uko kwenye gari hivyo uchafu wako uutupe nje.. Na kudhani huko hakukuhusu! Ni makosa makubwa kufikiri hivyo.

Dhana ya utunzaji mazingira ni pana sana na serikali haijawekeza vya kutosha kwenye hii kaliba.. Jamii imepotoshwa kwa kuzoezwa kuwa utunzaji wa mazingira ni kupanda miti na kwenda kusafisha fukwe za bahari au kwenda kufyeka, kulimia na kuokota uchafu maeneo ya jumuiya kama hospital nk huku mkipigwa picha na kutangazwa kwenye vyombo vya habari.. Huko sio kutunza mazingira huko ni kufanya usafi.

Kama vile unavyojipenda wewe mwenyewe basi na mazingira yako unapaswa kuyapenda hivyo hivyo.
Kutunza mazingira ni zaidi ya kupanda miti.. Kutunza mazingira kunaanza nawe mwenyewe mahali unapoishi, mahali unapokuwa, mahali unapopita.. Mpangilio mbaya wa vitu ndani ya nyumba yako huo sio utunzaji wa mazingira.. Ni uchafuzi..

 • Kurundika mavitu yasiyotumika tena ni uchafuzi wa mazingira
 • Kujisaidia sehemu zisizo stahili ni uchafuzi wa mazingira
 • Kutofuata utaratibu wa vitu popote ni uchafuzi wa mazingira
 • Kutupa chochote mahali pasipo pake ni uchafuzi wa mazingira
 • Kupenga kamasi, kutematema mate, makohozi nk ni uchafuzi wa mazingira

Mamlaka zetu zimejaa watu wasiojiweza na kujitambua... na badala ya kuwekeza kwenye elimu na ufahamu wa mazingira ninini na yanatunzwaje. Zinakimbilia kuweka sheria zenye adhabu kali na zinazotoa mianya ya rushwa na upigaji kwenye ngazi zote kuanzia kwenye viwanda na maeneo ya wafanyabiashara mpaka chini kabisa mitaani

Mwekezaji anapata cheti cha mazingira lakini hakidhi vigezo..Halmashauri zimeweka sheria ndogondogo na kuajiri wanamgambo wachovu wa fikra na ufahamu kuzisimamia.

Wamewatengenezea mianya ya kunyanyasa watu na kula rushwa. Kutozingatia kanuni za mipango miji hilo pekee ni uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa baraka za mamlaka.. Barabara za waenda kwa miguu na sehemu za maegesho na dharura zimejaa wafanyabishara ndogondogo ambao kimsingi hawapaswi kuwa hapo

Maeneo yanabadilishwa matumizi kiholela kabisa na ukiangalia inapingana kabisa na sheria za mipango miji...huu ni uchafuzi mkubwa wa mazingira unaonyamaziwa na mamlaka za nchi...!
Hakuna juhudi zozote za kuwekeza kwenye elimu ya utunzaji wa mazingira.. Na ikitokea ni siasa tupu na ujinga mwingi... Sheria na kampeni za kuwa na dust bins kwenye vyombo vya usafiri sijui vimeishia wapi
Mazingira ni maisha
Mazingira ni afya
Mazingira ni mafanikio
Bila afya hakuna maisha na bila maisha hakuna mafanikio
Mazingira yako ndio afya na maisha yako..ndio ustawi na mafanikio yako.. Yatunze yakutunze!
 
Kilele9

JF-Expert Member
Jun 1, 2017
1,356
2,000
Swami linalotangulia Mazingira yangu ni yapi ni ... Jirani yangu ni nani?
Tulipofundisha kwenye dini zetu kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe wengi walidhani jirani ni yule unayepakana naye mahali unapoishi.. Lakini sivyo! Jirani yako ni yule anayekuwa karibu nawe popote.. Iwe kazini, michezoni, safarini, sehemu za starehe. Ibadani nknk...!!!!

Tunapoaswa kutunza mazingira yetu.. Haimaanishi pale tunapoishi tuu, au makazini kwetu nk.. Mazingira yetu ni sawa na jirani .. Ulipo yupo, ulipo yapo..popote ulipo wakati wowote hayo ndio mazingira yako.. Yatunze.. Usijione uko kwenye gari hivyo uchafu wako uutupe nje.. Na kudhani huko hakukuhusu! Ni makosa makubwa kufikiri hivyo..!

Dhana ya utunzaji mazingira ni pana sana na serikali haijawekeza vya kutosha kwenye hii kaliba.. Jamii imepotoshwa kwa kuzoezwa kuwa utunzaji wa mazingira ni kupanda miti na kwenda kusafisha fukwe za bahari au kwenda kufyeka, kulimia na kuokota uchafu maeneo ya jumuiya kama hospital nk huku mkipigwa picha na kutangazwa kwenye vyombo vya habari.. Huko sio kutunza mazingira huko ni kufanya usafi.

Kama vile unavyojipenda wewe mwenyewe basi na mazingira yako unapaswa kuyapenda hivyo hivyo..!
Kutunza mazingira ni zaidi ya kupanda miti.. Kutunza mazingira kunaanza nawe mwenyewe mahali unapoishi, mahali unapokuwa, mahali unapopita.. Mpangilio mbaya wa vitu ndani ya nyumba yako huo sio utunzaji wa mazingira.. Ni uchafuzi.. Kurundika mavitu yasiyotumika tena ni uchafuzi wa mazingira
Kujisaidia sehemu zisizo stahili ni uchafuzi wa mazingira
Kutofuata utaratibu wa vitu popote ni uchafuzi wa mazingira
Kutupa chochote mahali pasipo pake ni uchafuzi wa mazingira
Kupenga kamasi, kutematema mate, makohozi nk ni uchafuzi wa mazingira

Mamlaka zetu zimejaa watu wasiojiweza na kujitambua... na badala ya kuwekeza kwenye elimu na ufahamu wa mazingira ninini na yanatunzwaje...zinakimbilia kuweka sheria zenye adhabu kali na zinazotoa mianya ya rushwa na upigaji kwenye ngazi zote kuanzia kwenye viwanda na maeneo ya wafanyabiashara mpaka chini kabisa mitaani

Mwekezaji anapata cheti cha mazingira lakini hakidhi vigezo..Halmashauri zimeweka sheria ndogondogo na kuajiri wanamgambo wachovu wa fikra na ufahamu kuzisimamia.. Wamewatengenezea mianya ya kunyanyasa watu na kula rushwa..!
Kutozingatia kanuni za mipango miji hilo pekee ni uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa baraka za mamlaka.. Barabara za waenda kwa miguu na sehemu za maegesho na dharura zimejaa wafanyabishara ndogondogo ambao kimsingi hawapaswi kuwa hapo

Maeneo yanabadilishwa matumizi kiholela kabisa na ukiangalia inapingana kabisa na sheria za mipango miji...huu ni uchafuzi mkubwa wa mazingira unaonyamaziwa na mamlaka za nchi...!
Hakuna juhudi zozote za kuwekeza kwenye elimu ya utunzaji wa mazingira.. Na ikitokea ni siasa tupu na ujinga mwingi... Sheria na kampeni za kuwa na dust bins kwenye vyombo vya usafiri sijui vimeishia wapi
Mazingira ni maisha
Mazingira ni afya
Mazingira ni mafanikio
Bila afya hakuna maisha na bila maisha hakuna mafanikio
Mazingira yako ndio afya na maisha yako..ndio ustawi na mafanikio yako.. Yatunze yakutunze!

"Mamlaka zetu zimejaa watu wasiojiweza na kujitambua... na badala ya kuwekeza kwenye elimu na ufahamu wa mazingira ninini na yanatunzwaje...zinakimbilia kuweka sheria zenye adhabu kali na zinazotoa mianya ya rushwa na upigaji kwenye ngazi zote kuanzia kwenye viwanda na maeneo ya wafanyabiashara mpaka chini kabisa mitaani

Mwekezaji anapata cheti cha mazingira lakini hakidhi vigezo..Halmashauri zimeweka sheria ndogondogo na kuajiri wanamgambo wachovu wa fikra na ufahamu kuzisimamia.. Wamewatengenezea mianya ya kunyanyasa watu na kula rushwa..!

Kutozingatia kanuni za mipango miji hilo pekee ni uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa baraka za mamlaka.. Barabara za waenda kwa miguu na sehemu za maegesho na dharura zimejaa wafanyabishara ndogondogo ambao kimsingi hawapaswi kuwa hapo"
Msisitizo
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
177,297
2,000
Kaka Kuna mahali umeharibu mazingira nini..
Leo niache niko kwenye maombolezo ya kumbukumbu ya baba wa Taifa la Tanyanyika marehemu hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mchonga meno mzee wa Mwitongo aliyetawala taifa hili kwa miaka 36 na kufariki mwaka 1999 tarehe 14 mwezi wa kumi huko London uingereza kwenye hospital ya wazungu iitwayo St. Thomas akiwa na umri wa miaka 77 kamili na mwili wake kurejeshwa nchini Tanyanyika na ndege ya serikali rubani akiwa mwanamama mtanzani Aitwaye Anna Mwakasege...NASEMA NIACHE!
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
19,143
2,000
Leo niache niko kwenye maombolezo ya kumbukumbu ya baba wa Taifa la Tanyanyika marehemu hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mchonga meno mzee wa Mwitongo aliyetawala taifa hili kwa miaka 36 na kufariki mwaka 1999 tarehe 14 mwezi wa kumi huko London uingereza kwenye hospital ya wazungu na mwili wake kurejeshwa nchini Tanyanyika na ndege ya serikali rubani akiwa mwanamama mtanzani mkuria...NASEMA NIACHE!
Umeanza kutoa ya moyoni Sasa..
Hizi taarifa za juujuu tu utaleta mpk zile za kilingeni subiri akupige tukio jengine mbona bado..😂
 
Mkuu wa Kibiti

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
735
1,000
Mkuu@mshanajr umetoa ujumbe murua sana kuhusu utunzaji wa mazingira jukumu ambalo ni muhimu katika mkakati wa kuendeleza kizazi.Tukitunza mazingira tunajiweka kwenye njia hakika ya muendelezo wa kizazi chetu kinyume chake tukiacha jukumu hili tunatengeneza siku za mateso na uangamivu kwa kizazi kijacho.Bahati mbaya wanasiasa wanataka madaraka tu hawapendi siasa hivyo hawajali sana kuhusu usalama wetu dhidi ya maslahi yao.Muhimu kwao ni wanapata nini zaidi kutoka kwetu na si wanafanya nini kwaajili yetu.Tutunze mazingira leo kwa maslahi ya kizazi kijacho
 
bievinii

JF-Expert Member
May 12, 2021
562
1,000
Leo niache niko kwenye maombolezo ya kumbukumbu ya baba wa Taifa la Tanyanyika marehemu hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mchonga meno mzee wa Mwitongo aliyetawala taifa hili kwa miaka 36 na kufariki mwaka 1999 tarehe 14 mwezi wa kumi huko London uingereza kwenye hospital ya wazungu na mwili wake kurejeshwa nchini Tanyanyika na ndege ya serikali rubani akiwa mwanamama mtanzani mkuria...NASEMA NIACHE!
Aiseee....!!!kongole KWAKO muombolezaji mzoefu
Kongole Sana Tena nasema kongole
 
Lyamba lya mfipa

Senior Member
May 13, 2021
120
225
Swami linalotangulia Mazingira yangu ni yapi ni ... Jirani yangu ni nani? Tulipofundisha kwenye dini zetu kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe wengi walidhani jirani ni yule unayepakana naye mahali unapoishi.. Lakini sivyo! Jirani yako ni yule anayekuwa karibu nawe popote.. Iwe kazini, michezoni, safarini, sehemu za starehe. Ibadani nknk.

Tunapoaswa kutunza mazingira yetu.. Haimaanishi pale tunapoishi tuu, au makazini kwetu nk.. Mazingira yetu ni sawa na jirani .. Ulipo yupo, ulipo yapo..popote ulipo wakati wowote hayo ndio mazingira yako.. Yatunze.. Usijione uko kwenye gari hivyo uchafu wako uutupe nje.. Na kudhani huko hakukuhusu! Ni makosa makubwa kufikiri hivyo.

Dhana ya utunzaji mazingira ni pana sana na serikali haijawekeza vya kutosha kwenye hii kaliba.. Jamii imepotoshwa kwa kuzoezwa kuwa utunzaji wa mazingira ni kupanda miti na kwenda kusafisha fukwe za bahari au kwenda kufyeka, kulimia na kuokota uchafu maeneo ya jumuiya kama hospital nk huku mkipigwa picha na kutangazwa kwenye vyombo vya habari.. Huko sio kutunza mazingira huko ni kufanya usafi.

Kama vile unavyojipenda wewe mwenyewe basi na mazingira yako unapaswa kuyapenda hivyo hivyo.
Kutunza mazingira ni zaidi ya kupanda miti.. Kutunza mazingira kunaanza nawe mwenyewe mahali unapoishi, mahali unapokuwa, mahali unapopita.. Mpangilio mbaya wa vitu ndani ya nyumba yako huo sio utunzaji wa mazingira.. Ni uchafuzi..

 • Kurundika mavitu yasiyotumika tena ni uchafuzi wa mazingira
 • Kujisaidia sehemu zisizo stahili ni uchafuzi wa mazingira
 • Kutofuata utaratibu wa vitu popote ni uchafuzi wa mazingira
 • Kutupa chochote mahali pasipo pake ni uchafuzi wa mazingira
 • Kupenga kamasi, kutematema mate, makohozi nk ni uchafuzi wa mazingira

Mamlaka zetu zimejaa watu wasiojiweza na kujitambua... na badala ya kuwekeza kwenye elimu na ufahamu wa mazingira ninini na yanatunzwaje. Zinakimbilia kuweka sheria zenye adhabu kali na zinazotoa mianya ya rushwa na upigaji kwenye ngazi zote kuanzia kwenye viwanda na maeneo ya wafanyabiashara mpaka chini kabisa mitaani

Mwekezaji anapata cheti cha mazingira lakini hakidhi vigezo..Halmashauri zimeweka sheria ndogondogo na kuajiri wanamgambo wachovu wa fikra na ufahamu kuzisimamia.

Wamewatengenezea mianya ya kunyanyasa watu na kula rushwa. Kutozingatia kanuni za mipango miji hilo pekee ni uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa baraka za mamlaka.. Barabara za waenda kwa miguu na sehemu za maegesho na dharura zimejaa wafanyabishara ndogondogo ambao kimsingi hawapaswi kuwa hapo

Maeneo yanabadilishwa matumizi kiholela kabisa na ukiangalia inapingana kabisa na sheria za mipango miji...huu ni uchafuzi mkubwa wa mazingira unaonyamaziwa na mamlaka za nchi...!
Hakuna juhudi zozote za kuwekeza kwenye elimu ya utunzaji wa mazingira.. Na ikitokea ni siasa tupu na ujinga mwingi... Sheria na kampeni za kuwa na dust bins kwenye vyombo vya usafiri sijui vimeishia wapi
Mazingira ni maisha
Mazingira ni afya
Mazingira ni mafanikio
Bila afya hakuna maisha na bila maisha hakuna mafanikio
Mazingira yako ndio afya na maisha yako..ndio ustawi na mafanikio yako.. Yatunze yakutunze!
Nakubali comrade mshana Jr
 
Kirumberumbe

JF-Expert Member
Mar 28, 2017
371
500

Mkuu; hii imekaa vizuri sana.👍Kwanza nakupongeza halafu Naongezea kidogo tu kwamba pia upigaji wa mziki usiojali wenzako(majirani zako) nayo ni kero. Utakuta mtu wa saloon hasa za wanaume kafungulia mziki kwa sauti kubwa bila kujua na kujali kwamba sio watu wote wanapenda mziki huo au aina ya mziki alioweka au mziki kwa sauti kubwa ki-vile i.e. hii nayo ni kero kwa wengine na hata huumiza masikio ki-afya (ref. sound frequency rafiki kwa ear drum kwa binadamu na wengine wanayo matatizo ya moyo) kwa baadhi ya watu.
Jambo lingine ni utumiaji wa maneno au matusi bila kujali kuheshimu(Heshima) kwa watu waliopo. Utamkuta kijana au mtu mzima (Me au Ke) anaongea hovyo kwa sauti kubwa bila kujali wanaomzunguka au watakao sikia. Hata humu Jf wapo watu wanaoandika matusi/maneno bila kujali kwamba hiyo ni kero kwa wasomaji wengine wanaopita humu mtandaoni. Ingefaa kujua kwamba jirani yako (Mazingira yako) ni pamoja na kile kinachotoka ndani(rohoni) mwako. Tujue kwamba unapoandika ni unaongea na watu wengi na huwaoni. Tujitahidi kutumia lugha ya staha au lugha iliyofichika kupeleka matusi (kama kweli ni lazima utumie Tusi) badala ya kuyaanika kikamilifu hadharani as if unadhani kwamba watu wengine hawayajui matusi wewe ndo unawaonesha kuyajua na kuyatumia.
Samahani kama nimewakwaza baadhi ya watu.
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
177,297
2,000
Mkuu; hii imekaa vizuri sana.Kwanza nakupongeza halafu Naongezea kidogo tu kwamba pia upigaji wa mziki usiojali wenzako(majirani zako) nayo ni kero. Utakuta mtu wa saloon hasa za wanaume kafungulia mziki kwa sauti kubwa bila kujua na kujali kwamba sio watu wote wanapenda mziki huo au aina ya mziki alioweka au mziki kwa sauti kubwa ki-vile i.e. hii nayo ni kero kwa wengine na hata huumiza masikio ki-afya (ref. sound frequency rafiki kwa ear drum kwa binadamu na wengine wanayo matatizo ya moyo) kwa baadhi ya watu.
Jambo lingine ni utumiaji wa maneno au matusi bila kujali kuheshimu(Heshima) kwa watu waliopo. Utamkuta kijana au mtu mzima (Me au Ke) anaongea hovyo kwa sauti kubwa bila kujali wanaomzunguka au watakao sikia. Hata humu Jf wapo watu wanaoandika matusi/maneno bila kujali kwamba hiyo ni kero kwa wasomaji wengine wanaopita humu mtandaoni. Ingefaa kujua kwamba jirani yako (Mazingira yako) ni pamoja na kile kinachotoka ndani(rohoni) mwako. Tujue kwamba unapoandika ni unaongea na watu wengi na huwaoni. Tujitahidi kutumia lugha ya staha au lugha iliyofichika kupeleka matusi (kama kweli ni lazima utumie Tusi) badala ya kuyaanika kikamilifu hadharani as if unadhani kwamba watu wengine hawayajui matusi wewe ndo unawaonesha kuyajua na kuyatumia.
Samahani kama nimewakwaza baadhi ya watu.
Jambo lingine ni utumiaji wa maneno au matusi bila kujali kuheshimu(Heshima) kwa watu waliopo. Utamkuta kijana au mtu mzima (Me au Ke) anaongea hovyo kwa sauti kubwa bila kujali wanaomzunguka au watakao sikia. Hata humu Jf wapo watu wanaoandika matusi/maneno bila kujali kwamba hiyo ni kero kwa wasomaji wengine wanaopita humu mtandaoni. Ingefaa kujua kwamba jirani yako (Mazingira yako) ni pamoja na kile kinachotoka ndani(rohoni) mwako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom