py thon
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 2,471
- 4,424
Aliyekuwa kocha msaidizi wa simba Jackson mayanja ,amesema iwapo uongozi wa simba utaendelea kuingilia kazi za benchi la ufundi,wasijeshangaa yanga ikiendelea kupeta msimu huu kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.
Mganda huyo alisema kuwa ubora wa kikosi cha simba msimu huu unaweza kuzaa matunda ,ikiwamo kutwaa ubingwa msimu huu iwapo tu viongozi hawataingilia kazi za benchi la ufundi .
Mayanja amesema kocha anatakiwa kufanya majukumu yake ya uwanjani na kuangalia kikosi chake anachokiamini na kuona wachezaji ambao watamfaa katika mechi hiyo kutokana na wapinzani anaokutana nao.
Amesema kama endapo watafanya hivyo ,hana shaka kabisa na ubingwa kwa msimu huu kwenda simba ,lakini kama uongozi utaingilia majukumu ,ana imani ubingwa utakuwa ni historia na mashabiki wa timu ya simba watajikuta wakiendelea kulizwa na watani wao wa jadi ,yanga.
Aliendelea kusema simba ina wachezaji wazuri na wenye uzoefu mkubwa wa michuano mikubwa,hivyo anaamini kila mmoja akifanya majukumu yake timu hiyo itafikia malengo ya kutwaa ubingwa.
Mayanja kaondoka kwa kile kinachodaiwa matatizo ya kifamilia lakini kilio chake angependa kuona viongozi wa timu wakiendeleza mikakati yao huku wakiwaachia bench la ufundi linaloongozwa na Omog kufanya majukumu yao kwa Uhuru bila kubughudhiwa.