Mazal Tov Yisrael – Congrats Israel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mazal Tov Yisrael – Congrats Israel

Discussion in 'International Forum' started by Ronal Reagan, May 13, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  Kesho Jumamosi tarehe 10 Iyyar 5771, yaani tarehe 14 Mei 2011, Israe inaadhimisha miaka 63 ya kuzaliwa kwake. Mnamo tarehe14 May 1948 (5 Iyyar 5708), Waziri Mkuu wa Israel David Ben Gurion alisoma Tangazo la Uhuru wa Israel lijulikanalo Israeli Declaration of Independence (Kiyahudi huitwa, Hakhrazat HaAtzma'ut). Ben Gurion alitangaza rasmi kuzaliwa kwa taifa la Israel, ikiwa ni miaka mitatu tu tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia mwaka 1945.

  Israel ni nini na nani hasa? Israel ni nchi, na Israel ni watu. Lugha yao ni Kiyahudi (lugha ya zamani huitwa Kiebrania). Neno au jina Yahudi latokana na neon Yudah au Yehudah, ambalo ni moja ya makabili halisi 12 ya watoto wa Yakobo au Israel. Yuda ni kabila ambalo baadaye, mwanzoni mwa utawala wa mfalme Rehoboam (mtoto wa mfalme Suleman), nchi ya Israel ilipogawanyika sehemu mbili, ilikuja kuwa dola. Kaskazini waliitwa Israel (ndiko walikokaa kabila kumi) na kusini waliitwa Yuda (ndiko kabila 2 za Yuda na Benyamini walikaa). Makao makuu ya Kaskazini yalikuwa mji wa Samaria, makao makuu ya kusini yalikuwa Yerusalem. Waliendelea hivyo (kuwa falme mbili) kwa karne nyingi. Pia neno/jina Yahudi ni utambulisho wa dini yao rasmi.

  Duniani humu ni nchi au jamii chache sana zenye historia iliyo hai ya kuishi mfululizo (yaani bila kuangamia au kupotea) na kuwa na utambulisho wao. Tena katika historia, hakuna nchi (watu) iliyowahi kuchukuliwa nje ya mipaka yao na kubaki na utambulisho wao na kisha baadaye kurudi katika nchi yao ya asili na kuweka tena mizizi na kuchipuka. Israel walichukuliwa utumwani Ashuru (Syria zamani), walichukuliwa utumwani Babeli (Iran/Iraq) na baadaye kwa takriban miaka 1,900 walitawanywa kila pembe ya dunia tangua mwaka 70 A.D. (kufuatia Warumi kubomoa hekalu lao) hadi 1948.

  Hivyo napenda kugusia kwa uchache sana jambo moja tu wakati huu wa kusherehekea miaka 63 ya kuzaliwa Taifa la Israel. Umuhimu wa Yerusalem kwa Israel. Ijulikane hapa kuwa MUNGU alipoichagua Israel kuwa nchi yake kadhalika aliichagua Yerusalem kuwa mji wake na makao yake. Hakuna nchi makini isiyo na mji mkuu (kitovu cha nchi). Israel na Yerusalem ni kitu kimoja, havitenganishiki wala kugawanyika. Yerusalem ni mji mkuu wa Israel milele. Amen.

  Israel ina historia ya ajabu, ya kushangaza, kusikitisha, ya kusisimua na ya kipekee. Nawiwa kuwake dondoo zifuatazo:-
  i) Ndio nchi au watu (kama jamii) ambao MUNGU aliwachagua na kujitambulisha kwao na kufanya nao maagano. Kwamba Yeye ni MUNGU wao, na wao ni watu wake na amewapa eneo husika la ardhi kuwa milki yao.

  ii) Katika vita kuu ya Pili ya dunia, takwimu zinaonyesha Wayahudi milioni sita waliauwa. Tukio hilo lilikuwa ni moja ya chachu ya kuharakisha mchakato wa uundwaji taifa la Israel, ili Wayahudi wasiendelee kuuawa, kuwa wakimbizi wasio na matumaini ya kuiona nchi ya babu na baba zao.

  iii) Israel ni nchi ya kidemokrasia, na Serikali yake huongozwa na Waziri Mkuu anayetokana na chama kilichoshinda uchaguzi. Benyamini Netanyahu ni WM wa 32 wa Israel. Bunge la Israel linaitwa Knesset. Pia Israel ina rais ambaye ni kiungo kati jamii na serikali yao. Inaundwa na majimbo nane kisha mikoa, wilaya na vijiji. Tofauti na jirani zake, Israel haina hazina ya mafuta, gesi au madini.

  iv) Israel imestawi sana katikati ya uadui mwingi na vita toka kwa majirani zake na hata mbali ya mipaka yao. Ndio dola la kidemokrasia ya kweli Mashariki ya Kati (MK). Ndio dola lenye uchumi imara zaidi MK, Ndio dola lililoendelea zaidi kisayansi, kielimu, kiviwanda na kilimo MK. Ndio dola lenye nguvu kijeshi MK.
  v) Kuelekea Vita ya Siku Sita – 1967 nchi za Kiarabu chini ya Abdel Nasser wwa Misri zilitaka kufunga ukurasa wa "historia" na "aibu" ya kushindwa vita ya 1948, zilizopelekea kuzaliwa taifa la Israel.

  vi) Vita ya Siku Sita – 1967, Kiyahudi "Mil'hement sheshet Hayamim", ilianza tar 5 Juni 1967 na kumalizika tar 10 Juni 1967. Tukio moja kubwa katika vita hiyo ni Israel kuukomboa mji wa Yerusalem na kuurudisha katika milki yake.

  vii) Uhalali, msingi na utashi wa kuwepo kwa Israel na watu wake hautegemei maazimio ya UN, au America au maoni ya mataifa. Uhalali na msingi wake ni maagano MUNGU wao aliyofanya nao. Ndio maana kila tunaposherehekea kuazaliwa kwa Israel pia huadhimisha uwezo wa neno "Waache watu wangu waende", ambalo Musa alimwambia Farao wa Misri.

  Tukitaka kujifunza tuna mengi tunaweza kujfunza kwa Israel kama watu na kama nchi.

  MUNGU IBARIKI ISRAEL! MUNGU WALINDE WATU WAKO ISRAEL!
   
 2. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  Naomba kujua kiwango cha uhusiano wa Tz na Israel kwa sasa, je kimefika ngazi ya ubalozi mdogo au bado uadui pale pale?
   
 3. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mungu ibariki Israel.
  Uhusiano wa kibalozi na Israel urudishwe. mbona Kenya wao wanao? Kuvunja ubalozi na Israel ni kati ya makosa machache aliyofanya mwl JKN. Sasa ni wakati wa kurekebisha makosa.
   
 4. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  Amen.

  Ni vizuri Tz kurejesha uhusiano an Israel, kwa mawazo yangu si tu ni vizuri bali ni muhimu sana.
  Katika nyanja za kilimo, madini na viwanda kuna vitu vingi sana ambavyo Tz ingefaidika badala ya hizi nchi za 10% ambazo ki ukweli zinaganga njaa ktokana na udhaifu na tamaa ya viongozi wa Tz. Rites ya India ni mfano mmoja mdogo wa kuwapa waganga njaa miradi ya maendeleo.

  Kenya wanao ubalozi na mashusiano mazuri sana na Israel, nchi ile kiuchumi iko mbali zaidi ya Tz...pamoja na kasoro na ufisadi ambao nao unaikabili Kenya.
   
 5. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hakika wewe ni mtumishi wa Mungu aliye hai, mtu anayeichukia Israel anamchukia Mungu aliyewachagua.
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Toa kinyesi chako hapa.
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  Ngwendu, sio lazima usome hii wala uchangie thread isiyokuhusu
   
 8. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  Tanzania kwa katiba yake haina dini (sio ya dini fulani). Tz ina uhusiano wa kibalozi na wa karibu sana na Mamlaka ya Palestina (toka enzi za Arafat). Hatuuiti uhusiano huo kuwa wa kidini. Lakini linapokuja suala la Israel ghafla hoja na hisia za udini huja....kwamba mtawakwaza watu wa dini fulani.

  Swali, Je hii ni sawa? Je hali hii iachwe iendele au kuna haja ya kuirekebisha sasa? ....... najiuliza tu, najabribu kutafuta majibu
   
 9. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,812
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  nasikiaga wana kiburi na ubaguzi usio na mfano, hasa sisi watu weusi!
   
 10. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Umeandia pumba, sijui kwasababu unataka tujui kuwa unajua kiyehudi? Anyway hujui uliandikalo zaidi ya kujionesha wajua sana kiyehudi. Mpaka nyerere akaondoa uhusiano wakibalozi sio kitu cha mchezo. Kama unaakili timamu usingeshabikia. Hivi huoni jinsi wayahudi wanavyowaua mamia kwa maelfu majirani zake? hivi unajua shida wanayopata wale watu watu wamashariki ya kati.?
  karibia theluthi ya wanaotoa maamzi ktk government ya US ni mayahudi na kumbuka wao ni 7% tu ya wamerekani zaidi ya mil 300. Na nguvu iliyopo pale Isreil huiwezi kuitofoutisha ya US hata kidogo. Je wajua ni Mabilion mangapi yanaenda Isreil kutoka US? Unajua hata Misri ilikuwa ikipata mgao huo kutoka US kwa ajili ya kuilinda Isreil? Isreil inamilike silaha za nyuklia, je umeshawahi kusikia US na wenzake hata wakiziongelea? what about Iraq (hata kama hazipo), Libya, Iran etc.
  Au unaandika tu ili kufurahisha umma? Je hutaki hii dunia iwe nchi salama ya kuishi? hata Obama alipoingia madarakani alikuja na kile alichokiita two natios solution, je imeishia wapi? Unajua kwa nini alisulender tofauti na mwanzoni alivyosema kuwa serikali ya Jeruselem isitishe ujenzi wa makazi ya walowezi wa kiyehudi?
   
 11. umkhonto

  umkhonto Member

  #11
  May 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Israeli ina uhusiano wa kibalozi na Tanzania,ingawa haina Resident_embassador hapa Tanzania.ubalozi wao ulioko kenya unahudumia nchi za Uganda, Tanzania, Zambia, Malawi and Seychelles pia.Nadhani ubalozi wa Tanzania Cairo unahudumia Israel pia.
  kwa kuzingatia itifaki ya JF,napiga hodi pia kwani hii ni post ya kwanza.
   
 12. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu kama hii thread imekukera ipotezee tu, ila kwa sie wengine tunajua kuwa Israel imefungamanika na ama baraka au laana, na sie wenzio tumeichagua Baraka.
   
 13. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sawa mkuu.
   
 14. A

  Ame JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Ana heri kila aiombea amani Israel maana amani ya Mungu aliye hai ipitayo ufahamu wa mwandamu itakaa pamoja naye. Naye ulinzi wake utakuwa imara kama milima iizungukavyo Yerusalemu; Mungu atakuwa kwake kama ukuta wa moto kumzunguka na huo utukufu ndani yake. Ijapo shida ama adha hatatikisika milele mana bwan amefanyika kwake kuwa jiwe na kila mwenye kuangukiwa nalo humponda na kumsaga kama majivu!

  Unaheri wewe Yerusalemu maana ndiwe ule mji wa ahadi ambapo wana wa Mungu aliye hai watafanya makao yao na kumwabudu Mungu wao milele na hapo watapata mafao yao nao wataponywa na kupozwa magonjwa yao yote wala kifo hakitatawala tena. Bwana Yesu ndiye atakuwa mwanga wao na wala jua hata mwezi havitakuwepo tena bali mwanga wa mwana kondoo wa mungu, kuhani milele kwa mfano wa Melkizedeck! Amani ya Israel na iwafikie wote walio na mapenzi mema na hili Taifa la Mungu; Amina!
   
 15. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wapalestina asili yao ni Wafilisti, ndugu zake akina Goliathi aliyeuawa na Daudi, asili yao ni Gaza, kwa hiyo kudai maeneo mengine ya Israeli ni ndoto ya mchana! Watazeekea na kufia kwenye kambi za wakimbizi mpaka hapo watakapotambua kwamba Yerusalemu ni mji mmojawapo wa Miji ya Israeli (1Falm. 11:32) na sio Mji wa Wafilisti!
   
 16. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,600
  Likes Received: 6,767
  Trophy Points: 280
  Hebu jifungueni nyinyi kutoka utumwa wa Kifikra!, hautabarikiwa wewe kwa sababu ya kuipenda Israel, bali utabarikiwa kwa kupenda haki na kuitenda, Kumwabudu Mwenyezi Mungu wa haki na pia kutenda mema.

  Mara nyingi Kwenye biblia Israel imeadhibiwa kwa Ukaidi wao, hebu rejeeni kwenye Biblia jinsi kabila kuu la Efraim wakati huo lilipoadhibiwa kwa kwenda kinyume na Mwenyezi Mungu. Ikiwa nyinyi mnaipenda Israelm basi pendeni Matendo mema na siyo jina!!. maana hata Masiha Alipindua meza za Wauza fedha kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu, alichukizwa nao kwa sababu ya matendo yao japo hao wauza fedha ni Wana wa Israel, alichukizwa na Wafarisayo wanafiki japo nao ni wana wa Israel. na nyinyi basi chukizweni na Matendo!, na pia pendezweni na matendo!. Waisralei wakinyensha mvua ya mabomu Gaza kuweni fair, je wanahaki na wanastahili kufanya hivyo?
   
 17. M

  Masauni JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2011
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtakapo ona mti wa mizeituni(Israel) umeanza kuchanua(israel inarudi katika nchi yake ya asili) tambueni mwisho wa dunia umekaribia. Ndugu ngwendu!! huelewi unachoongea!! Mungu akusamehe
   
 18. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #18
  May 14, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Israel huwa wanarusha mabomu baada ya uchokozi wa mabomu ya kujitoa muhanga ya Hamas na magaidi wengine! Kila mara Israel wanapotaka kufikia amani na Wafilisti (Wapalestina), kama walivyosaini mikataba ya amani na Jordan na Misri, Hamas na magaidi wengine hutibua mambo! Ukiwaambia Hamas wakuchoree Ramani ya Palestina watachora Ramani inayoonesha kwamba hakuna nchi iitwayo Israel! Kwa hiyo Wafilisti watakula jeuri yao wenyewe!
   
 19. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #19
  May 14, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Waisrael wamebarikiwa na Mungu, hata ukibisha-Neno lake litasimama daima. Kinachotutafuna kama taifa ni "kuwakataa wabarikiwa" kwa kutokuwa na uhusiano nao wa kiserikali, kwa hiyo tumekosa Baraka zake pia.

  -Tuna kila rasilimali ambazo hazipo popote duniani lakini bado tu masikini wa kutupwa!
  -Nchi hii kila msomi anapoingia serikalini kwa mlango wa CCM akili inageuka na kuwa aidha mwizi au fisadi ama mhongwaji!
  -Nchi iliyo gubikwa na imani potofu za kishirikina na ulozi!
  -Nchi ya serikali inayo fikiri kwa upeo wa miaka mitano tu!
  -Nchi yenye serikali inayoficha ficha kila kitu na kudandanya ili ukweli usijulikane hata kwa wananchi wake!

  Aibu jamani!
   
 20. M

  Mtemakuni JF-Expert Member

  #20
  May 14, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kweli ukipenda chongo huoni kengeza bali atadai hilo ndo jicho la mahaba..!! Pamoja na mateso yote wanayowafanyia majirani zao achilia mbali kuwaua, kuendelea kuimega ardhi yao kila siku ( rejea mipaka ya UN-1948) bado tu kunawatu insteady of kuombea wapatane na majirani zao bado wanaomba wazidishe uharamia wanaowafanyie wenzao...!! Kwa taarifa yako this world will never be fair if wayahudi wakiendelea na wanachokifanya sasahivi na anguko lao kuu linakaribia pindi watakapojaribu kuishambilia IRAN maana wameona baba zao US wanasita kuwaunga mkono sasa wanataka kujipeleka kichwa kichwa..!! Wamesahau mungu amekua akiwakanya kimatendo pindi wanapokosea na mapito yake huwa magumu kupindukia...!!! Kumbuka amani haipatikani kwa kuwatesa na kumgandamiza mwenzio bali ni kupandikiza chuki ya milele kwa vizazi na vizazi..!!:smow:
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...