Mayai ya Pasaka yanamaanisha nini?

Mayai ya Pasaka yanamaanisha nini?

Shaka-Zulu

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2018
Posts
432
Reaction score
831
Heri ya sikukuu ya Pasaka kwenu wakuu!

Siku kuu za kikristo zina symbolism za kipekee - Christmas ina Santa Claus na mti wa krismasi! Easter ina yai na pia kuna sungura (Easter bunny). Nasikia pale White House kila Easter watoto wanaalikwa kwenye shindano ya kutafuta mayai! Wazungu wanadesturi ya kutoa zawadi ya chocolate eggs wakati wa Easter.

Ningependa wajuzi watujuze hii Easter Egg na Easter Bunny ina maana gani?
 
kitabu Britannica kinasema kwamba desturi nyingi za sikukuu ya Ista “hazihusiani” na ufufuo wa Yesu “bali zinatokana na desturi za kale.” Kwa mfano, kitabu The Encyclopedia of Religion kinasema hivi kuhusu matumizi maarufu ya mayai na sungura wakati wa sikukuu ya Ista: “Yai linawakilisha uhai mpya unaotokea baada ya kuvunjika kwa gamba la yai.” Kitabu hicho kinaongeza hivi: “Sungura ni mnyama aliyejulikana kuwa na uwezo mkubwa wa kupata watoto, na hivyo aliwakilisha mwanzo wa majira ya masika.”

Philippe Walter, profesa wa uandishi wa enzi ya kati, anaeleza jinsi desturi hizo zilivyokuja kuwa sehemu ya sikukuu ya Ista. Aliandika kwamba “katika jitihada za kuwageuza wapagani kuwa Wakristo,” ilikuwa rahisi kuhusianisha sherehe ya wapagani ya kusherehekea “mwisho wa msimu wa baridi kali na mwanzo wa msimu wa masika,” na kufufuliwa kwa Yesu. Profesa Walter anasema kwamba hiyo ilikuwa hatua muhimu ya kuziingiza “sherehe za Kikristo” kwenye kalenda za matukio ya wapagani na hivyo kuwashawishi wapagani wengi iwezekanavyo wajiunge na Ukristo.

Jitihada hiyo ya “kuwageuza wapagani kuwa Wakristo” haikufanyika mitume walipokuwa hai, kwa sababu walikuwa “kizuizi” dhidi ya mafundisho ya wapagani. (2 Wathesalonike 2:7) Mtume Paulo alitoa onyo kwamba baada ya yeye “kuondoka . . . watu watasimama na kusema mambo yaliyopotoka ili kuwavuta wanafunzi wawafuate wao wenyewe.” (Matendo 20:29, 30) Pia, mwishoni mwa karne ya kwanza, mtume Yohana alizungumzia kuhusu watu fulani ambao walikuwa wakiwapotosha Wakristo. (1 Yohana 2:18, 26) Hilo lilifanya desturi za wapagani zienee upesi.

17883700_903622603110268_349407304691007854_n.jpeg
 
Mara nyingi Wanaochunguza maandiko na wasiopenda kuburuzwa na Mapadri wameuliza ya kwamba ule mkate mdogo kama sungura (bunny rabbit) na yai la Ista (Easter egg) vina uhusiano gani na ufufuo wa Kristo.

NAKUJIBU HIVI...

Kusema kweli, havina uhusiano wo wote na [ufufuo] huo. Sungura alichaguliwa kwa sababu alikuwa anazaa sana. Yai pia lilichaguliwa kwa sababu lilikuwa nembo ya kuzaa sana. Hata nembo hizo zenyewe, mkate mdogo kama sungura na mayai, vinatunzwa kama ukumbusho wa asili yake ya kipagani [ya siku hiyo]. Mifano hii imetolewa ili kuonyesha tu jinsi ilivyokuwa rahisi kwa Mwovu kulazimisha mawazo yale ya kipagani juu ya kanisa lile.

Swali linakuja mawazoni mwetu, Hivi ni kweli tunaifuata Biblia katika mafundisho yetu yote ya dini? Iwapo MAPOKEO na DESTURI za kipagani zimeweza kuteleza kwa urahisi na kuingia kanisani, ni vipi kuhusu mafundisho mengine ya dini?

Hatuna amri yo yote kuhusu uadhimishaji wa ufufuo au kuzaliwa kwa Kristo. Tunaweza kutafakari juu ya ufufuo Wake na kuzaliwa Kwake kwa wakati wo wote ule na katika siku yo yote ile ya mwaka.

366.jpeg
 
Hii haina ukweli wowote, ni imani potofu za kipagani zinazolenga koteza maana halisi ya Pasaka. Pasaka ya Bwana inaonekana kuanzia wana wa Israel walipokuwa wanaandaliwa kuondoka Misri. Na hata pale Mungu anapomwamuru Musa anyooshe fimbo juu ya bahari ya Sham na maji yakajitenga ili Waisrael wapite, ilikuwa ni Pasaka pia, ambayo niliendelea kuadhimishwa muda mrefu hata kabla Kristu na Ukristu kuja. Na siku ile ya Alhamisi Kuu Bwana Yesu alipokuwa anawaandaa na kuwaaga wanafunzi wake kwa ajili ya kuteswa kwake na hatimaye kufa na kufufuka, alikula nao Pasaka ya Bwana.

View attachment 1077298
 
Pasaka ya kwenye biblia ndio hii easter? Nan kakudanganya ?
 
Hii haina ukweli wowote, ni imani potofu za kipagani zinazolenga koteza maana halisi ya Pasaka. Pasaka ya Bwana inaonekana kuanzia wana wa Israel walipokuwa wanaandaliwa kuondoka Misri. Na hata pale Mungu anapomwamuru Musa anyooshe fimbo juu ya bahari ya Sham na maji yakajitenga ili Waisrael wapite, ilikuwa ni Pasaka pia, ambayo niliendelea kuadhimishwa muda mrefu hata kabla Kristu na Ukristu kuja. Na siku ile ya Alhamisi Kuu Bwana Yesu alipokuwa anawaandaa na kuwaaga wanafunzi wake kwa ajili ya kuteswa kwake na hatimaye kufa na kufufuka, alikula nao Pasaka ya Bwana.
Usichanganye pasaka (passover) Ya biblia na easter sikukuu ya kipagani kutoka babeli,

SIKILIZA KWA MUJIBU WA BIBLIA ....

Basi, kabla ya sikukuu ya pasaka ,Yesu,hali akijua kwamba saa yake imefika,atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba,naye amewapenda watu wake katika ulimwengu,aliwapenda upeo,Yesu hali akijua ya kwamba Baba amempa vyote mikononi mwake,na ya kuwa anatoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,aliondoka chakulani,akaweka kando mavazi yake,akatwaa, kitambaa akajifunga kiunoni.Kisha akatia majia katika bakuli,akaanza kuwatawadha miguu na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga….Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena,akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu,nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo KUTAWADHANA miguu ninyi kwa ninyi...Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. YOHANA 13:1-151

Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,Naye akiisha kushukuru akaumega, akasema,Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa UKUMBUSHO wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa UKUMBUSHO wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, MWAITANGAZA MAUTI YA BWANA HATA AJAPO WAKORINTHO 11:23-26

KUHUSU (EASTER) SASA AMBAYO UMEDANGANYWA NDIO PASAKA(PASSOVER)

Easter Ni sherehe inayojulikana sana ambayo,inaadhimishwa na makanisa yetu ya siku hizi. Walakini hii pia ilisherehekewa na wapagani muda mrefu kabla ya ufufuo wa Kristo.

Siku zote Pasaka inaangukia Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu (full moon) mara tu baada ya jua kuwa kichwani kaskazini ya Ikweta (Equinox ---March 2l).Wapagani wale wa zamani za kale waligundua ya kwamba kila kitu kilionekana kupata uzima mpya mapema katika majira yale ya kuchipua (Spring), mara tu baada ya jua kupita mstari wa ikwinoksi (equinox) kaskazini ya Ikweta. Basi wakachagua siku moja katika majira ya kuchipua [Machi, Aprili, Mei] ili KUMHESHIMU mungu WA KIKE WA UZAZI. Siku ile ikatolewa kwa ISHTA (ISHTAR), mungu wa kike wa uzazi, kwa sababu ya uhai mpya na kukua kwa mimea ya asili.

Neno lilo hilo ISTA (EASTER) limeandikwa kwa herufi nyingine zisizokuwa za lugha yenyewe kutokana na jina la mungu huyo wa kike ISHTA (ISHTAR), ambaye ibada yake iliwekewa ukumbusho wake kwa kutumia sikukuu ya Ista (Easter) [Pasaka].
 
Mkuu AROON neno ISHTAR asili yake ni wapi!

Asili ya Easter

Rejea nukuu zifuatazo.

“Neno la kingeleza Easter na la kijerumani Ostere yote yanatokana na asili moja (Eostur, astur, Ostara, Ostar), ambalo kwa Wanorwei humaanisha msimu wa kuinuka (kukua) jua, msimu wa kuzaliwa upya. Neno hilo lilitumiwa na mababu zetu kuteua sikukuu ya maisha mapya katika majira ya vuli. Mzizi huo huo unaonekana kwa ajili ya mahali ambapo jua huchomoza (East, Ost). Neno Easter, harafu, kwa asili linamaanisha maadhimisho ya jua katika majira ya vuli (spring sun) ambayo yanazaliwa katika mashariki na kuleta maisha mapya juu ya nchi. Ishara hii ilihamishwa kuwa maana isiyo ya kawaida ya Pasaka (Easter) yetu, kwa maisha mapya ya Kristo aliyefufuka, aliye nuru ya milele isiyoumbwa. Kulingana na kifungu katika maandishi ya mtakatifu Bede Mpendwa, neno Easter mara kwa mara limeelezewa kama jina la mungu mke wa waingereza (Eostre)…...” –Francis X. Weiser,Handbook of Christian Feasts and Customs (New York: Harcourt, Brace & World, Inc., 1958), p. 211. Copyright 1952 by Francis X. Weiser.…Ostara.

“(Kama machi 21 lakini tarehe zinaweza kutofautiana kama siku mbili) pia inajulikana kama; Ikwinoksi ya majira ya vuli, Ostara, Alban Eiler, Esther, Eostre, Ostarun, startag’, Eastre, Eoastrae, Oestre Siku ya kwanza ya kweli ya kuchipuka. Mchana na usiku sasa zote ziko sawa katika urefu kama mungu kijana anavyoendelea kukomaa na kukua. Tunaanza kuona mashina ya ukuaji mapya na machipukizi yanayopanuka katika miti. Nishati inajenga kadri siku zinavyozidi kuwa joto pamoja na ahadi. Unaweza; unaweza kuiita Easter Sisi tunaiita Ostara [1 assays -56, 869 inasomeka]–Unaiita Easter (pasaka), sisi tunaiita Ostara na Peg Aloi. Jaribu hii wakati mwingine pamoja na watoto wako au mpwa kijana, mpya au binamu: Siku ya Ikwinoksi ya majira vuli muda mfupi tu kabla ya wakati halisi wa Ikwinoksi.” –-The Witches VoiceThe 8 Pagan Holidays

“Je nini maana ya neno Easter lenyewe? Siyo jina la Kikristo. Linachukua asili ya Ukalidayo katika paji lake la uso kabisa. Easter sio kitu kingine zaidi kuliko Astarte, moja ya majina ya Beltis, malikia wa mbinguni, ambaye jina lake, kama lilivyotamkwa na watu wa Ninawi, alikuwa kwa dhahiri anatambulikana hivyo sasa katika matumizi ya kawaida katika nchi hii. Jina hilo, kama Lyard alivyolipata katika makaburi ya Ashuru ni Ishtar.” –The Two Babylons, na Alexander Hislop, kilichochapishwa 1943 na 1959 katika U.S. na Loizeaux Brothers, Neptune, New Jersey, page 103.

“Hakuna dalili ya uadhimishaji wa sikukuu ya (Easter) katika Agano Jipya au katika maandiko ya mababa wa kanisa la mitume.” Mwanahistoria wa kanisa, Socrates amenukuliwa katika makala hiyo hiyo kama anavyoonyesha kwamba Bwana wala mitume wake hawakujiingiza katika kutunza siku hii. Anasema, “Mitume walikuwa hawana wazo la kuteua siku za sikukuu, lakini la kukuza maisha yasiyo na mawaa na ucha Mungu.” Anahusisha maadhimisho ya Pasaka na kanisa kwa kuendeleza matumizi ya zamani, “vile vile kama desturi zingine ambazo zimeanzishwa.” Wanamatengenezo wa kanisa la mwanzo kama vile Calvin na Knox walipinga kwa nguvu dhidi ya Pasaka ya Katholiki (Easter) kwa sababu ya asili yake ni ya kipagani. Uadhimishaji wa siku hiyo haukusherehekewa sana katika Marekani mpaka baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe. (Easter: Its Story and Meaning by Alan Watts; Babylon, Mystery Religion, Ralph Woodrow;Calvin Tracts; Knox’s History) –Encyclopedia Britannica, article “Easter”

“Wakati Waprotestanti walipokuja amerika ya kaskazini, waliiangalia sherehe ya Pasaka–na sherehe ya Krismasi–kwa kuzituhumu. Walijua kwamba wapagani walisherekea kurudi kwa majira ya vuli kwa muda mrefu kabla ya Wakristo kusherehekea Pasaka (Easter)…kwa miaka mbali mbali ya mwanzo ya maisha ya Ulaya katika Amerika ya kasikazini, walikuwa tu wachache, wengi wao katika upande wa kusini, waliipa kipaumbele sana Pasaka” Siyo mpaka baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoisha Waamerika wakaanza kusherekea sikukuu hii; Pasaka mwanzo ilikuwa desturi ya Marekani katika miaka ya 1870. Chakukumbukwa! ni koloni 13 za awali za amerika zilianza kama taifa la “Kikristo” kwa kilio cha “Hakuna Mfalme ila Yesu!” Taifa halikuadhimisha Pasaka ndani ya karne nzima ya kuanzishwa kwake. Je nini kilitokea kulibadilisha hili?” -A Children’s book about the holiday, Easter Parade: Welocome Sweet Spring Time!, na Steve Englehart, p 4-5

Wana wa Israeli pia waliangukia katika ibaada hizi za kipagani za “malkia wa mbinguni,” na walioka mikate kwajili ya kumtukuza.

Yeremia 7:18 “Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.”

“Ishtar alikuwa mama mkuu, mungu mke wa uzaaji na malikia wa mbinguni.” -Microsoft Encarta Multimedia Enyclopedia.

Harafu angalia kwa makini Ishtar “malikia wa mbinguni” ndiye yule yule Beltis, au Semiramis, au Astarte mungu mke wa Ashuru ambaye jina lake ni” (“Easter”). Jina jingine la mungu mke huyo ni “Asht-tart” ambalo kwa kiebrania ni “Ashtoreth.” Ibada ya Ashtorethi mfalme Sulemani aliingiza katika Israeli wakati amemwasi Bwana, na kusababisha Israeli imwache Bwana na kuleteleza uharibifu wa kitaifa.

kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake. (1 Wafalme 11:33). Leo pia ibada hii ya Ashtorethi imeingizwa kanisani na mapapa na kuleta uharibifu wa Kanisa la Kristo, Mungu hatanyamaza juu ya hili, bali atachukua hatua kama alivyochukua hatua kwa Israeli ya zamani. Jipone nafsi kwa kuachana na upagani huu.

“Nini maana ya neno Easter lenyewe? Siyo jina la Kikristo. Linachukua asili ya ukalidayo katika paji lake la uso kabisa. Easter siyo kitu kingine zaidi ya Astarte, moja ya majina ya Beltis, malikia wa mbinguni… mungu mke wa Ashuru, au Astarte, anatambulika kama Semiramis. By Athenagoras (Legatio, vol. ii. p. 179), na [by] Lucian (De Dea Syria, vol. iii. p. 382)…sasa, hakuna jina linaloweza kwa hakika zaidi kutoa picha ya sifa ya Semiramis kama malkia wa Babeli, kuliko jina la ‘Asht-tart,’ kwa maana hilo humaanisha “Mwanamke yule aliyefanya minara”…Ashturit, harafu…ni kwa wazi jina hilo hilo kwa kiebrania ni ‘Ashtoreth.'” -Alexander Hislops, The Two Babylons, pp 103, 307-308).

Majina yote haya Beltis, Semiramis, Easter(Pasaka), Astarte, ni majina ya mungu mke ambaye ni malkia wa mbinguni, na jina lake hili “Asht-tart” kwa kiebrania ni “Ashtoreth”. Na katika Biblia tunaona Mungu aliwakataza wana wa Israeli kuwa na sikukuu hizi za maashtorethi, au Easter

Waamuzi 3:11-13 “Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali…wakafuata miungu mingine, baadhi ya miungu ya watu wale waliokaa karibu nao pande zote…Wakamwacha Bwana, wakamtumikia Baali na Maashtorethi.”

1Samweli 7:3-4 “Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia Bwana kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee Bwana mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katikaMatendo 2:42 “Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.”

Wakatoliki waliingiza sherehe ya pasaka wakidai ni kwa ajili ya kuadhimisha ufufuo wa Yesu Kristo. Lakini kibiblia Wakristo huadhimisha Kifo na Ufufuo wa Yesu kwa njia ya ubatizo.

Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake….Warumi 6:3-5

Wakatoliki hudai kwamba ule mkate ni mwili halisi wa Yesu, na ile divai ni damu halisi kabisa ya Yesu, lakini huo sio ukweli. Mkate na divai ni viwakilishi tu, na sio vitu halisi. Kwa sababu kama ni hivyo Kristo pia katika Maandiko huwakirishwa kama mzabibu. Je Kristo ni mzabibu halisi kweli? Pia huwakirishwa kama kondoo, Je Yeye ni kondoo halisi kweli? Kulingana na kanisa Katoliki Yesu ni mti wa mzabibu, au kondoo halisi. Yeyote anayemruhusu Roho wa Mungu kumfundisha ataona wazi kwa macho ya kiroho kuwa huo si ukweli.

1Wakorinto 10:18-21 “Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.”

Kikombe au meza ya Bwana ni Agizo la Kristo la kumega mkate na kunywa divai.

Kikombe au meza ya shetani ni agizo la kanisa Katoliki la kuadhimisha Pasaka(Easter) sikukuu waliyosherehekea wapagani zamani kwa kuheshimu “ufufuo” wa jua, tamuzi au baali.

Ndugu hatuwezi kushiriki katika meza ya Bwana, na meza ya mashetani.

1Wakorintho 10:22 “Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?”
 
Nasadiki kwa Kanisa Moja takatifu Katoliki la Mitume. Jee, Unasadiki?
 
Heri ya sikukuu ya Pasaka kwenu wakuu!

Siku kuu za kikristo zina symbolism za kipekee - Christmas ina Santa Claus na mti wa krismasi! Easter ina yai na pia kuna sungura (Easter bunny). Nasikia pale White House kila Easter watoto wanaalikwa kwenye shindano ya kutafuta mayai! Wazungu wanadesturi ya kutoa zawadi ya chocolate eggs wakati wa Easter.

Ningependa wajuzi watujuze hii Easter Egg na Easter Bunny ina maana gani?
Hivi kumbe sikukuu ya Pasaka inaambatana na sungura na mayai! Duh! Pamoja na miaka yangu yote ya kuwa mkatoriki sijawahi kujua, kuona wala kusikia hiki kitu! Kweli Jf kisiwa cha maarifa.

Kwenye makanisa yetu huku mtaani vinawekwaga wapi (sungura na yai) kesho nikavichungulie! Maana jumatatu ya Pasaka kuna misa na naamini watakuwa hawajavitoa
 
Mkuu, hizi desturi za mayai na sungura pengine hutaziona makanisani kwa sababu huwa zinafanyika manyumbani. Na kama hazipo hapa kabisa pia ni jambo njema. At least inaonyesha kuwa hatukuiga kila desturi ya wazungu, na tumeikataa hii ya yai na sungura kusherehekea Pasaka!
 
Mkuu Aroon, asante sana kwa mchango wako iliyonielimisha. Kumbe wazungu wameendeleza desturi nyingi za kipagani huku wakiivalisha mavazi ya kidini! Kwenye culture ya wazungu huwezi kusherehekea Christmas bila ya mti wa christmas au Easter bila ya mayai ya Easter! Wazungu wameanza kuweka uzito zaidi kwenye miti na mayai kuliko ibada!!! Watoto wakiulizwa kuhusu Christmas wanafikiria zawadi ya Christmas na miti, na Easter ni mayai ya chocoleti! Ingawa hizi desturi hazijafika hapa kwetu, Utandawazaji inazileta karibu! Lakini wafanyabiashara pengine watafurahia!

Mara nyingi Wanaochunguza maandiko na wasiopenda kuburuzwa na Mapadri wameuliza ya kwamba ule mkate mdogo kama sungura (bunny rabbit) na yai la Ista (Easter egg) vina uhusiano gani na ufufuo wa Kristo.
NAKUJIBU HIVI...
Kusema kweli, havina uhusiano wo wote na [ufufuo] huo. Sungura alichaguliwa kwa sababu alikuwa anazaa sana. Yai pia lilichaguliwa kwa sababu lilikuwa nembo ya kuzaa sana. Hata nembo hizo zenyewe, mkate mdogo kama sungura na mayai, vinatunzwa kama ukumbusho wa asili yake ya kipagani [ya siku hiyo]. Mifano hii imetolewa ili kuonyesha tu jinsi ilivyokuwa rahisi kwa Mwovu kulazimisha mawazo yale ya kipagani juu ya kanisa lile.
Swali linakuja mawazoni mwetu, Hivi ni kweli tunaifuata Biblia katika mafundisho yetu yote ya dini? Iwapo MAPOKEO na DESTURI za kipagani zimeweza kuteleza kwa urahisi na kuingia kanisani, ni vipi kuhusu mafundisho mengine ya dini?
Hatuna amri yo yote kuhusu uadhimishaji wa ufufuo au kuzaliwa kwa Kristo. Tunaweza kutafakari juu ya ufufuo Wake na kuzaliwa Kwake kwa wakati wo wote ule na katika siku yo yote ile ya mwaka.
View attachment 1077302
 
Back
Top Bottom